Tafuta utendi wowote kisha onesha mfumo wake wakupagawisha kama unavyoelezwa na plato .
UTANGULIZI
Mulokozi: (1994) anaeleza kwamba utendi ni ushairi wa
matendo. Ni utango mrefu wenye
kusimulia matukio yakishuja awenye uzito
wa kijamii au kitaifa .matokoe hayo
yanaweza kuwa ya
historia ya kisale.
ufafanuzi huu wa mlokozi,, umepiga hatua mbele kwa kueleza
utendi kama ushauri wa matendo . Utendaji hufungamana na matendo wakati wa utendaji
wake , matendo hayo huathirika utendi unapokuwa katika
maandishi .
Plato alizaliwa 427 bk kabla ya kristo alitoke katika
ukoo wa kasomi, alikuwa mshairi
maarufu sana huko ugiriki, plato
alisoma falsafa chini ya mwalimu wake
socrate lakini baadaye alisoma hisabati ,sayansi na sheria .Plato alianzisha academia yake mwaka
387 na alifundisha masomo
sheria, na
sayansi.Kazi alizozitioa ni kama
vile the republic pamoja na law, Plato
alifariki 347 kk
Kwa
kutumia utendi wa fumo Liyongo uliotungwa na bwana Muhamadi
Bin Abubakar bin
Omar Al Bakry
aliyejulikana jina Muhamadi Kijumwa mwaka 1913, umeweza kudhihirisha dhana
ya kupagwisha (mfumo wake kupagawisha) kama iliyoelewa
na Plato.
i)Dhana ya kimungu ; kwa mujibu
wa plato anaamini kwamba mshairi anapata
uwezo wa
kuandika mashairi kutokana
kwa mungu wa sanaa anayeitwa "muses" ambaye ndiye anawapa
jaziba ya kutunga au kuandika mashairi au tendi mbalimbali .- Waashairi wengi
katika kazi zao huaneza kwa kumshukuru mungu wao katika beti zao
mwanzo .mfano katika utendi wa fumo liyongo ulioandikwa
na Mohamedi Kijumwa katika beti za mwanzo aliweza kumushukuru
mungu .
1
. Bismillahi nabutadi
kwa
ina la muhamadi
nandikie
au ladi
nyuma
watakao kuya.
2.Unipe
wino mweusi
na ya shamu karatasi
na
kalama la unyasi
umpe
kuyandikiya
ii) Tungo ndefu; Ni idadi ya uwingi wa beti katita
tungo, kwa mujibu wa plato, anasema kwamba mwandishi akisha
pagawishwa au kupata jazibu ,ndipo
anapata ufunuo au uwezo wa
kutunga tungo ndefu
zaidi .mfano mwandishi Mohamedi Kijumwa (1913)kutokana na
kupagawishwa aliweza kutunga
tungo ndefu zenye
zaidi ya beti
elfu moja katika utendaji wa fumo
liyongo .
iii)kujirudia rudia kwa tungo au mistari
katika beti .plato
anaeleza kwamba kutokana
na mwandishi kupagawisha na
mungu wa sanaa anayeitwa moses anapata
uwezo wa
kuandika kazi wa
msisitizo wa jambo Fulani,
hali imejitokeza katika utendi
wa fumo liyongo katika
beti na 190
na 191
190. Mamakwe wabanwendeya
kwa
lyongo wufe piya
mama
cheri sikiliza
ruhu
zimo hupotera
191 Mamakwe
wakamwendeya
Naye mana
baridhia
Wakatoka kwa umoja
nde
wala sikiliya
katika, beti hisi mbili
msitari wa kwanza wa
kila beti umeweza kufanana
iv)
Msani alishapagawishwa na mungu moses"
- huweza kuandika mambo mabilmbali
ambayo wanajamii hukumbana
nayo .mfano
wa mambo hayo ni
kama vile mapenzi ,utawala
matabaka dhumuna na rushwa .Mwandishi huandika
mambo hayo ili kuwaelimisha
wanajamii kuhusu mambo
hayo na pia huonesha ni ki vipi
jamii itaweza kutatua matatizo hayo .katika utendaji wa
fumo liyongo tunaona linatokea ,Mohamedi kijumwa amewewza kueleza
masuala ya mapenzi katika ubeti
wa 47 .
47. kamuyeya kimtunda
Kwa mahaba kimpenda
Kama wa matoni wanda
Na kwa f`unu na kidaya
Pia
Mohamed kijumwi ameweza kueleza masuala
ya dhuruma katika ubeti
wa 101
101 . Na mamake kwa hakika
Chakula cherna kipika
Asikari humpoka
Chakula wakailiya .
HITIMISHO
Kwa ujumla plato amefanikiwa kueleza ushairi kwa kiasi kikubwa na kutoa maoni na
mapendekezo kuhusu ushairi au utendi, na ametoa mchango
kuhusu sanaa na kuonesha ni
jinsi wasanii walio wengi huweza kupagawishwa
na mungu wao wa sanaa
moses. kwa mfano msaanii
Mohamedi Kijumwa katika
utendaji wake wa
fumo liyongo amedhihikisha
mawazo ya plato .
MAREJEO.
Kijumwa,
M. (1913), Utenzi wa fumo liyongo . Da-
r es salaam : IKR
Mulokozim.,M.M
( 1999 ) , Utenzi Tatu za Kale : Chuo kikuu
cha Dares salaam .TUKI
Comments
Post a Comment