MKATABA WA KUPANGA NYUMBA
MKATABA
WA KUPANGA NYUMBA/ CHUMBA KATIKA NYUMBA YA BI ZAINABU MUSSA M’BISI ILIYOKO ENEO
LA KISUTU MTWARA MJINI.
Makubaliano
yaliyobainishwa hapo chini yamefanyika hapa Mtwara siku ya tarehe……….mwezi
wa…………….mwaka…………………
Baina ya
Bi Zainabu M. M’bisi ambaye
katika mkataba huu anajulikana kama mmiliki halali wa nyumba iliyoko katika
mtaa wa kisutu kiwanja namba…………………Mtwara.
Na
Bw/Bi………………………………………………….atakayejulikana
katika mkataba huu kama mpangaji kwa mwenye nyumba kwa kuwa nia ya mwenye
nyumba ni kupangisha watu/mtu katika nyumba yake, kwa mpangaji aliyetajwa hapo
juu ambaye ameomba apate nafasi ya chumba/ nyumba hii. Kwa kuwa mpangaji
ameomba apange chumba/ nyumba kwa matumizi ya kuishi/ kulala humo na mwenye
nyumba amekubali kumpangisha mpangaji kama alivyoomba.
Hivyo basi kwa mkataba
huu pande zote mbili zimekubaliana kama ifuatavyo;-
1. Kwa
malipo ya pango yaliyoainishwa hapa chini mwenye nyumba anampangisha mpangaji
chumba/ nyumba.
2. Kipindi
cha upangaji kwa mujibu wa mkataba huu ni muda wa miezi sita (6), kuanzia
tarehe……….. mwezi wa………………..hadi tarehe…………. Mwezi wa…………….. na iwapo mpangaji
anataka kuongeza kipindi kingine cha upangaji anatakiwa kumtaarifu mwenye
nyumba miezi miwili kabla ya kipindi cha mwanzo kumalizika na kulipa upya.
Asipofanya hivyo mwenye nyumba/mmiliki wa nyumba ana uhuru wa kumpokea mpangaji
mwingine na kumpangisha ili aingie chumba hicho kwa kuzingatia makubaliano ya
mkataba uliopo kati ya mwenye nyumba/mmiliki wa nyumba na mpangaji unasemaje.
3. Upande
wowote unaweza kukatisha mkataba huu kwa kutoa ILANI (Notice), isiyopungua
miezi tatu (3) kwa upande mwingine.
4. Imekubaliwa
na pande zote mbili kwamba kodi ya kila mpangaji itakuwa kiasi cha shilingi
Elfu ishirini na tano tu.Tsh.(25000/=) kwa mwezi ambazo zinapaswa kulipwa kwa
mara moja kwa hesabu ya miezi sita (6) kabla ya kupewa/ kukabidhiwa chumba.
malipo
ya gharama za umeme na maji ni juu ya mpangaji/wapangaji kulipia katika ofisi
husika kwa kuchangiana wao wenyewe kadiri ya matumizi yao katika nishati hizo
(Bill) watayoletewa kutoka ofisi husika.
5. Mpangaji/wapangaji
hawaruhusiwi kuchora/ kutoboatoboa kuta za nyumba na kubandika karakatasi kwa
gundi wala kubandika ukutani picha za magazeti.
6. Mpangaji/wapangaji
hawaruhusiwi kufanya marekebisho katika miundombinu ya umeme na maji.
7. Mpangaji
anapohama chumba/ nyumba kwa sababu yoyote ile anapaswa kuiacha nyumba/ chumba
katika hali ya usafi, haruhusiwi kubomoa au kung’oa kitu au sehemu ya jengo
husika au kufanya uharibifu wa aina yoyote ile.
8. Mpangaji
sharti/aweke saini ya makubaliano kuthibitisha kuwa anaipokea nyumba/ chumba
ikiwa safi na salama na chumba atakabidhiwa tu endapo mpangaji ameshakamilisha
malipo ya miezi sita (6) na kusaini mkataba huu. Nae pia anapomaliza muda wake
wa kuishi katika chumba / nyumba ataikabidhi nyumba/ chumba kwa mwenye nyumba
katika hali ya usafi mwisho wa mkataba huu au wakati wowote akitaka kuhama
kabla ya kufikia mwisho wa mkataba.
9. Mpangaji
haruhusiwi kupangisha chumba/ nyumba kwa mtu mwingine au kuingia ubia na mtu
mwingine au kumkabidhi mtu mwingine chumba/ nyumba kabla au baada ya kwisha
mkataba bila au pasipo idhini na kibali cha mwenye nyumba.
10.
Mpangaji haruhusiwi kuunganisha umeme
kwa njia zake nje ya soketi na holda zilizowekwa katika jengo kulingana na
ramani ya jingo. Haruhusiwi kutumia jiko la umeme.
11.
Endapo litatokea tatizo lolote lile
katika chumba/ nyumba mpangaji anatakiwa kutoa taarifa mara moja kwa mwenye
nyumba. Kwa mfano kuvuja kipindi cha masika.
12.
Mpangaji atagharamia mwenyewe
matengenezo ya vifaa vifuatavyo;- vitasa, kuungua balbu, kuharibika kwa bomba
la maji, kupoteza au kuvunja ufunguo, kuvunja madirisha, kuchimba shimo la taka. Matengenezo makubwa
na matatizo ambayo yanahitaji matengenezo kutokana na kimbunga, mvua kali au
hali ya hewa ya pekee sana yatafanywa na kulipwa na mwenye nyumba.
13.
Mpangaji/wapangaji watafanya/ atafanya
usafi kwenye chumba chake/ nyumba yake usafi wa juu na chini ya sakafu. Usafi
wa choo, bafu na kiwanja watapeana zamu. Taka kavu zichomwe moto shimoni na
zisizochomeka zitupwe shimoni.
14.
Mpanngaji akivunja sharti lolote la
mkataba huu mwenye nyumba atakuwa na haki ya kukatisha mkataba huu mara moja.
15.
Ulevi na kuvuruga wengine hakutakiwi
kabisa kwa mkaaji wa nyumba hii muziki wa redio, TV, simu ziwe na milio ya
chini/ sauti ndogo hasa muda wa usiku ili kuzuia kusumbua jirani zako unaoishi
nao ambao labda wamechoka na wanahitaji kupumzika kwa utulivu na ukimya.
16.
Kwa kuthibitisha yote yaliyotangulia
pande zote mbili zimeweka sahihi zao leo tarehe………. Mwezi………… mwaka…………… mbele
ya mwenyekiti wa mtaa wa kisutu na mashahidi wengine kama inavyoneka hapo
chini.
Jina la Mmiliki wa
nyumba…………………………….....Sahihi………………
Jina la
Mpangaji………………………………………..Sahihi…………………
Jina la msimamizi kwa
niaba ya mwenye nyumba……………………………Sahihi………….
Jina la shahidi wa
mwenye nyumba…………………………………….Sahihi…………………
Jina la shahidi wa
mpangaji………………………………………….Sahihi………………………
Jina la M/kiti wa mtaa
wa Kisutu..………………………………..…..Sahihi…………………..
Muhuri………………………………..
MALIPO
YA PANGO LA CHUMBA/ NYUMBA/ CHUMBA NA UKUMBI
Mimi………………………………………………..kwa
niaba ya Bi Zainabu M M’bisi nimepokea malipo ya pango la chumba na kiasi cha
……………………………………………………….. Tsh.(………………) kutoka kwa Bw./Bi…………………………………… malipo ya
miezi sita (6) toka tarehe ……………….. mpaka tarehe………………………… nyumba iliyoko
katika Mtaa wa Kisutu Kiwanja Namba 448.
Sahihi kwa niaba ya
mwenye nyumba.
Jina la
Mpokeaji……………………………………..Sahihi……………………
Jina la shahidi wa
mpokeaji…………………………………….Sahihi…………………..
Jina la Mpangaji/
Mlipaji…………………………………………Sahihi………………….
Jina la shahdi wa
mpangaji/ Mlipaji…………………………………..Sahihi………………
Tarehe…………………………….
Makabidhiano yote
yamefanyika na kusimamiwa na M/kiti wa Mtaa
wa kisutu.
Jina na sahihi ya
M/kiti wa Mtaa………………………………..... Sahihi……………….
Muhuri…………………………………
Comments
Post a Comment