Sanaa
Sanaa
ni ufundi anaotumia mwanadamu ili
kufikisha fikra au mawazo yaliyo ndani
ya akAAili yake vilivile sanaa ni uzuri unaojidhihirisha katika umbo
lililosanifiwa, hivyo kazi yoyote ya sanaa inategemea ioneshe ufundi wa hali ya
juu ili iwe na mvuto kwa hadhira yake. Kuna aina nane za sanaa ambazo ni sanaa
za maonesho, sanaa za uchongaji, sanaa za uchoraji, sanaa za ufinyanzi, sanaa za ufumaji, sanaa za ushonaji,sanaa za ususi na sanaa za
utarizi, pia kimsingi fasihi ni aina moja wapo ya kazi ya sanaa ambayo inatumia
lugha.
Ni
kweli kwamba sanaa si halisi zaidi kuliko uhalisia wenyewe na haina ukweli
zaidi kuliko ukweli wenyewe, kwa hoja zifuatazo kama zilivyo ainishwa hapo
chini,
Wahusika,
wahusika ni viumbe vyovyote vinavyotumika katika ya sanaa, msanii huwachora wahusika katika
sura mbalimbali akirejelea tabia ama hulka za watu kutoka katika jamii husika,
mfano katika tamthiliya ya Kilio chetu msanii amemchora Joti kama mhusika
mwenye tabia ya umalaya lakini tabia hii
inapatikana katika jamii zetu, hivyo sanaa si halisi kuliko uhalisia
wenyewe na pia haina ukweli zaidi kuliko
ukweli wenyewe kwa sababu kwa huiga
tabia za watu kutoka katka jamii zetu na kuwachora wahusika katka kazi
yake.
Mandhari,
ni mahali popote ambapo tukio la kifasihi hutendeka , masanii huchora mandhari
mbalimbali kaitka kazi zake akirejelea mandhari halisi katika mazingira halisi yanayo
patikana katika jamii, mfano katika riwaya
Usiku utakapokwisha msanii ametumia mandhari halisi, mandhari hayo
yanapatikana katika jiji la Dar ES Salaam kama eneo linalojulikana kwa jina la
Tandika na Manzese, hivyo sanaa si halisi kuliko uhalisia wenyewe na pia haina
ukweli zaidi kuliko ukweli wenyewe kwa sababu
hutaja maeneo halisi katika kazi zao
Mtindo,
ni upekee wa mwandishi, upekee huo ambao humtofautisha na watunzi wengine,
mtindo hutofautiana kati ya mtunzi mmoja na mtunzi mwingine, msanii huiga
mitindo mbali mbali ambayo inapatikana katika jamii zetu mfano katika
tamthiliya ya orodha msanii ametumia mbinu ya barua, kiuhalisia mbinu hii
hupatikana katika mazingira yetu halisi , hivyo sanaa si halisi kuiliko
uhalisia wenyewew na pia haina ukweli zaidi kuliko ukweli wenyewe kwasababu
mitindo kadhaa ambayo hutumiwa hutoka
katika jamii zetu
Muundo,
ni mpangilio wa kiufundi anaoutumia mtunzi kupangilia kazi yake , kuna aina
tatu za miundo ambazo ni muundo wa moja kwa moja, muundo wa rejea ama kioo,
muundo rukia, kwa mfano katika riwaya ya takadini msanii ametumia muundo wa
moja kwa moja, hivyo sanaa si halisi
kuliko uhalisia wenyewe na pia haina ukweli zaidi kuliko ukweli wenyewe kwa
sababu miundo yote hii inapatikana katika jamii zetu halisi na sanaa uiga tu.
Matumizi ya lugha,
matumizi ya lugha ndio mzizi wa fasihi. Matumizi ya lugha ni ustadi wa kuyaibua
mawazo yaliyomo katika jamii kwa kuisuka na kuifuma lugha kiufundi na kuifanya
ionekane ya kifasihi, matumizi ya lugha hujidhihirisha kwa namna tatu ambazo ni
tamathali za semi, semi na mbinu nyingine za kisanaa, wasanii katika kazi zao
hutumia lugha na lugha hizo hupatikana katika jamii zetu, mfano katika
tamthilya ya kilio chetu msanii ametumia tamathali za semi , hivyo sanaa si
halisi kuliko uhalisia wenyewew na pia haina ukweli zaidi kuliko ukweli wenyewe
kwa sababu tuhumia lugha ambazo msingi wake binadam anaepatikana katika mazingira
halisi.
HITIMISHO
Kwa
ujumla sanaa si halisi na wala haina ukweli zaidi kuliko ukweli wenyewe kwa
kuwa huiga kila kitu katika jamii husika, msanii hurejerea mambo halisi ambayo
hupatikana katika mazingira halisi, na kwa kiasi fulani huongeza ubunifu katika
utunzi wa kazi zake.
Bakari,
Juma A.,& Mterego, Gonche R. 2008. Sanaa kwa Maendeleo :Stadi, Mbinu na
Mazoezi. Moshi:Viva Productions
Comments
Post a Comment