Unominishaji,
Unominishaji, habwe na kavanja [2007] ni
hali ya kuunda nomino kutoka katika kategolia nyingine ya neno. Kategolia hizi
zinaaweza kuwa kitenzi, kivumishi, au nomino yenyewe. Hali hii ya uniminiashaji
husababisha kuwepo kwa mofimu changamano zenye mofimu nying ndani yake.
Tuki
{1981} ni kutoa neno katika kategolia moja na kuliingiza katika kategolia ya
nomino.
Kwa
ujumla unominishaji ni kitendo cha
kubadili neno kutoka kwenye kategolia nyingine ya neno na kupeleka katika nomino.kwa hiyo mchakato
huu hufanywa ili kupata nomino za lugha ya Kiswahili ,unominishaji pia husaidia
sana katika kuongeza misamiati katika lugha ya Kiswahili hivyo basi tuangalie
mchakato wa unominishaji kutokana na kategolia mbalimbali za lugha ya Kiswahili
isipokua kategoria ya kitenzi ,na nomino yenyewe michakato hio ipo kama
ifuatavyo hapo chini;
v Unominishaji katika vivumishi
Kivumishi
– nomino
Unominisaji
huu wa kivumishi hubadilika na kuwaa nomino
Tunaunda nomino kutokana na vuvumush kwa kutumia
viambisha awali cha unominishaji[U} pamoja na Mzizi wa nomino
Mfano
kanuni
(unominishaji
Kivumishi = {u}
{shina}-
nomino
Baya = {u} + {baya} = ubaya
Zuri = {u} + {zuri} = uzuri
Kubwa = {u} + {kubwa} = ukubwa
Bora = {u} + {bora} = ubora
Katili = {u} + {katili} = ukatili
Chafu
= {u} + [chafu} = uchafu
Vivu = {u} + {vivu} = uvivu
v Unominishaji katika vielezi
Kuna
baadhi ya vielezi hubadilika,kutokana na
kufanyiwa unominishaji unominishaji wa vielezi hutokea katika aina
mbili yaani katika vielezi vya mahali na
vielezi vya namna hii huweza kuwa kama
ifuatayo;
Ø Vielezi
vya mahali huweza kubadilika na kuwa
nomino hiyo kutokana na kuondosha kiambishi “ni” mwizhoni mwa kielezi hicho
hivyo tunapata nomino.
Mfano
Kielezi Nomino
Jikoni jiko-“ni”
Hapa
tumeona silabi “ni” imeondolewa tumepata
nomino jiko
Kielezi nomino
Shambani shamba-“ni”
Hapa
katika kielezi shambani tukiondoa silabi
“ni” tunapata nomino shamba hilo
limetokana baada ya kuondoa silabi “ni”
Mifano
mingine ni kama vile shuleni –tukiondoa nitunapata shule
Kanisani
tunapata kanisa
Kabulini
tunapata kabuli
Kabatini
tunapata kabati
Ø vielezi
vya namna hivyo hupelekea mchakato wa unominishaji na kielezi hicho hubadilikana kuwa nomino kwa
mfano
Mary
anaimba vizuri
Vizuri
{kielezi}-nomino-uzuri
Vibaya{kielezi}-nomino
–ubaya
Hitimisho
Kwa
hiyo mchakato wa unominishaji hauwezi kutokea katika kategoriaya neno mchakato
huu hufanyika kwenye kategoria chachetu za maneno madhara ni katika vivumishi,vitenzi,nomino
yenyewe na vielezi hiyo mchakato wa
unomishaji hubagua baadhi ya kategoria kwa mfano
Kiunganishi
hakiwezi kupokea unominishaji ,kihusishi.na kihisishi.
Tuki{1981}kamusi
ya Kiswahili sanifu
Hambwe
na Kavanje{2007}
Comments
Post a Comment