Dhana ya kategoria ya kileksika
Dhana ya kategoria ya kileksika; imejadiliwa kwa namna
tofauti tofauti:-
Khamisi na Kiongo
(2002); wamegawa kategoria katika mitazamo miwili ambayo ni:- mtazamo wanamapokeo na wanausasa, ambapo
wanamapokeo walitumia dhana ya kategoria ya kileksika kumaanisha sifa bainifu
ya vitu na wanausasa wanaona kategoria kuwa ni zile aina za maneno kama vile
nomino, kivumishi, vielezi, viunganishi, vihusishi na vitenzi.
Massamba (2009),
anatoa maana ya kategoria ya kilekisika kwa kusema kuwa ni jumla ya maumbo,
faridi au vipashio vingine ambavyo huchangia sifa fulani au ambavyo viko katika
kiwango kimoja. Maana hii ni ya jumla kwani imeeleza dhana ya kategoria ya
kileksika kwa ujumla bila kujikita katika kategoria za miundo ambayo ndiyo
sintaksia.
Kategoria za
kileksika katka lugha ya kiswahili zipo kategoria nane za kileksika ambazo ni
nomino, vitenzi, viwakilishi, vielezi, viunganishi, vivumishi, vihusishi na
vihisishi.
Kwamjibu wa Massamba,
Kihole, Hokororo (2012 uk.67), wanasema tungo ni nomino ambayo imetokana na
kitenzi tunga ambacho kinamaana kushikanisha vitu kwa pamoja kwa kutumia kitu
Kama uzi, ungwe ndani yake. Hivyo katika taaluma ya sarufi neno tungo lina
maana ya kuweka au kupanga vipashio sahihi ili kujenga vipashio vikubwa katika
tungo. Katika lugha ya kiswahili Kuna aina nne za tungo ambazo ni tungo neno,
tungo kirai, tungo kishazi na tungo sentensi ambapo tungo hizo huundwa na aina
mbalimbali za maneno Kama nomino, kiwakilishi, vivumishi,
viunganishi,vitenzi,vielezi,vihisishi na vihusishi. Kamusi
teule ya kiswahili (2001); tungo ni kifungu cha maneno kinachoongozwa na kanuni
kisarufi, vipashio vinavyo ungana huunda vipashio vikubwa zaidi.
Kamusi ya kiswahili
(2014), tungo ni kipashio cha kimuundo kipatikanacho kwa kuunganisha vipashio
sahihi kuweza kupata kipashio kikubwa zaidi, kwa ujumla tungo ni kipashio cha
kimuundo ambacho huwekwa pamoja ili kujenga vipashio vikubwa zaidi katika
sarufi.
Kategoria za
kileksika na kategoria za tungo ni kweli zinamipaka inayo pitika kwa sababu
tungo hujidhihilisha katika miundo minne ambayo ni tungo neno, tungo kirai,
tungo sentensi na tungo kishazi. Viwango hivi ndivyo vinavyodhibitisha kupitika
kwa kategoria za kilekisika na kategoria za tungo katika lugha.
Kwa kuanza na muundo
wa tungo neno, ni tungo ambayo ina muundo wa vipashio zaidi ya neno ambayo ni
mofimu au fonimu, mfano anacheza, kakimbia. Kategoria ya tungo neno inahusisha
aina kuu za maneno yanapo undwa, kinacho zingatiwa katika uainishaji wa tungo
neno ni aina za maneno ambayo kwa mantiki hiyo huonedha kupitika huko kwa
kategoria za kileksika na kategoria za tungo kwa kutumia aina za maneno ambayo
pia hupatikana katika kategoria za kilekisika mfano wa kategoria mojawapo ni
nomino, kitenzi, kiunganishi, kihisishi, vihusishi, kiwakilishi, na kivumishi.
Mfano; - Mama
anapika
- Mjomba
anapenda kuimba mziki wa kizazi kipya.
- Mama
anapenda kufanya kazi zake vizuri.
Hivyo aina hizi za maneno ambazo zimetumika katka kuunda sentensi
hizo pia zinapatikana katika tungo mfano tungo neno, tungo neno kuna nomino
ndaniyake hivyo tunasema inapitika katika kategoria za kileksika na kategoria
za tungo.
Miundo ya tungo
kirai, kirai ni neno au fungu la maneno ambalo kwapamoja hutoa taarifa fulani.
Kirai sikuzote hakitoi taarifa fulani isiyo kamili ukiachilia mbali vitenzi vya
lugha za kibantu. Kategoria ya kirai huundwa kwa aina kuu za maneno, virai hivi
huwa na neno kuu na ndilo linalo dhibitisha kirai kipewe jina lipi. Hivyo aina
izo za maneno pia ndizo hupatikana katika kategoria za kilekisika. Kwamfano wa
tungo kirai Kuna kirai nomino mfano, Rahma mrembo, kirai kitenzi kitenzi mfano
anapika vibaya, kirai kivumishi mfano kizuri sana, kirai kielezi mfano kizuri
sana, kirai kiunganishi mfano kule,walakini, kihusishi mfano kwa gari na wa
baba hivyo kupitia aina hizi za virai pia tunaziona kwenye aina za maneno
ambayo ndio ni kategoria za kilekisika kwa sababu hihi inaonesha mipaka inayo
pitika.
Miundo ya kishazi, ni
fungu la maneno lenye kiima na kiarifu. Matinde (20012), hata hivyo anadai kuwa
kishazi lazima kiwe na kitenzi ndaniyake. Kitenzi kinacho kuwepo katika muundo
wa kishazi ndicho kinacho amua kishazi kiitwe kishazi huru au kishazi tegemezi
na kukifanya kishazi kitoe taarifa kamili au taarifa isiyo kamili. Mfano
kishazi kimegawanyika katika Aina mbili, kishazi huru na kishazi tegemezi hivyo
kupitia aina za vishazi vinatumia aina za maneno Kama nomino, vitenzi, vielezi,
viwakilishi, vihisishi na vihusishi hivyo sababu hii inadhihilisha kupitika kwa
kategoria za kileksika na kategoria za tungo kwa mfano:-
- Mtoto amekuja
N T
- Mtoto analima
N T
- Mtoto aliekuja
jana
N BV
E
Miundo ya sentensi,
kategoria ya sentensi inahusu kipashio kikubwa kabisa katika taaluma ya sarufi.
Sentensi ni tungo inayo toa taarifa iliyo kamili yenye kiima na kiarifu. Kuna
aina kuu tatu za sentensi kimuundo ambazo ni:-
(i). Sentensi sahili,
ni Sentensi inayoundwa na kishazi huru kimoja ambacho hutoa taarifa kamili. Kwamfano;
-Mtoto mkorofi
sana.
(ii).Sentensi
changamano,ni Sentensi inayoundwa na kishazi tegemezi kimoja au zaidi na
kishazi huru kimoja. kwamfano:-
- Mtoto
aliyekufa Jana.
(iii).Sentensi
ambatano ni aina ya sentensi ambayo huundwa na sentensi mbili kwa kuunganishwa
na lakini, na pia alama za uandishi Kama vile nukta, mkato .nk. kwamfano:-
- Mama anapika
na Baba analima
Aina hizi tatu za sentensi muundo wake huundwa na aina za
maneno ambayo hupatikana katita kategoria za kileksika hivyo huonesha mipaka
inavyo pitika Kati ya kategoria za kileksika na kategoria za tungo kwa mfano wa
sentensi ambazo zimetumia aina za maneno ni;
- Magambo
anakuja leo asubuhi.
N T
E
- Tiffa
analima.
N T
- Mama na baba
wanalima na kaka na mimi tunacheza mpira kiwanjani.
N U
N T U
N U N
T N E
Kwakuhitimisha
kategoria za tungo na kategoria za kileksika zote zinategemeana bila tungo
hapawezi kuwa na maneno na bila maneno hatuwezi kuunda tungo hivyo kategoria za
kileksika na kategoria za tungo zote zina saidia kuonesha uchunguzi sahihi wa
maneno na uteuzi wa tungo sahihi katika lugha yoyote ulimwenguni iwe kiswahili,
kireno n.k, aina za maneno ndizo zinaamua tungo ipewe jina gani inaweza ikawa
sentensi, kirai, kishazi, na neno hivyo kupitia kanuni mbalimbali za kisarufi
ndipo tunapata kupitika huko Kati ya kategoria za kileksika na kategoria za
tungo Kama tungo neno, kirai, kishazi na sentensi.
MAREJEO.
TUKI, (2004), Kamusi ya Kiswahili Sanifu Chuo Kikuu cha Dar
es salaam.
Massamba na Wenzake (20012), Sarufi ya kiswahili sanifu
(samakisa) Sekondari na Vyuo Dar es
salaam.
Ndugu, A E, bubwa, H,N, mirkau, S.A, (2014), Kamusi teule ya
kiswahili, Nairobi, Kampala, Dar es salaam,Kingali.
Kiwere A.D, (2007) Ukuaji wa Kiswahili na ustawi was Jamii
ya wazungumzaji wake Dar es salaam.
Sijapata kuelewa zipi ndizo kategoria za kileksia?..
ReplyDelete