Uhalisia


Senkoro F.E,M.K  (1987) fasihi na jamii  ananukuu Engles  alieulezea  uhalisia kwa  maneno  yafuatayo; “Realism  to  my  implies  besides  truth  of  detail  the  truthful  the  reproduction  of  typical  characters under  typical  circumstances”
Uhalisia ,nionavyo mimi,unamaanisha , zaidi ya  kueleza jambo  katika undani wa ukweli wake , usawirishaji wa kikweli kweli wa   wahusika, mahususi katika mazingira mahususi …,katika  uhalisia basi ,wahusika wa kazi za safihi  husawiriwa  katika uhalisia wa  maisha yao ya kila siku .kusawiriwa  kuna zingatia  furaha  ya mtu ,matamanio yake,matazamio yake huzuni , matatizo na mengineyo .
Kazi za fasihi.ni kazi ambazo hutumia lugha kufikisha ujumbe uliokusudiwa katika jamii husika.wasanii katika jamii zao huweza kutumia lugha katika kuandika yale yaliyopo katika jamii ambayo ni uhalisia  wa maisha ya jamii. msanii huandika  kazi yake kwa kuionya jamii juu ya  maovu na kuitaka  jamii ifuate misingi  iliyo chanya katika kuijenga jamii mpya,hivyo mwandishi hutumia wahusika ambao hubebeshwa uhalisia wa maisha halisi ya jamii yake. kwa kutumia kazi ya takadini iliyoandikwa Ben Hanson  na  kazi ya Mfadhili iliyoandikwa na Hussein Tuwa usawirishaji wa wahusika umejidhihilisha kama ifuatavyo,
Takadini.
Mtoto wa sekai na makwati ambaye nimuhanga wa mila  na desturi  katika jamii  zinazo watenga   walemavu .alizaliwa na ulemavu wa ngozi akatengwa na jamii nzima ambapo sekai anatoloka na  mtoto  wake  takadini  ambapo baadae anapata mke shingai nakupata mtoto  asiye na  ulemavu na  jamii  inashangazwa na maisha takadini  kwamba kuwa mlemavu sio sababu kutopata asiye na ulemavu .pia   katka jamii kuna wtoto wanaotengwa kama alivyotengwa takadini japo nao wanawza  kufanya mambo  kama mtu asye na ulemavu
Sekai
Ni  mama wa takadini ambae nae  muhanga wa mila na desturi kwamba  kupata mtoto mlemavu ni kusasabisha matatizo/balaa katika  jamii.jambo lililopekea  sekai kutoloka kumuokoa mtoto wake  kwahiyo sekai ni mama jasiri na katika jamii  zetu  baadhi ya wanawake wanaujasiri na mapenzi kwa watoto  wao
Makwati
Ni  baba wa takadini ambae ambae amshikria mila  na desturi zisizo faa na zimeptwa  na wakati anamimi   kumpata  mtoto mwenye ulemavu ni chanzo cha  matatizo katka jamii anachukua jukumu la kutaka kumuua mtoto wake hivyo makwati ni baba mkatili na anayefuata  mila na dsturi katka mazingira halisi ya jamii zetu
Mzee  chivelo
Ni mzee aliye mpokea sekai  na mtoto wak takadini na kwnda kuwaomba mtemi masasa na wazee wawapatie makazi wapate kuishi .anaonsha mapenzi  ya dhati kwa  takadini alimtibu alipo vunjwa muguu mpaka akapona pia anaenda  kumuombea aweze kushiriki katika  mashindano kupiga piano pia katika mazingira halisi kuna watu  na mashirika wanatoa msaada kwa watu walemavu.        
Nhamo
Ni kijina aliyefanya unyanyasaji na ubaguzi kwa takadini alimvunja takadini  alimzalau takadini kwa sababu ya ulmavu.ni mtoto aliye pandikizwa na wazazi wake kwamba kucheza na mtoto ni mwiko.kutokana na iman potofu watu katika  mazingira  halisi watu  uwatnga walmavu katika mambo yote ya  kimaisha wasijua nao wanaweza  kufanya kama wengine katka jamii.
Shangai
Ni msichana aliyempenda takadini na anaamua kuolewa na takadini alikuwa na mapenzi ya dhati na jasiri wazazi wake walimkataza  kuolewa na takadini lakini  anachukua  maamuzi kinyume na wazazi na  jamii kwa ujumla.katika uhalisa wa mazingira katika  jamii  wasichana wenye mapenzi ya dhati hawabagui  ulemavu wapo  kwa  ajiri kumpatia mapenz ya kweli na kufurahia ndoa.
Katika kitabu cha mfadhili kilicho andikwa na Hussein  tuwa  anaonesha jinsi uhalisa  ni usawirishaji wa kikwelikweli wa wahusika  halisi katika mazigira halisi  ya wakati maalum.
Mfadhili
Gaddibullah 
Huyu alikuwa muhusika ambaye alijitoa muhunga kwa dania alitoa figo ili dania apate kupona japo walikuwa kwenye  mgogoro  kwa  maana iyo  muhuska gaddibullah  pia ni mchapa kazi anonesha  uhalisia wa watu wenye mapenzi dhati katika jamii.katika jamii kuna watu wanamapenzi ya dhati wapo tayari kujitoa kwa ajili ya kumuokoa mwenzake katika mazingira magumu.
Dania
Ni mschana anayefanya kazi chini ya  usimazi wa mama mlole  anaoneshwa kama  mchapa kazi na muajibikaji , Dania anavurugwa na usaliti alio fanya Jerry kutofika  kwa ajili  kufunga ndoa lakini Jerry anaporudi kuomba msamaha  anasamehe jambo linalosababisha  hata utendaji  wa  kazi unakuwa mdogo na  msongo wa mawazo.Pia  katika jamii wasichana wanajikita katika mapenzi na  ufanisi wa kazi unashuka wanaposalitiwa na wapenzi wao.
Nyambuja
Ni mke wa gaddibullah amechorwa na  msanii katika usaliti  anamuacha mume wake kwa kuandika barua ya kuachana na kuiweka mezani jambo linapelekea mume wake ufanisi wake katika kazi unashuka na msongo  wa  mawazo.Katika jamii kuna wanawake ambao hawana mapenzi ya kweli kwa wanaume wao .
Jerry
Ni mpenzi wake dania walizaa  mtoto aliyeitwa junior ,jerry alimsaliti dania kwa kutofika siku ya kufunga ndoa na kwenda marekani ,pia katika mazinigira halisi wanaume uwasaliti wapenzi wao  bila kujali  wamezaa nae mtoto.kwa iyo  muhusika jerry anasawiri  uhalisa wa uhusika.

Dr veran
Huyu ni muuguzi  anaoneshwa kumuuguza Junior na  Dania walipopatwa na dhoruba ya kuumwa wanapelekwa hosptalini ambako daktari Veran anawajibika kuwauguza na wanapona.Pia alitunza siri  ya  Gaddibullah   ambayo alimsaidia  katika kutoa  figo ili amfadhili dania .hivyo basi katika jamii yate pia tunao  madaktari  ambao wanatunza siri na kuwasaidia  kwa kuwapa matitabu .
Hivyo basi fasihi huchota yanayofanywa na watu  katika jamiii  ili kuonyesha  uhalisia uliomo ndani ya jamii kwa kuwatumia wahusika  kama hao waliotajwa hapo  juu kuonyesha matamanio yao ,mitazamo yao , kero na wakati mwingine majonzi. Kwa  hiyo fasihi  ipo kwa ajili kuelimisha  ,kufunza , na kufurahisha jamii  iliyo  andikiwa  kwa kufuata  yale   yalioandikwa  katika  kazi ya fas

MAREJELEO
Senkoro F.E,M. K  (1987) Fasihi na Jamii  ,Dar es  Salaam: Press  and  Publicity  Centre


Comments

Popular posts from this blog

International Law

KATIBA YA KIKUNDI