KATIBA YA KIKUNDI
KATIBA YA VACK GROUP
SEHEME YA 1. UTANGULIZI
1 JINA LA KIKUNDI VACK GROUP
IBARA YA PILI: 2: TAFSIRI YA MANENO MBALIMBALI
2.1 Kikundi kina mkusanyikon wa watu
2.2 Wanachama wa kikundi wana mtazamo moja
2.3 Wanadhamira moja katika kujenga taifa
IBARA YA 3. UTANGULIZI
Wanachama wa kikundi cha VACK GROUP tumejipanga kufanya kazi kwa ushirikiano ili kufikia malengo yetu
IBARA YA 4. KATIBA
Katiba ni kanuni ya nchi au taasisi iliyopangwa kwa makubaliano maalumu yanayosimamia sheria kufuata miongozo yake bila kwenda kinyume.Kwenda kinyume cha hapo ni kosa.
IBARA YA 5. JINA LA KIKUNDI
Kikundi kinaitwa VACK GROUP
IBARA YA 6. LUGHA RASMI YA KIKUNDI
Lugha rasmi ya kikundi ni Kiswahili na kingereza.
IBARA YA 7. OFISI KUU
Makao makuu ya kikundi yatakua ndani ya Mbinga mjini.
IBARA YA 8. ENEO LA UTENDAJI WA KAZI
Itakuwa ndani ya wilaya ya mbinga
IBARA YA 9. KANUNI ZA KIMAADILI
9.1 Kuheshimiana wenyewe kwa wenyewe na viongozi wa kikundi
9.2 Kufuata matamko yaliyowekwa na viongozi waliowekwa kisheria
9.3 Mwanachama atakaye kiuka kanuni na taratibu zilizowekwa na kikundi atapata adhabu kulingana na mkutano wa chama
9.4 Endapo mwanachama atajihusisha kakita suala la wizi wa fedha za kikundi atafikishwa katika vyombo vya dola.
9.4 Kiongozi atakayetumia madaraka vibaya ataonywa kwa kosa la kwanza na pili na la tatu atasitishwa uongozi kupisha uchunguzi ufanyike endapo atabainika anakosa hatua kali za kisheria zitachukuliwa.
9.5 Mwanakikundi asiyehudhuria shughuli za kikundi mara tatu mfululizo ataonywa na mara ya tatu ataondolewa uanachama.
SEHEMU YA III: DIRA,DHAMIRA,MADHUMUNI,ULINZI WA KIKUNDI
IBARA YA 10.DIRA
Kutokomeza kabisa umasikini
IBARA YA 11. DHAMIRA
11.1Dhamira ya kikundi ni kutoa elimu ya ujasilimali mfano,kuandaa matamasha ,kutoa elimu juu ya magonjwa mbalimbali mfano HIV,Malaria n.k ,Elimu ya biashara ndogo ndogo na kilimo .Kwa kufanya hivyo tutaweza kuongeza kipato na kujitangaza zaidi ili kufikia lengo la sera ya mheshimiwa Raisi wa nchi Mh. JOHN POMBE MAGUFULI Tanzania ya viwanda.
IBARA YA 12.MADHUMUNI YA KIKUNDI
Kuboresha maisha ya wanakikundi kwa kujishughulisha na shughuli za ujasiriamali ambazo ni:
I. Kutafuta masoko ya bidhaa kama nguo, vifaa vya umeme na vitu vya thamani
II. Ufugaji wa mifugo mbalimbali mfano kuku
III. Kuwaelimisha vijana kujihusisha na ujasiriamali kwa kuwatengenezea mazingira rafiki mfano machinga
IV. Kutoa elimu juu ya maambukizi ya virusi vya ukimwi
V. Kutoa elimu juu ya utunzaji mazingira
IBARA YA 13. KANUNI NDOGONDOGO ZA KIKUNDI
Kutumika kwa kanuni na adhabu za sheria zilizopo za serikali za jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia utawala bora wa sheria.Sheria zilizopo zitatumika kuazibu makosa yatakayofanyika ndani ya kikundi
13.1 Kupoteza mali ya kikuindi atalipa kulingana na thamani ya mali hiyo
13.2 Kuchelewa kwenye vikao au kutohudhuria muda uliopangwa
SEHEMU YA IV. UWANACHAMA NA AINA YA UWANACHAMA
IBARA YA 14. UWANACHAMA
14.1 Awe mkazi wa mbinga
14.2 Awe na akili timamu na awe mwenye kuamini dini yeyote
14.3 Awe na umri kuanzia miaka
18 14.4 Awe na akili timamu
IBARA YA 15. HAKI ZA MWANACHAMA
15.1 Kuchagua au kuchaguliwa kuwa kiongozi
15.2 Kupata taarifa za maendeleo ya kikundi
15.3 Kushiriki katika kutoa maamuzi ya kikundi
15.4 Kujadili au kuhoji taarifa mbalimbali za kikundi
15.4 Kupata gawiwo sawa linalotokana na faida za kikundi
IBARA YA 16. UKOMO WA MWANACHAMA
16.1 Kufariki.
16.2 Kujihudhuru mwenyewe kwa hiari na uhalali(ili mwanachama aweze kujitoa kwenye kikundi lazima pawepo na makubaliano ya wanakikundi wote katika mkutano mkuu).
IBARA YA 17. WAJIBU WA MWANACHAMA
17.1 Kuheshimu na kutekeleza katiba.
17.2 Kushiriki mikutano yote inayohusika.
17.3 Kuchanga mchango,ada,viingilio na masuala yoyote yanayohusika katika kikundi.
17.3.1 Kiingilio katika kikundi Tsh. 5,000/=
17.3.2 Mchango wa mwanakikundi kwa kila mwezi ni Tsh. 10,000/= (Lazima)
17.4 Kuheshimu na kutii maamuzi ya kikundi.
17.5 Kuhudhuria mafunzo ya ujasiliamali inapobidi.
SEHEMU YA V: MUUNDO WA UONGOZI
IBARA YA 18. MWENYEKITI
IBARA YA 19. KATIBU
IBARA YA 20. MWEKA HAZINA
SEHEMU YA VI: MAMLAKA YA VIONGOZI
IBARA YA 21. MWENYEKITI
Mwenyekiti anachaguliuwa na wanachama na kuwekwa madarakani kwa muda uliokubaliwa na wanachama. Wajibu wake ni:
21.1 Msimamizi wa shughuli zote
21.2 Atasimamia na kuendesha mikutano
21.3 Atasibitisha maamuzi ya vikao kwa kutia sahihi kama kutakuwepo na mabadiliko mbalimbali ya katiba
IBARA YA 22. KATIBU
Katibu atachaguliwa pasipo kuvunja katiba ya kikundi kwa muda uliokubaliwa na chama. Wajibu wake ni:
22.1 Mtendaji mkuu wa kikundi.
22.2 Kuandaa ajenda mbalimbali na vikao vilivyofanywa na kikundi.
22.3 Kutia sahihi hati za kumbukumbu na kutoa matangazo ya kikundi.
IBARA YA 23. MWEKA HAZINA
23.1 Msimamizi wa mali zote za kikundi
23.2 Kutunza pesa na hati zote za kumbukumbu za pesa za kikundi
23.3 Kutia sahihi za kumbukumbu zote za taarifa za pesa za kikundi
23.4 Kuandika bajeti na kuhakiki fedha zote zinatumika ilivyopangwa
23.5 Kukisaidia kikundi kuongeza vyanzo vya mapato
IBARA YA 24.UKOMO WA UONGOZI
24 .1 Kufariki
24.2 Akijihudhuru mwenyewe kwa hiari
24.3 Akishtakiwa na mahakama au kukutwa na makosa
24.4 Akipata maradhi ya muda mrefu
24.5 Muda wake ukifika
SEHEMU YA VII:MIKUTANO YA KAWAIDA NA DHARURA
IBARA YA 25 MKUTANO WA KAWAIDA
25.1 Kupata taarifa na mirejesho ya vikundi
IBARA YA 26. MKUTANO WA DHARURA
26.1 Kutoa taarifa haraka kama kuna dharura
IBARA YA 27.MKUTANO MKUU
27.1 Kutoa taarifa ya maendeleo kwa muda wote kikundi kilivyokuwa kinafanya shughuli za maendeleo
27.2 Kubuni vyanzo vya mapato na njia za ukusanyaji wa fedha katika kikundi
SEHEMU YA VIII: UTUNZAJI,VYANZO, NA MATUMIZI YA FEDHA
IBARA YA 28. UTUNZAJI WA FEDHA
28.1 Mwenyekiti , Katibu na Muhasibu wataandaa bajeti na kukabidhi kwenye mkutano wa kikundi 28.2 Viongozi watatakiwa kutoa muongozo wa mapato na matumizi kwa mwaka mzima
IBARA YA 29. VYANZO VYA FEDHA
29.1 Viingilio,mchango na hisa
29.2 Mapato yanayotokana na shughuli za kikundi
29.3 Mikopo kutoka taasisi za fedha na serikali
IBARA YA 30. MATUMIZI YA FEDHA
Pesa zitatumika kutokana na makubaliano ya kikundi katika kundeleza mipango ya kikundi
IDARA YA 31.UENDESHAJI WA AKAUNTI YA BENKI
30.1 Kikundi kitafungua akaunti ya banki
30.2 Watia sahihi watakuwa wafuatao mwenyekiti ,mwasibu,katibu na mjumbe mmoja
30.3 Fedha zitachukuliwa benki na watiasahihi wawili au wane wanaotambuliwa na Benki
.
IBARA YA 32. UTHIBITI NA UKAGUZI WA PESA
32.1 Ukaguzi wa pesa utafanyanywa 32.2 Mkaguzi huyo atachaguliwa na mkutano mkuu
SEHEMU YA 9.
MABADILIKO YA KATIBA ,KUVUNJIKA KWA KIKUNDI ,MHURI WA KIKUNDI
IDARA YA 33.MABADILIKO YA KATIBA
Marekebisho ya katiba ya tafanywa na wanakikundi wote
IBARA YA 34. KUVUNJIKA KWA KIKUNDI
34.1 Serikali au wadhamini kuvunja kwa sababu za msingi.
34.2 Kukua kwa uchumi kwa wanachama itapelekea kuvunjwa kikundi na kuanzishwa kampuni.
IBARA YA 35. MUHURI WA KIKUNDI
35.1 Kikundi kitatakiwa kuwa na muhuri ambao utatumika katika nyaraka mbalimbali
35.2 Muhuri utatunzwa na mwenyekiti wa kikundi mahali salama
35.3 Muhuri huo utaonekana hivi:
SEHEMU YA X: MENGINEYO
IBARA YA 36: UTATUZI WA MIGOGORO
36.1 Kamati ya utendaji wa kikundi na viongozi ndio wenye dhamana ya kutatua migogoro
36.2 Mwanakikundi mwenyewe atafikisha malalamiko mbalimbali kwenye kamati siku saba kabla ya mkutano
36.3 Siku maalumu ya kusikiliza malalamiko na migogoro itapangwa nza kamati ya utendaji
IBARA YA 37.HITIMISHO
Sisi ambao majina yetu yapo hapo chini ni waanzilishi wa kikundi cha
VACK GROUP
JINA MWANCHAMA WASIFU SAHIHI
1 GODLUCK H. KAWONGA MWANYEKITI
2 GEOFREY MATEMBO MUHASIBU
3 FESTO GERMANUS MBWILO KATIBU
4 GOODLUCK LUPEMBE MWANACHAMA
5 ANDREW MAPUNDA MWANACHAMA
6 JANUARY MAPUNDA MWANACHAMA
7 SHARIF MALKI MWANACHAMA
8 DICKSON HYERA MWANACHAMA
9 KERBIN NDUNGURU MWANACHAMA
10 FIRBETH NDOMBA MWANACHAMA
11 PROSPER NDIWU MWANACHAMA
12 CHESTER B. KAPINGA MWANACHAMA
13 STEVEN KOMBA MWANACHAMA
14 MELKION MKWELA MWANACHAMA
nzuri sana
ReplyDeleteASANTEEE
DeletePia
ReplyDeleteWana
*VICOBA TEMPLATE*
Tunapatikana kupitia link ZIFUATAZO
1. https://is.gd/Xz8omc
2. https://facebook.com/events/s/promotion-ya-mfumo-wetu/289315515570843/
Karibuni WANAKIKUNDI tuna mfumo wetu mzuri utakao warahisishia kazi zenu zote za kikundi. KARIBUNI