UTANGULIZI Tamthiliya ya Mashetani ni tamthiliya ambayo ilitungwa na msanii Ebrahim N.Hussein na kuchapishwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka (1971). Tamthiliya hii ni tamthiliya ya kimajaribio inayosawiri mazingira ya kikoloni kwa mchezo kati ya Juma na Kitaru ambapo kati yao Kitaru ni binadamu na Juma ni shetani. Hii ni tamthiliya inayoakisi ukoloni mkongwe katika nchi za dunia ya tatu. Tamthiliya hii ilimtumia muhusika shetani kama jazanda ya ukoloni na binadamu kama raia wa nchi za ulimwengu wa tatu na jinsi raia hao walivyoathiriwa na ukoloni. Ukoloni mamboleo, ni suala la nchi chache zenye nguvu zaidi za kiuchumi na kisiasa kuzitawala nchi zisizo na nguvu. Padley (2006). Zifuatazo ni athari hasi za ukoloni mamboleo katika tamthiliya ya Mashetani; Kuwepo kwa matabaka kutokana na elimu ya kikoloni, mwandishi ameonesha kuwa elimu ya kikoloni imeleta mkanganyiko katika fikra za wananchi na kupelekea matabaka yanayohasimiana katika jamii. Kundi lililobahatika kupata elimu ya kimagharibi linaitumia elimu hii kama ni nyenzo ya kupata madaraka, nafasi za uongozi na kutwalia mali za umma. Fursa hizi zinatumiwa vibaya na vibaraka wa ukoloni mamboleo ili kuwanyanyasa na kuwakandamiza waliokosa elimu hio. Msanii anasema; “Juma: Wewe unaishi leo. Mimi ninaishi jana. Tutakuwaje marafiki? Na kila leo yako ni kidato cha kesho yako. Mimi, kila leo yangu ni kidato cha jana zangu. Na kila nikienda huko, nikirudi narudi na hadithi ….hadithi za mashetani”. Pia, kimsingi elimu ya kikoloni inaonekana kutowasaidia wananchi kwani haiendani na mazingira na mahitajio yao. Msanii anawatumia Juma na Kitaru, vijana waliobahatika kupata elimu ya Kimagharibi katika ngazi ya Chuo Kikuu hata hivyo hawawezi kujikomboa. Msanii anasema: “Juma: Sasa unaniambia nini. Hujaniambia kitu. Kweli inauma bwana. Ukweli…acha yote hayo. Ukweli bwana, digirii iankupa tonge ya wali na mchuzi, tena mchuzi wa kuku, badala ya ugali na maharage” (uk.17). Kuanzishwa kwa sera ya utandawazi na ubinafsishaji, ambazo zimekuwa zikisimamiwa na vibaraka wa kikoloni ili kundeleza unyonyaji. Wanapokea sera na mikataba kikasuku bila ya kuhakiki faida na hasara zake. Shetani anasema: Shetani: Unanijua mimi nani? Mimi Shetani. Sio Jini wa Kuhani Mimi Shetani Uwezo wangu hauhifadhiki Wema wangu hauhesabiki Ubaya wangu hausemeki Ninajenga Ninabomoa Ninatukuza Ninadhalilisha nitakavyo Mimi ni nguvu na nguvu ni mimi, Mimi ni uwezo na uwezo ni mimi. (uk. 1-2) Ukoloni mamboleo umepelekea kuwepo kwa ukiukwaji wa demokrasia katika jamii za Afrika baada ya kupata uhuru wa bendera. Mara tu baada ya Wafrika kushika hatamu za uongozi, tabaka lililokuwa katika hatamu za uongozi kabla yao walinyanganywa mali zao, ikiwamo mashamba ya mikarafu na nyumba. Hali hii ilisababisha mifarakano, chuki na uhasama miongoni mwa pande hizo mbili. Msanii anatuonesha namna Kitaru na Juma walivyo na uhasama unaotokana na msingi huu wa ukiukwaji wa demokrasia. Msanii analidhihirisha kwa kumtumia baba Kitaru ambapo ana tueleza kuwa familia ya Juma inatokea Unguja na familia ya Kitaru inatokea Tanganyika. Wazazi wa Juma walikuwa na mashamba ya mikarafuu lakini baada ya mapinduzi ya Zanzibar serikali iliyachukuwa. Mwandishi anadhihirisha hili kwa kusema: Baba: (Anajaribu kubadilisha mazungumzo) Rafiki yako Juma anatoka wapi? Ninafahamu anatoka Unguja. Lakini wapi? sehemu gani? Wazee wake walikuwa Wanafanya nini huko? Kitaru :Wazee wake walikuwa na mashamba ya karafuu lakini baada ya mapinduzi serikali iliyachukuwa” (uk26). Mwandishi ametuonesha tukio la utaifishaji wa huko Zanzibar lilivyoingiza migogoro kati ya Juma na Kitaru. Kitendo hiki tunakiita kwamba ni ukiukwaji wa demokrasi kwani kilifanyika bila ya kuzingatia misingi ya haki na sheria. Tukio hili limeacha huzuni za kihistoria miongoni mwa wale walioathirika. Msanii anasema: “…Ulikuwa na mangapi, licha ya mabenzi. Ulikuwa na mashamba madallbasari. Ulikuwa na watu chini yako. Haya yaliopita si basi tu, mwenyewe Mungu ndivyo alivyopenda-mali yetu kuchukuliwa na kugaiwa watu. Watu tu hivi hivi, watu wasiojua hata maana ya milki ni nini” (uk. 38). Katika maelezo ya hapo juu mwandishi anaonesha masikitiko waliyonayo wale walionyanganywa mali zao kama vile bibi yake Juma baada ya mapinduzi ya Zanzibar ambapo serikali ilichukuwa mashamba yao na kupewa watu wengine. Jambo hili linaonekana kuzua chuki na mfarakano miongoni mwa marafiki hawa. Familia ya Juma ilibidi ihamie Dar es Salam na kuanza maisha upya kwa kuanzisha biashara ya kidua. Ukoloni mamboleo umepelekea kuwepo kwa uongozi mbaya, kwa mfano katika tamthiliya ya Mashetani mwandishi anaonesha namna utawala mbaya unavyotumia nafasi waliyonayo katika kuhujumu na kufanya ubadhirifu wa mali za uma. Msanii anamtumia mhusika Baba Kitaru ambaye anatumia pesa za kampuni kwa manufaa yake binafsi. Baba Kitaru ananunua gari la kifahari kwa fedha za ubadhirifu. Msanii analieleza hili kwa kusema: MTU 1: Aaah, acha bwana we. Sasa unataka kuniambia nini? (Mlio wa gari inapita). Doo doo! Salale! Umeuona mdudu ule? MTU 2: Nini? Ile gari? Nimeiona. Aah, ataiuza kesho ile. We ngoja tu. MTU 1: Kwani we unamjua yule? MTU 2: Kwani we humjui? MTU 1: Hata. MTU 2: Jana hatukuwa wote pamoja, alipo akitusimulia Bwana Methew juu ya kufungwa kwa ile kampuni. MTU 1: Aah, aah! Ndiyo, ndiyo, ndiyo. Aha! Kwani huyu ndiye bwana mwenyewe? MTU 2: Pesa chungu nzima bwana zimepotea. Lakini ndiyo haijulikani kuwa zimeibiwa au zimepote katika mahisabu. MTU 1: Alaa. Kumbe ndiye huyu? Shetani kweli kweli. (uk.42-43). Hivyo, wakoloni wanaonekana ni viongozi wabaya wanaotumia mbinu mbali mbali ili kukandamiza nchi maskini. Matokeo ya uongozi mbaya wa kikoloni ni kukithiri kwa ukandamizaji na unyonyaji katika jamii. Kutokana na uongozi mbaya wa kikoloni nchi nyingi leo hii zimeingia katika machafuko na vita na hivyo kuchafuliwa kabisa. Msanii anasema: “SHETANI: unanijua mimi nani? Mimi shetani. Sio jini wala kuhani. Mimi shetani. Uwezo wangu hauhifadhiki. Wema wangu hauhesabiki. Ubaya wangu hausemeki. Ninajenga. Ninabomboa. Ninadhalilisha nitakavyo” (uk. 1). Ukoloni mamboleo unarudisha nyuma ujenzi wa jamii mpya, katika tamthiliya ya Mashetani mwandishi anaonesha jinsi anavyomtumia Shetani kuashiria ukoloni mamboleo ambapo anaonesha umekuja kwa sura mpya tofauti na ulivyokuwa mwanzo. Hivyo, jamii za Kiafrika hazina budi kupambana na ukoloni mamboleo ili kujenga ukombozi wa kweli katika kuijenga jamii mpya. Pia, jamii hii inaonekana ikikumbwa na tatizo la wazawa kujilimbikizia mali kwa maslahi yao binafsi hii inatokana na kuwepo kwa tabia za kikoloni katika jamii. Msanii anaitumia familia ya Kitaru ambayo ilikuwa imejilimbikizia mali. Msanii anaakisi hali hiyo kwa kusema: MTU 1: Aaah, acha bwana we. Sasa unataka kuniambia nini? (Mlio wa gari inapita). Doo doo! Salale! Umeuona mdudu ule? MTU 2: Nini? Ile gari? Nimeiona. Aah, ataiuza kesho ile. We ngoja tu. MTU 1: Kwani we unamjua yule? MTU 2: Kwani we humjui? MTU 1: Hata. MTU 2: Jana hatukuwa wote pamoja, alipo akitusimulia Bwana Methew juu ya kufungwa kwa ile kampuni. MTU 1: Aah, aah! Ndiyo, ndiyo, ndiyo. Aha! Kwani huyu ndiye bwana mwenyewe? MTU 2: Pesa chungu nzima bwana zimepotea. Lakini ndiyo haijulikani kuwa zimeibiwa au zimepote katika mahisabu. MTU 1: Alaa. Kumbe ndiye huyu? Shetani kweli kweli. (uk.42-43).
UTANGULIZI
Tamthiliya ya Mashetani
ni tamthiliya ambayo ilitungwa na msanii Ebrahim N.Hussein na kuchapishwa
kwa mara ya kwanza mnamo mwaka (1971). Tamthiliya hii ni tamthiliya ya
kimajaribio inayosawiri mazingira ya kikoloni kwa mchezo kati ya Juma na Kitaru
ambapo kati yao Kitaru ni binadamu na Juma ni shetani. Hii ni tamthiliya
inayoakisi ukoloni mkongwe katika nchi za dunia ya tatu. Tamthiliya hii
ilimtumia muhusika shetani kama jazanda ya ukoloni na binadamu kama raia wa nchi
za ulimwengu wa tatu na jinsi raia hao walivyoathiriwa na ukoloni.
Ukoloni mamboleo, ni
suala la nchi chache zenye nguvu zaidi za kiuchumi na kisiasa kuzitawala nchi
zisizo na nguvu. Padley (2006).
Zifuatazo ni athari hasi
za ukoloni mamboleo katika tamthiliya ya Mashetani;
Kuwepo
kwa matabaka kutokana na elimu ya kikoloni, mwandishi
ameonesha kuwa elimu ya kikoloni imeleta mkanganyiko katika fikra za
wananchi na kupelekea matabaka yanayohasimiana katika jamii. Kundi
lililobahatika kupata elimu ya kimagharibi linaitumia elimu hii kama ni nyenzo
ya kupata madaraka, nafasi za uongozi na kutwalia mali za umma. Fursa hizi
zinatumiwa vibaya na vibaraka wa ukoloni mamboleo ili kuwanyanyasa na
kuwakandamiza waliokosa elimu hio. Msanii anasema;
“Juma:
Wewe unaishi leo. Mimi ninaishi jana.
Tutakuwaje
marafiki? Na kila leo yako ni kidato
cha kesho yako.
Mimi, kila leo yangu ni kidato cha jana zangu.
Na kila
nikienda huko, nikirudi narudi na hadithi
….hadithi
za mashetani”.
Pia, kimsingi elimu ya kikoloni inaonekana
kutowasaidia wananchi kwani haiendani na mazingira na mahitajio yao. Msanii
anawatumia Juma na Kitaru, vijana waliobahatika kupata elimu ya Kimagharibi katika
ngazi ya Chuo Kikuu hata hivyo hawawezi kujikomboa. Msanii anasema:
“Juma: Sasa unaniambia nini. Hujaniambia
kitu. Kweli inauma bwana.
Ukweli…acha
yote hayo. Ukweli bwana, digirii iankupa tonge ya wali na mchuzi, tena
mchuzi wa kuku, badala ya ugali na maharage”
(uk.17).
Kuanzishwa
kwa sera ya utandawazi na ubinafsishaji, ambazo zimekuwa zikisimamiwa na vibaraka wa kikoloni ili kundeleza unyonyaji. Wanapokea
sera na mikataba kikasuku bila ya kuhakiki faida na hasara zake. Shetani
anasema:
Shetani: Unanijua mimi nani?
Mimi Shetani.
Sio Jini wa Kuhani
Mimi Shetani
Uwezo wangu hauhifadhiki
Wema wangu hauhesabiki
Ubaya wangu hausemeki
Ninajenga
Ninabomoa
Ninatukuza
Ninadhalilisha nitakavyo
Mimi ni nguvu na nguvu ni mimi,
Mimi ni uwezo na uwezo ni mimi. (uk. 1-2)
Ukoloni
mamboleo umepelekea kuwepo kwa ukiukwaji wa demokrasia katika
jamii za Afrika baada ya kupata uhuru wa bendera. Mara tu baada ya Wafrika
kushika hatamu za uongozi, tabaka lililokuwa katika hatamu za uongozi kabla yao
walinyanganywa mali zao, ikiwamo mashamba ya mikarafu na nyumba. Hali hii ilisababisha
mifarakano, chuki na uhasama miongoni mwa pande hizo mbili. Msanii anatuonesha
namna Kitaru na Juma walivyo na uhasama unaotokana na msingi huu wa ukiukwaji
wa demokrasia. Msanii analidhihirisha kwa kumtumia baba Kitaru ambapo ana
tueleza kuwa familia ya Juma inatokea Unguja na familia ya Kitaru inatokea
Tanganyika. Wazazi wa Juma walikuwa na mashamba ya mikarafuu lakini baada ya
mapinduzi ya Zanzibar serikali iliyachukuwa. Mwandishi anadhihirisha hili kwa
kusema:
Baba: (Anajaribu kubadilisha
mazungumzo) Rafiki yako Juma anatoka wapi?
Ninafahamu anatoka
Unguja. Lakini wapi? sehemu gani? Wazee wake
walikuwa Wanafanya nini
huko?
Kitaru :Wazee wake walikuwa na
mashamba ya karafuu lakini baada ya
mapinduzi serikali
iliyachukuwa” (uk26).
Mwandishi ametuonesha
tukio la utaifishaji wa huko Zanzibar lilivyoingiza migogoro kati ya Juma na
Kitaru. Kitendo hiki tunakiita kwamba ni ukiukwaji wa demokrasi kwani
kilifanyika bila ya kuzingatia misingi ya haki na sheria. Tukio hili limeacha
huzuni za kihistoria miongoni mwa wale walioathirika. Msanii anasema:
“…Ulikuwa na mangapi,
licha ya mabenzi. Ulikuwa na mashamba
madallbasari. Ulikuwa na
watu chini yako. Haya yaliopita si basi tu,
mwenyewe Mungu ndivyo
alivyopenda-mali yetu kuchukuliwa na kugaiwa
watu. Watu tu hivi hivi,
watu wasiojua hata maana ya milki ni nini” (uk. 38).
Katika maelezo ya hapo
juu mwandishi anaonesha masikitiko waliyonayo wale walionyanganywa mali zao
kama vile bibi yake Juma baada ya mapinduzi ya Zanzibar ambapo serikali ilichukuwa
mashamba yao na kupewa watu wengine. Jambo hili linaonekana kuzua chuki na
mfarakano miongoni mwa marafiki hawa. Familia ya Juma ilibidi ihamie Dar es
Salam na kuanza maisha upya kwa kuanzisha biashara ya kidua.
Ukoloni
mamboleo umepelekea kuwepo kwa uongozi mbaya, kwa mfano katika tamthiliya ya
Mashetani
mwandishi anaonesha namna
utawala mbaya unavyotumia nafasi waliyonayo katika kuhujumu na kufanya
ubadhirifu wa mali za uma. Msanii anamtumia mhusika Baba Kitaru ambaye anatumia
pesa za kampuni kwa manufaa yake binafsi. Baba Kitaru ananunua gari la kifahari
kwa fedha za ubadhirifu. Msanii analieleza hili kwa kusema:
MTU
1: Aaah, acha bwana we. Sasa unataka kuniambia nini?
(Mlio wa gari inapita). Doo doo! Salale!
Umeuona mdudu ule?
MTU
2: Nini? Ile gari? Nimeiona. Aah, ataiuza kesho ile. We ngoja tu.
MTU
1: Kwani we unamjua yule?
MTU
2: Kwani we humjui?
MTU
1: Hata.
MTU
2: Jana hatukuwa wote pamoja, alipo akitusimulia Bwana Methew juu ya
kufungwa
kwa ile kampuni.
MTU
1: Aah, aah! Ndiyo, ndiyo, ndiyo. Aha! Kwani huyu ndiye bwana
mwenyewe?
MTU
2: Pesa chungu nzima bwana zimepotea. Lakini ndiyo
haijulikani
kuwa
zimeibiwa au zimepote katika mahisabu.
MTU
1: Alaa. Kumbe ndiye huyu? Shetani kweli kweli. (uk.42-43).
Hivyo, wakoloni
wanaonekana ni viongozi wabaya wanaotumia mbinu mbali mbali ili kukandamiza
nchi maskini. Matokeo ya uongozi mbaya wa kikoloni ni kukithiri kwa ukandamizaji
na unyonyaji katika jamii. Kutokana na uongozi mbaya wa kikoloni nchi nyingi
leo hii zimeingia katika machafuko na vita na hivyo kuchafuliwa kabisa. Msanii
anasema:
“SHETANI: unanijua
mimi nani?
Mimi
shetani.
Sio
jini wala kuhani.
Mimi
shetani.
Uwezo
wangu hauhifadhiki.
Wema
wangu hauhesabiki.
Ubaya
wangu hausemeki.
Ninajenga.
Ninabomboa.
Ninadhalilisha
nitakavyo” (uk. 1).
Ukoloni
mamboleo unarudisha nyuma ujenzi wa jamii mpya, katika tamthiliya ya Mashetani mwandishi
anaonesha jinsi anavyomtumia Shetani
kuashiria ukoloni mamboleo ambapo anaonesha umekuja kwa sura mpya tofauti na
ulivyokuwa mwanzo. Hivyo, jamii za Kiafrika hazina budi kupambana na ukoloni
mamboleo ili kujenga ukombozi wa kweli katika kuijenga jamii mpya. Pia, jamii
hii inaonekana ikikumbwa na tatizo la wazawa kujilimbikizia mali kwa maslahi
yao binafsi hii inatokana na kuwepo kwa tabia za kikoloni katika jamii. Msanii
anaitumia familia ya Kitaru ambayo ilikuwa imejilimbikizia mali. Msanii
anaakisi hali hiyo kwa kusema:
MTU 1: Aaah, acha bwana
we. Sasa unataka kuniambia nini? (Mlio wa gari inapita). Doo doo! Salale!
Umeuona mdudu ule?
MTU 2: Nini? Ile gari?
Nimeiona. Aah, ataiuza kesho ile. We ngoja tu.
MTU 1: Kwani we unamjua
yule?
MTU 2: Kwani we humjui?
MTU 1: Hata.
MTU 2: Jana hatukuwa wote
pamoja, alipo akitusimulia Bwana Methew juu ya kufungwa kwa ile kampuni.
MTU 1: Aah, aah! Ndiyo,
ndiyo, ndiyo. Aha! Kwani huyu ndiye bwana mwenyewe?
MTU 2: Pesa chungu nzima
bwana zimepotea. Lakini ndiyo haijulikani kuwa zimeibiwa au zimepote katika
mahisabu.
MTU 1: Alaa. Kumbe ndiye
huyu? Shetani kweli kweli. (uk.42-43).
Comments
Post a Comment