mofolojia ni utanzu wa isimu ambao huchunguza , hupambanua na kuchanganua maumbo maneno na aina zak
UTANGULIZI
Kuna baadhi ya wataalamu
mbalimbali wamefafanua au wamefasili
dhana ya mofolojia kama ifuatavyo
Matinde (2012) anasema
kuwa mofolojia ni utanzu wa isimu ambao huchunguza , hupambanua na kuchanganua
maumbo maneno na aina zake.
Rubanza (1996:1) anasema
Mofolojia ni taaluma inayojishughulisha na vipashio vya lugha na mpangilio wake
katika uundaji wa maneno . Anaongeza
kwamba mofolojia huzingatia namna vipashio vinavyotumika katika kupangilia mfumo wa muundo wa maneno katika lugha.
Habwe na Karanja (2004)
wanasema kuwa"Mofolojia " Ni tafsiri ya neon la kiingereza
"Morphology" ambalo limetokana na na neno la kiyunani "Morphe
" lenye maana ya muundo au umbo, hivyo basi mofolojia ni neno linalotumika
kumaanisha kiwango cha isimu kinachoshughulikia muundo wa ndani wa maneno.
Kwa ujumla , Mofolojia
ni taaluma au kiwango cha isimu au sarufi ya lugha ambacho huchanganua
maumbo ya maneno katika lugha husika.
Hivyo mofolojia huchunguza muundo wa ndani na ule wa nje wa maneno katika lugha
fulani
MAWANDA YA MOFOLOJIA
Mofolojia ina mawanda
mawili ambayo ni
Mawanda ya mofolojia
minyambuliko ya maneno, tawi hili hushughulikia minyumbuliko mbalimbali ambayo
huwekwa kwenye mizizi ya maneno bila kubadili aina au kategoria ya neno, kwa
maana kwamba kama litakuwa ni kitenzi , hata baada ya mnayumbuliko neno hilo
litabaki kuwa kitenzi.
Mfano, -imb- imbia, imbisha, imbiana
-pig- pigia, pigisha, pigana, pigwa
Katika mifano hiyo
maneno yote yametokana na na mizizi {-imb-} na {-pig-} ni vitenzi , licha ya
kuwa na maumbo tofautitofautiyenye dhima
na maana tofauti.
Mawanda ya mofolojia ya
uundaji wa maneno, hili ni tawi la isimu maumbo ambalo hushughulikia michakato
mbalimbali ya uundaji wa maneno katika lugha husika. Kila lugha huwa na
utaratibu maalumu wa maneno. Tawi hili hushughulikia minyambuliko mbalimbali
ambayo huwekwa kwenye mizizi ya maneno na ama kubadili au kutobadili aina au
kategoria ya neno.
Mfano, Kitenz Nomino
Imba wimbo
Lima kilimo
Piga pigo
Ufuatao ni msigano wa
mawanda ya mofolojia kama ifutavyo:
Mofolojia minyambuliko
ya maneno haibadili aina au kategoria ya neno, kwani hushughulikia minyambuliko
mbalimbali ambayo huwekwa kwenye mizizi ya maneno bila ya kubadili neno hilo,
yaani kwamba maneno hubakia katika kategoria ileile ya mwanzo hata baada ya
kufanyiwa minyambuliko
Mfano, {chez-} chezea, chezesha, chezeana
{som-} soma, somesha, someana
Lakini mofolojia ya
uundaji wa maneno hubadili aina au
kategoria ya neno au maneno
Mfano,Kivumishi Kitenzi
Safi safisha
Dogo dogosha
Tulivu tuliza
Erevu Erevusha
Mawanda ya mofofolojia
minyambuliko ya maneno, viambishi huongezwa baada ya mzizi wa neno
Mfano, {lia-}, lilia,
liliana
{lim-}, limia, limisha, limiana
Lakini mofolojia ya
uundaji wamaneno, viambishi hupachikwa mwanzo au mwisho mwa mzizi wa neno
Mfano, {-chez-},
A-na-chez-a
Hivyo kiambishi A- huonesha nafsi , -na- njeo, -chez- mzizi ,
-a maana
Mofolojia minyambuliko
ya maneno huzalisha maumbo mbalimbali ya maneno yaliyo katika kategoria moja au
ileile
Mfano, Kimb- kimbiana, kimbizwa, kimbilia
Pit- pitiana, pitiwa, pitiana
Hivyo basi maumbo ya awali ni vitenzi lakini pia maumbo
yote yaliyozalishwa baada ya mnyambuliko ni vitenzi. Lakini katika mofolojia ya
uundaji wa maneno huzalisha maumbo mbalimbali yaliyopo kwenye kategoria tofautitofauti
Mfano, Kitenzi Nomino
Lia kilio au mlio
Cheza mchezo au mchezaji
Hakiki mhakiki
Utumwa mtumwa
Hivyo huo ni msigano
mojawapo wa mawanda haya mofolojia.
Mofolojia mnyumbuliko
wa maneno huwakilisha dhana mbalimbali kama vile njeo, nafsi, udogoshi,
ukubushi, hali, ukanushi, urejeshi, upatanisho wa kisarufi na idadi.
Mfano, njeo neno
Anakimbia linaonesha wakati uliopo.
Lakini mofolojia ya
uundaji wa maneno haiwezi kuwakilishwa dhana hizo, bali hubeba kategoria tu.
Mfano, Kitenzi kuwa
nomino
Pika Mpishi
Ubepari Bepari
Linda Lindo
Mofolojia ya uundaji wa maneno huhusisha kanuni mbalimbali
kama uyeyushaji, udondoshaji,
Mfano, uyeyushaji Nomino
Nomino
Muaka mwaka
Muembe mwembe
Udondoshaji Nomino
Nomino
Mutu mtu
Mufalme mfalme
Wakati mofolojia ya
minyumbuliko ya maneno haihusishi kanuni hizo, isiopokuwa ni utaratibu wa
kisarufi.
Hitimisho
Kwa ujumla mawanda ya
mofolojia yanamchango mkubwa katika lugha, kwani huongeza msamiati katika lugha
husika kwa kupitia kanuni mbalimbali hususani katika mofolojia ya uundaji wa maneno ambapo neno moja
hubadilika kuntoka kategoria moja hadi nyingine, kwani pia hata kwenye minyambuliko
husaidia kuongeza msamiati katika luha.
MAREJEO.
Rubanza, Y.T. (1996) Mofolojia ya Kiswahili. Dar es salaam:
Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania.
Habwe, J. &
Karanja, P. (2004) Misingi ya Sarufi ya
Kiswahili. Nairobi: Phoenex Press.
Matinde, S. (2012) Dafina Lugha, Isimu na Nadharia: Kwa
Sekondari, Vyuo Vya Kati n Vyuo Vikuu. Mwanza, Tanzania: Serengeti Publisher
Ltd.
Comments
Post a Comment