: kwa kutumia mifano jarabati eleza kwa utondoti tofauti iliyopo baina ya isimu elekezi na isimu elezi
.
Isimu
ni ‘taaluma yauchunguzi wa lugha kisayansi’. Ipo taaluma kama vile ya Falsafa
ambayo nayo inaweza kujishughulisha na uchambuzi wa masuala ya lugha lakini si
kwa kutumia vigezo vya kisayansi. Wanaisimu huhakikisha kuwa wakati wa kutafiti
na hatimae kuwasilisha matokeo ya utafiti wao wanatumia vigezo vya kisayansi
hatua kwa hatua. Kwanza huchunguza na kukusanya data, Halafu, wanafanya malinganisho
kabla ya kuunda nadharia na kuzipima nadharia na kuonyesha matokeo yake.Baadaye
hujiundia nadharia na kutoa kanuni ambazo zinapimika.
Isimu imegawanyika katika
matawi mbalimbali, miongoni mwa matawi hayo ni pamoja na matawi mawili ambayo ni isimu elekezi na isimu
elezi kama yafuatavyo.
Uelekezi (isimu elekezi).
Huu ni mtazamo unaojaribu kuweka kanuni
za usahihi wa namna watu wanavyotakiwa kutumia lugha. Isimu hii ilianzishwa
katika kipindi cha mapokeo ambapo wanaisimu waliwekeza kwenye sheria na kanuni
za kuzingatia watumiaji wa lugha wanavyotakiwa kutumialugha hiyo wakati wa
kuandika na kuzungumza. Sheria na kanuni hizo ni pamoja na muktadha, mada, wahusika,
jinsia, na umri.
Isimu elezi.
Uelezi au ukipenda (isimu elezi) ni
mtazamo ambao huelezea ukweli wa lugha jinsi ilivyo na inavyotumika na jamii
lugha husika na wala sio namna inavyotakiwa kutumika. Isimu elezi haiweki
kanuni ngumu au sheria ngumu zozote zinazotokana na mawazo ya mtu juu ya lugha
fulani bali huelezea lugha kwa kuangalia namna lugha hiyo inavyojidhihirisha
yenyewe. Huelezea sheria na kanuni ambazo mwanajmaii wa lugha ameziweka
kichwani na zinazoakisi uwezo wake wa lugha. Kwa kifupi, haielezi wala kuagiza
namna mtu anavyotakiwa kutumia lugha bali namna lugha ilivyo na inavyotumika na
wamilisi wa lugha hiyo.
Pamoja na yote kuwa ni matawi ya
isimu lakini matawi haya yametofautiana kwa namna moja ama nyingine. Tofauti
iliyopo baina ya isimu elekezi na isimu elezi.
Isimu elekezi
hii hujaribu kuweka sheria na kanuni za matumizi sahihi ya lugha ili watumiaji
wa lugha walazimike kuzitumia sheria hizo, wakati wa sarufi mapokeo
wagreek na wanawima wengine walielezea
safuri ya lugha kwa kuegemea matumizi sahihi jinsi ya kuizungumza na kuiandika,
wanaoshikilia mtazamo wa wanaotumia kigezo cha maana katika kutathimini usahihi
wa kusema. Kwa mujibu wa wanasarufi elekezi neno huelezea kwa kuzingatia kigezo
chenye maana, hivi kwamba ni kipashio chenye maana moja. Wanazingatia neno na
maana yake bila kuhusisha muktadha aidha hawakutoa maelezoya kutosha kuhusu
uchanganuzi wao wa lugha walizingatia andishi na hivyo maelezo yao yaliegemea
katika sarufi maandishi. Lakini mkabala
huu wa isimu una udhaifu wake kama ifuaatavyo.
-
waliegemea katika lugha ya maandishi na kusahau lugha ya mazungumzo,
-hawashughulikii
miundo mbalimbali ya sentensi,
-wanasisitiza
maneno bila kujali amilifu gani katika sentensi,
-huzingatia
maana bila muktadha siyo sahihi mfano mbuzi.
Lakini, Isimu
elezi ni mtazamo wa isimu unaozingatia umuhimu wa kuchambua vipemgele vya
lugha kama vilivyo, hii hujikita katika kutoa maelezo ya muundo wa lugha na
kila lugha ina miundo yake inayojitokeza kupitia ruwaza zinazo bainika bayana.
Lengo la wanaisimu elezi ni kuchunguza uhusiano wa vipashio katika sentensi na
kutumia mwelekeo wa uchunguzi wao kuigawa sentensi katika makundi mbalimbali
lama kirai nomino na kirai kitenzI (KN+ KT). Wanaisimu elezi walitumia vigezo
vifuatavyo katika kubainisha vipashio katika sentensi,
(a) Kutambulisha
uhusiano sambamba, ni kubainisha uhusiano wa maneno katika uhusiano sambamba
(ulalo) mfano. Mtoto huyu amechapwa (sentensi hii ipo sahihi imeanza na
kikundi nomino)
Kimevunjika kiti hiki (sentensi hii haipo
sahihi kwasababu
haijaaza na kikundi nomino)
(b)
Kutambulisha uhusiano wima, kutambulisha
uhusiano wa maneno na kuweka mazingira sawa ya kiwima. Mfano. Mtoto huyu amelala
Kiti hiki kimevunjika
Isimu
elezi ni msingi mwafaka katika uchanganuzi wa lugha kubainisha viamba jengo
katika sentensi. Mkabala huu unabainisha viamba jengo kwa kuzingatia maumbo ya
maneno na jinsi ya navyo husiana ndani ya sentensi, sentensi kwa kawaida
huundwa na mfatano viamba jengo au makundi ya maneno makundi hayo ndo huitwa
viamba jengo. Lakini pia mkabala huu wa isimu una udhaifu wake kama ifuatavyo,
Udhaifu
wa isimu elezi ni kwamba ni vigumu
kutumia mkabala huu kuchambua sentensi yenye utata kwasababu yenyewe imejikita
katika kuangalia muundo wa sentensi na sio maana ya sentensi, kwa mfano sentensi, ulifikaje hapa?
Kwa kuhitimisha,
tofauti kuu iliyopo baina ya isimu elekezi na isimu elezi ni kwamba isimu
elekezi imejikita katika sheria na kanuni za lugha lakini isimu elezi yenyewe
imejikita katika kutazama muundo wa sentensi, pamoja na hayo lakini yote ni
matawi ya isimu yanayoshughulika na sayansi ya uchunguzi wa lugha kama
tulivyoelzwa na wataalamu mbalimbali walivyoelezea maana ya isimu.
AAA TUKI (1990)Kamusi
sanifu ya isimu na lugha. Dar es salaam:
Mgullu,R.S
(1999).Mtaala wa isimu, fonetiki, fonolojia na mofolojia ya kiswahili, Nairobi Kenya,
longhorn publishers.
King’ei, K.
(2010).Misingi ya Isimu Jamii. Taasisi ya Taaluma za Kiswahili: Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam.
Comments
Post a Comment