Fasihi Simulizi
Fasihi Simulizi ,ni fasihi inayotungwa au kubuniwa
kichwani na kuwasilishwa kwahadhira kwa njia ya mdomo na vitendo bila kutumia maandishi
mulokozi( 1996).
Hivyo fasihi simulizii na
fungamana namuktadha au mazingira Fulani ya kijamii na kutawaliwa na mwingiliano
wa mambo kama vile fanani, hadhira, fani, tukio, mahali pamoja na wakati wa utendaji.
Ni aina ya fasihi ambayo hutumia mdomo katika kuumbwa,
kuwasilishwa na kusambazwa kwa wasikilizaji na watumiaji wake (Balisidya,
1983).
Fasilihi hii zinasisitiza
kwamba fasihi simulizi inategemea uwepo wafanani, hadhira, jukwaa na mada.
Hivyo kwa ujumla, tunaweza tunaweza kusema kuwa fasihi simulizi ni sanaa
inayotumia lugha kisanaa ili kufikisha ujumbe kwa hadhira iliyokusudiwa kwa
njia yam domo.
Msanii katika fasih isimulizi
ni mtu anayesimulia hadithi, methali, vitendawili au kucheza ngoma mbele za hadhira
.
Msanii ,mahiri, ni
fundi stadi mwenye akili timamu ,mwenye uwezo wa kueleza na kupanga fikra katika
njia ya hisia au zana. Anao uwezo wa kubuni sanaa za mitindo ya aina mbalimbali
kama vile kuchora, kuchonga kufinyanga kusuka na kufuma. Baraza la sanaa la
taifa( 1982).
Hadhira ni wapokeaji
,watazamaji,au wasikilizaji wakazi yafasihi . Katika fasihi simulizi hadhira wanahusiana
kwa karibu sana na msanii wakazi ya fasihi ssskiutendaji. Kwani utendaji wa fasihi
simulizi hukutanisha pamoja hadhira na fanani pamoja na kufanikisha kazi hiyo.
Kuna uhusiano wakaribu sana
baina ya fanani na hadhira katika fasihi
simulizi kama sifuatavyo:
Ushiriki
Hadhira anahusiana na fanani
kama ushiriki wa kazi yake kwani fanani anamtegemea hadhira katika utendaji wakazi
yake . fanani ili kufikisha ujumbe aliokusudia katika jamii lengwa anamtegemea uhusika
wahadhira katika vipengele mbalimbali mfano
, kupiga makofi, fanani anaetamba hadithi anaanza kwakushikisha hadhira yake
mfano:
Fanani :hadithi hadithi
Hadhira :hadithi njoo utamkolea.
Fanani: hapo zamani za kale………………
Hadhira: mmhhh
Kutokana na uhusiano huo
huipa fasihi simulizi sifa ya uhai kwani fanani na hadhira wanakuwa pamoja kiutendaji
tofauti na fasihi andishi ambapo hadhira yake haiusiki kabisa katika kazi husika.
Lakini katika tanzu mbalimbali ya fasihi simulizi hadhira wanahusika katika ushiriki
wao mfano katika kupiga makofi kusikitika
kucheka kuimba nyimbo au kujibu maswali hadhira
ikikoseka na fanani ni ngumu kufanya kazi yake hivyoo ni kweli kuwa kuna uhusiano
kati ya hadhira na fanani.
Utazamaji
Katika kufanikisha kwa kazi
ya fasihi simulizi kiutambaji jukwaani inatagemea pia kuwepo kwa hadhira ambao ndio
watazamaji wa kazi hio hadhira ikikosekana ni vigumu kufanikisha kwa kazi hio mfano
sanaa za maonyesho, ngoma, maigizo, utani, hutegamea kuwepo kwa watazamaji
wa matukio hayo kukosekana kwa watazamaji huondoa sifa ya fasihi simulizi hali hii
ndio hupelekea kukutanisha ana kwa ana baina ya fanan na hadhira hivyo msanii ana
uhusiano mkubwa na hadhira yake Kwani hutegemea hadhira kutazama kile kinafanyika jukwaani tofauti na fasihi andish itanzu kama riwaya ushairi hautegeme
I uwepo wa hadhira ana kwa ana kutazama kazi hio.
Suala
la fanani kuitambua hadhira yake.
Msanii wa fasihi simulizi
ni zao la jamii husika hivyo ana uhusiano na hadhira kwa kuwa yeye ni zao la
jamii hio hivyoo ingekuwa ngumu msanii kutamba hadithi ambae ninje ya jamii yake
na kutoa mifano kulinga na na mandhari hayo
kulingana na tajiriba ya jamii husika hivyo kutokana na msanii ni mjuzi wa
tamaduni husika ndio humwezesha msanii kuitawala
hadhira yake vizuri suala hili hudokeza uhusiano kati ya msani inahadhira katika
fasihisi mulizi tofautina fasihi andishi msani in ivigumu kuelewa tamaduni nahadhira
kwa sababu hadhira yake ni pana zaidi.
matumiziyaishara
Nalo linathibitisha uhusiano
uliopo baina ya msanii na hadhira kiutendaji kwani kutokana na kuwa na uhusiano
wa karibu humsaidia msani ipiakutumia lugha ya ishara mfano kutikisa kichwa,
kukonye za macho na kutikisa mabega ambaye humsaidia katika uwailishaji wake
kwa hadhira hali hii ni kwa sababu ya uhusiano baina ya msanii na hadhira kiutendaji
katika fasihi andishi kutokana na kukoseka na uhusiano huo msani ihawezi kutumia
ishara kumsaidia katika hadhira yake.
Uteuzi
wa matumizi ya lugha
Uhusiano wa msanii na hadhira ndio utakae muongoza katika uteuzi wa lugha ili kuitawala jamii yake kulingana na hadhi ya watu aliokuwa nao
mfano wazee atatumia lugha ya hekima na busara pia kwa vijana atatumia lugha ya
kihuni kulingana nao ili asiweze kuwa kwaza
na kuwaondolea hadhira hio umakini wakumfuatiliua kwani atakuwa anawakera hivyoo
kutokana na kuwepo kwa uhusiano huoina msaidia fanani kufanya kazi itakaopendwa
na kila mtukuto kanana uhusino huo.
Suala
la toni
Toni ni hali ambaea na kuwa nae
msani ipindianawa silishakazi yake mfano huzuni furaha hasira hali hio inakuwa na
uhusiano wa moja kwa moja mfano msani ianaposimulia hadithi za kuhuzunishawa kati
huo hadhira itawapelekea kuhuzuni kapia hata kutokwana machozi lakini msanii atakapotamba
kazi za kufurahisha mfano hadithi za abunuasi,atasababisha hadhira yake kufurahi
sana na kucheka hivyo toni ya msanii ndio inahusianawa moja kwa moja na toni ya
hadhira sa yake hivyo basi msani inahadhira wana uhusiano katika kazi ya fasihi.
Uwezo
wa msani ikuitawala hadhira yake.
Msanii anaweza kuwa ni
chanzo cha kufanya hadhira yake kuwa makini kufuatilia kazi yake kama atakuwa na
uwezo mkubwa wakuitawala mfano msanii anapoonyesha umahiri wake, kujiamini
,kutumia lugha ya ucheshi kiutendaji ataweza kuifanya hadhira yake kufurai na kuwa
makini wakati wote na kuwa na hamu ya kuendelea kumfuatilia msanii lakini kama msanii
atashindwa kuitawala hadhira yake atasabaisha hadhira kuchoka kwa haraka kisha kupoteza umakini wao wa kufuatilia tukio linalotendeka jukwani hivyo .msanii anapoona
hadhira yake inaanza kuchoka kufuatilia kazi
anakuwa huru kutumia mbinu mbalimbali ya kurudisha hadhira yake katika hali ya mwanzo
swala ambalo ningumu kufanyika katika fasihi andishi.
HITIMISHO
Hivyo katika utendaji wa
fasihi simulizi inahusisha kuwepo kwa fanani, hadhira ,tukio lenyewe na muktadha
wakufanyika tukio hilo . Kutokana na kukutana ana kwa ana kati ya msanii
na hadhira unajenga uhusiano mkubwa kati ya hadhira na msanii na ndio huipa fasihi
simulizi sifa ya uhai kwani fanani na hadhira wanahusiana katika kukamilisha kazi
hiyo.
MAREJEO
Baraza la sanaa la
taifa (1982) falsafayasanaatanzania . Dar- es-salama
Mhando,J. naBalisidya,
N. (1976) Fasihi , Tanzania
Publishing House, Dar es salaam.
Mulokozi, M.M. (1989:5)
“TanzuzaFasihiSimulizi” Katika MULIKA
Na. 21, D.SM.
Muhando, P
&Balisidya, N (1976) FasihinaSanaazaMaonyesho.
Tanzania Publishing
House(TPH) Dar es
Salaam.
Comments
Post a Comment