SWALI Fafanua kwa kina msigano wa mawanda ya mofolojia


SWALI  Fafanua kwa kina msigano wa mawanda  ya mofolojia
Kuna wataalamu mbalimbali wamejaribu kutoa fasili mbalimbali kuhusu dhana unominishaji na mnyumbuliko kama ifuatavyo;
Unominishaji Ni ule utaratibu wa kuunda nomino kutokana na maneno mengine ambayo si nomino. Lugha ya kiswahili huunda nomino nyingi kutokan na vitenzi, vivumishi na nomino yenyewe. (Mgulu 1999: 141).
Habwe  na Karanja (2004) wanasema kuwa Unominishaji ni hali ya kuunda nomino kutoka katika kategoria nyingine ya neno.
Kwa ujumla unominishaji ni kitendo cha kibadili kategoria mbalimbali za maneno kua nomino. Mfano wa kategoria hizo ni kitenzi kivumishi na nomino yenyewe.
Unyambulishaji ni utaratibu katika lugha wa kupachika au kuongeza viambishi kwenye mzizi wa neno ili kuunda maneno mapya ( Massebo 2012 : 127).
Unyambulishaji ni mbinu ya uundaji wa hivi kwamba viambishi mbalimbali huambikwa kwenye mzizi husika na kuunda neno jipya ( Matinde 2012:119).
Kwa ujumla, unyambulishaji ni kitendo cha kupachika au kuweka viambishi kwenye mzizi wa neno ili kuunda maneno mapya.
Ifutayo ni michakato ya unomiishaji ya minyumuliko geuzi ya kateria ya lugha ya kiswahili
Nomino Kutoka Kwa Vitenzi
Nomino za Kiswahili zinaweza kuundwa kutoka kwa vitenzi. Katika hali hii, viambishi awali na viambishi tamati vya umominishaji huambikwa kwenye mizizi au mashina ya vitenzi. Baadhi ya viambishi awali vya unominishaji ni kama vile: {mu}, {m}, {ki}, {u} na {Ø} na vya wingi ni {wa}, {vi}, {ma}, {u} na {Ø}. Kwa upande mwingine viambishi tamati vya unominishaji ni kama vile: {ji}, {zi}, {fu}, {o} na {i}. Ifuatayo ni michato mbalimbali ya unominishaji inayohusu mashina na mizizi ya vitenzi: Kutumia viambishi awali vya unominishaji {m} au {mu} katika umoja na {wa} katika wingi pamoja na shina la kitenzi na kiambishi tamati cha unominishaji {ji}.
{mu}
{m}     + {shina-T} + {ji}
{wa}
Kwa mfano
Kimbia{mu}+{imb}+{a}+{ji} > mwimbaji
Winda {mu}+{wind}+{a}+{ji} > mwindaji
Ua {mu}+{u}+{a}+{ji} > mwuaji
Cheza {mu}+{chez}+{a}+{ji} > mchezaji
Tangaza {mu}+{tangaz}+{a}+{ji} > mtangazaji
Chora {mu}+{chor}+{a}+{ji} > mchoraji
Kutumia kiambishi awali cha unominishaji {m} na {mu} pamoja na mzizi wa
kitenzi na viambishi tamati vya {zi} na {ifu}.
{m}                 + {mzizi-T} + {zi}
{wa}                                                   {ifu}
Kwa mfano
Simamia {m}+{simami}+{zi} > msimamizi
Kimbia{m}+{kimbi}+{zi} > mkimbizi
Kagua {m}+{kagu}+{zi} > mkaguzi
Lea {m}+{le}+{zi} > mlezi
Danganya {m}+{dangany}+{i}+{fu} > mdanganyifu
Komboa {m}+{kombo}+{zi} > mkombozi
Kutumia kiambishi awali cha unominishaji {m} au {ki} pamoja na mzizi wa
{m}
{ki}                 + {mzizi-T} + {O}
{wa}
{vi}
Kwa mfano
Cheza {m}+{chez}+{o} > Mchezo
Kopa {m}+{kop}+{o} > Mkopo
Chora {m}+{chor}+{o} > Mchoro
Lia {m}+{li}+{o} > Mlio
Panga {m}+{pang}+{o} > Mpango
Koma {ki}+{kom}+{o} > Kikomo
Kwaza {ki}+{kwaz}+{o} > Kikwazo
Lima {ki}+{lim}+{o} > Kilimo
Vuka {ki}+{vuk}+{o} > Kivuko
Lia {ki}+{li}+{o} > Kilio
Kutumia kiambishi awali cha unominishaji {mu} au {mi} pamoja na mzizi wa kitenzi na kiambishi tamati {o} cha unominishaji
{mu}               + {mzizi-T} + {O}
{mi}
Kwa mfano
Enda {mu}+{end}+{o} > mwendo
Alika {mu}+{alik}+{o} > mwaliko
Ita {mu}+{it}+{o} > mwito
Isha {mu}+{ish}+{o} > mwisho
Unda {mu}+{und}+{o} > muundo
Ungana {mu}+{ungan}+{o} > muungano
Kutumia kiambishi awali cha unominishaji {Ø} pamoja na mzizi wa kitenzi na
kiambishi tamati {o} cha unominishaji
{Ø}                 + {mzizi-T} + {O}
{ma}
Kwa mfano
Pamba {Ø}+{pamb}+{o} > Pambo
Pinda {Ø}+{pind}+{o} > Pindo
Soma {Ø+{som}+{o} > Soma
Tenda {Ø}+{tend}+{o} > tendo
Tatiza {Ø}+{tatiz}+{o} > tatizo
Tangaza {Ø}+{tangaz}+{o} > tangazo
Umba {Ø}+{umb}+{o} > umbo
Tamka {Ø}+{tamk}+{o} > tamko
Pambana {Ø}+{pamban}+{o} > pambano
Kutumia kiambishi awali {Ø} katika umoja pamoja na mzizi wa kitenzi na kiambishi tamati cha unominishaji {a}
{Ø}                 + {mzizi-T} + {a}
{ma}
Kwa mfano
Shitaki {Ø}+{shitak}+{a} > shitaka
Sifu {Ø}+{sif}+{a} > sifa
Subiri {Ø}+{subir}+{a} > subira
Kutumia kiambishi awali {u} cha unominishaji pamoja na mzizi wa kitenzi na kiambishi tamati cha unominishaji {zi}
{U}   + {mzizi-T} + {zi}
Kwa mfano
Bagua {u}+{bagu}+{zi} > ubaguzi
Chagua {u}+{chagu}+{zi} > uchaguzi
Chochea {u}+{choche}+{zi} > uchochezi
Chukua {u}+{chuku}+{zi} > uchuku
Fafanua {u}+{fafanu}+{zi}
Komboa {u}+{kombo}+{zi}
Fumbua {u}+{fumbu}+{zi}
Pekua {u}+{peku}+{zi}
Kutumia kiambishi awali {u} cha unominishaji pamoja na mzizi wa kitenzi na viambishi tamati vya unominishaji {o} na {i}
{u}/ {m}         + {mzizi-T} + {i} {O}
{wa}
Kwa mfano
Bisha {u}+{bish}+{i} > ubishi
Shinda {u}+{shind}+{i} > ushindi
Penda {u}+{pend}+{o} > upendo
Batiza {u}+{batiz}+{o} > ubatizo
Ita {u}+{it}+{o} > wito
Imba {u}+{imb}+{o} > wimbo
Nomino Kutoka kwa Vivumishi
Tunaweza kuunda nomino kutoka kwa vivumishi kwa kutumia kiambishi awali {u} cha unominishaji pamoja na shina la kivumishi.
{u} + {shina-V}
Kwa mfano
{baya} {u}+{baya} > ubaya
{bovu} {u}+{bovu} > ubovu
{fupi} {u}+{fupi} > ufupi
{kubwa} {u}+{kubwa} > ukubwa
{dhaifu} {u}+{dhaifu} > udhaifu
{katili} {u}+{katili} > ukatili
{bora} {u}+{bora} > ubora
Nomino kutoka kwa Nomino Zingine
Tunaweza kuunda nomino kutoka kwa nomino zingine kwa kutumia kiambishi awali {u} cha unominishaji pamoja na mzizi wa nomino.
{u} + {mzizi-N}
Kwa mfano
Rafiki {u}+{rafiki} > urafiki
Balozi {u}+{balozi} > ubalozi
Bingwa {u}+{bingwa} > ubingwa
Chachu {u}+{chachu} > uchachu
Bepari {u}+{bepari} > ubepari
Fundi {u}+{fundi} > ufundi
Seremala {u}+{seremala}
HITIMISHO
Kwa ujumla michakato ya unomiishaji ya mnyumbuliko geuzi ya kategoria ya lugha ya Kiswahili inatusaidia katika kunadili kategoria mbalimbali za maneno na kuwa nomino. Hivyo maneno mbalimbali ya lugha ya Kiswahili kama vile vitenzi vivumishi na nomino yenyewe tunaweza kubadili kategoria hizo na kuwa nomino.


MAREJELEO
Habwe na Karanja ( 2004). Misingi ya Sarufi ya Kiswahili; Nairobi Kenya: Phoenix Publishers.
Massebo, J.A (2012). Nadharia ya Lugha Kiswahili. Dar es Salaam.Nyambari Nyangwine                                     Publishers.
Mgullu, R.S (2012). Mtaala wa Isimu: Fonetiki, Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili; Longman                            publishers.
Matinde, S (   2012). Dafina ya Lugha, Isimu na Nadharia kwa Shule za Sekondari, Vyuo vya                              kati na Vyuo Vikuu.


Comments

Popular posts from this blog

Historical Background Of Tanzania Revenue Authority (TRA)

It's true that agriculture is a change agent in Tanzania development due to the following reasons;