Utafiti
UTANGULIZI.
Utafiti
ni uchunguzi unaotumia mbinu za kisayansi katika kutafuta taarifa juu ya jambo
Fulani.Kuna aina mbili za utafiti ambazo ni utafiti wa msingi na utafiti wa
matumizi.
Utafiti
wa msingi hutumika zaidi na wanasansi kama vile wana falsafa ili kukuza
nadharia mbalimbali kwa njia ya ugunduzi wa msingi na kanuni mbalimbali.
Utafiti
wa matumizi ni utafiti unao kazia matumizi ya matokeo ya utafiti huo katika
kutatua matatizo na kufanya shughuli Fulani iwe bora zaidi.
Katika
kazi hii tutatumia aina ya pili ya utafiti ambayo ni utafiti wa matumizi
kulingana na suala la utafiti tulilochagua pamoja na malengo ya suala hilo.
SUALA
LA UTAFITI
UMUHIMU
WA KUWEPO KWA ADHABU SHULENI SHULE YA MSINGI LUPASO MASASI
Mhusika
wa suala tunalolitumia katika kuboresha matokeo ya utafiti ni ndugu Eriyo
Ismail H.ambaye katika utafiti wake alikuwa na malengo yafuatayo:
Malengo
makuu
Utafiti
ulijikita katika kubainisha umuhimu wa kuwepo kwa adhabu mashuleni.
Malengo
mahususi
Namna
ya kutoa adhabu kwa wanafunzi.
Namna
adhabu inavyoweza kuamsha ari ya wanafunzi kujifunza.
Baada
ya kufanya utafiti matokeo ya ripoti ya utafiti yaliwasilishwa kama ifuatavyo:
·
20% ya sampuli waliunga
mkono umuhimu wa kuwepo kwa adhabu mashuleni
·
20% ya sampuli wamesema
kuwa ni sahii kutofautisha namna ya kutoa adhabu kwa waschana na wavulana.
·
20% ya sampuli wamesema
kuwa huamsha ari ya wanafunzi kujifunza
·
15% ya sampuli wamesema
kuwa kuna athari ya kutowepo kwa adhabu shuleni.
·
10% ya sampuli imesema
kuwa adhabu zitolewazo mashuleni hazilingani na makossa ya wanafunzi.
·
15% ya sampuli imesema
kuwa kuwepo kwa adhabu mashuleni ni chanzo cha watoto kutoendelea na masomo.
Kutokana na matokeo ya tafiti saidizi tulio yapata
tumeweza kuandaa mpango wa kuinua ubora wa ujifunzaji na ufundishaji kwa
kuzingatia vipengele vifuatavyo:
MIKAKATI
KATIKA UTOAJI WA ADHABU SHULENI.
Kuwepo
kwa sheria na kanuni zitakazo ongoza utoaji wa adhabu kwa wanafunzi; serikali
pamoja na wadau mbalimbali wa elimu wanapaswa kuona umuhimu wa adhabu na hivyo
kutilia mkazo kwa kuweka sheria na kanuni ambazo mtoa adhabu anapaswa kuzifuata wakati wa kutoa adhabu kwa
mfano kuwepo na utaratibu unao tofautisha namna ya kutoa adhabu kwa mvulana na
mschana mfano mvulana kuchapwa fimbo matakoni na mschana kuchapwa mkononi aidha
utowaji huo wa adhabu hasa ya viboko uzingatie na tofauti za jinsia.
Kuweka
wazi malengo ya utoaji wa adhabu shuleni; Walimu wanapaswa wanapotoa adhabu
kubainisha kwanini wanampa adhabu mtoto kutokana na kosa lililotendeka ili
kuonesha kuwa lengo ni kumuonya au kumuelimisha na si kumkomoa mwanafunzi ili
kumuwezesha kufikia malengo ya kielimu.Mfano mwanafunzi atakae feli atarudishwa
darasa, hivyo itamjenga katika ari ya kusoma kwa bidii.
Kuanisha
aina ya makosa pamoja na adhabu kulingana na kosa hilo;Ili kuwandaa wanafunzi
kuwa na nidhamu nzuri wawapo mazingira ya shule au nyumbani ni vyema wanafunzi
waambiwe makosa na adhabu yake atakayo paswa kupewa mkosaji.Mfano mwanafunzi
akibainika kwa kosa la wizi adhabu ni kusimamishwa masomo kwa muda wa kipindi
Fulani.Hii itasaidia watoto kupatiwa adhabu zinazo lingana na kosa husika.
Adhabu
kutolewa kwa wakati ;Endapo mwanafunzi amefanya kosa mwalimu anapaswa kutoa
adhabu papohapo ili mwanafunzi kutambua kosa alilotenda.Kutofanya hivyo huweza
kusababisha kujengeka kwa uhasama baina ya walimu na wanafunzi kwani mwanafunzi
atahisi ameonewa endapo atasahau kosa lake.
Kuwepo
kwa motisha kwa wanafunzi wenye nidhamu; Uongozi wa shule husika unatakiwa
kuweka siku maalum kwaajili ya kutoa zawadi kwa wanafunzi watakao fanya vizuri
kinidhamu.Hii itafanya wanafunzi kujiweka mbali na makosa kwa lengo la kuwania
zawadi ya nidhamu.Mfano katika shule nyingi kipindi cha mahafali au kufungwa
kwa shule wanafunzi waliofanya vizuri klipindi chote cha mafunzo ndipo
utunukiwa zawadi.
KUWASHIRIKISHA
WADAU KATIKA UTEKELEZAJI WA MIKAKATI YA KUBORESHA MATOKEO YA UTAFITI.
Ili
kufanikisha mikakati tuliyo ipanga tunapaswa kushirikisha wadau tofauti tofauti
wa elimu kwa namna zifuatazo.
Kuwepo
kwa vikao vya mara kwa mara; Uongozi wa shule upange siku za vikao vya shule
vya mara kwa mara kwa kila mwezi ili kufanya tathmini za maendeleo ya kinidhamu
ya taaluma shuleni na hata nyumbani .Hivyo wadau kwa kupitia vikao huweza kutoa
maoni yao katika kudhibiti nidhamu kwa wanafunzi.Mfano kupanga adhabu
zinazostahiki kutolewa kwa wanafunzi.
Kuwepo
kwa semina elekezi kwa walimu kuhusu utoaji wa adhabu; walimu wapatiwe mafunzo
ya ndani yanayohusu namna bora ya kutoa adhabu kwa wanafunzi ili kuzingatia
wakati sahihi wa utoaji wa adhabu,namna sahihi,adhabu sahihi kuzingatia jinsia
na kuepuka utoaji wa adhabu kwa kuongozwa na hasira.Kwahiyo utoaji wa adhabu
uweze kuzingatia sheria na taratibu sahihi kwa mwanadamu.
Kutoa
elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa adhabu kwa mwanafunzi;walimu kwa kushirikiana
na serikali wanatakiwa kuweka vikao na wanajamii kwa ajili ya kutoa elimu juu
ya adhabu kwa wanafunzi kwani kuna wazazi wengine huwa wanakuja juu pale watoto
wao wanapopatiwa adhabu shuleni.Mfano kuna wazazi wanadiliki kwenda shuleni
kutoa maneno makali kwa walimu pale wanapopata taarifa kuwa mtoto wake
kaadhibiwa na hii yote ni kwa sababu huwa hawajui ni kwanini walimu huwa
wanatoa adhabu kwa wanafunzi pindi wanapokosea na elimu hii inaweza kuwasaidia
wazazi kutoa adhabu pindi watoto wao wanapokosea wawapo nyumbani.
Kuhamasisha
vyombo vya habari kuelezea kuhusu adhabu;kwenye vyombo vya habari kama vile
redio,magazeti na televisheni viwepo vipindi vinavyotoa mafunzo kuhusu utoaji
sahihi wa adhabu au kutoa taarifa kuhusu madhara ya utoaji wa adhabu pasipo
kuzingatia sheria na kanuni.Kwa mfano taarifa za mwalimu aliyechapa mwanafunzi
hadi kufa zilipotolewa walimu wengi walijifunza kutokana na hilo hivyo
imepunguza kasi kwa walimu wenye kutoa adhabu bila mpangilio.
KUSIMAMIA
UTEKELEZAJI WA MIKAKATI YA KUBORESHA ELIMU
Kutunga
sheria na kuweka kanuni,kuzisambaza kwa watumiaji na kuhuakikisha zinzfuatwa kama
zilivyokusudiwa.Ili kusimamia mkakati huu serikali inapaswa kutunga sheria
ambazo zitawaongoza walimu katika kutoa adhabu pamoja na kuzisambaza sheria
hizo ili ziweze kutumika na kila mtu.
Kutoa
adhabu zenye uwiano na makosa;ili kupunguza kasi ya wanafunzi kukimbia shule
walimu wanatakiwa kutoa adhabu kulingana na makossa yanayofanywa na
wanafunzi,kwa mfano mwanafunzi akipigana na mwenzake asipewe adhabu kubwa kama
kuchimba visiki au kukusanya ndoo nyingi za kokoto kwani adhabu kama hizi
zinawapelekea wanafunzi kuacha shule na hivyo kutofikia malengo ya elimu.
Kuwaadhibu
wanafunzi pale tu wanapokosea ili kutowaharibu kisaikolojia;walimu hawana budi
kutoa adhabu pindi tu wanafunzi wanapokosea kwani kuchelewesha adhabu kunaweza
kuwaathiri kisaikolojia.kwa mfano mwanafunzi anapokosea na akafahamu kuwa
amekosea asipopatiwa adhabu anaweza kukosa amani kwani hajui atapatiwa adhabu
gani au muda mwingine anaweza kusahau kosa na atakapopatiwa adhabu atahisi
ameonewa na hivyo kuharibiwa kisaikolojia.
Kugawa
madaraka kwa walimu ili kurahisisha ufuatiliaji wa nidhamu shuleni;shule
inatakiwa kugawa madaraka kwa kuunda kamati mbalimbali kwa kufanya hivyo
kutarahisisha ufuatiliaji wa wanafunzi katika sekta mbalimbali.kwa mfano kamati
ya nidhamu itafuatilia nidhamu,kamati ya taaluma itafuatilia taaluma,kamati ya
afya itafuatilia mambo ya afya hivyo kufanya wanafunzi kuweza kufuatiliwa kwa
urahisi katika ngazi zote.
Kuwepo
na siku maalumu za kutoa tuzo kwa wanafunzi wenye nidhamu;uongozi wa shule
unatakiwa kupanga siku ya kutoa zawadi kwa wanafunzi kwa kufanya hivi
kutawasaidia walimu kupata wanafunzi wenye nidhamu na kupunguza wanafunzi wasio
na nidhamu.kwa mfano siku za kufunga shule au za mahafali zawadi zikitolewa
wanafunzi wanapatwa na hamasa ya wao kuwania zawadi.
KUFANYA
TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA KUINUA UBORA WA ELIMU
Tathmini
ni kitendo cha kutaka kujua ni kwa kiasi gani jambo lilikusudiwa kutekelezwa
limefikia mafanikio au la.kuna aina nne za tathmini ambazo ni
Tathmin
ya awali
Tathmini
endelevu
Tathmini
tatuzi
Tathmini
tamati
Katika
kutathmini matokeo ya utafiti tumetumia tathmini tatuzi na tumetumia tathmini
tatuzi kwa lengo la kuboresha matokeo ya utafiti katika kuinua ubora wa elimu
na baada ya kutekeleza mikakati iliyopangwa tunapata majibu kuwa adhabu
zimeleta mabadiliko baada ya wanafunzi
kuomgeza ari ya kujifunza na hatimae kupanda katika taaluma,kuimarika
kimaadili pamoja na kuongeza ushirikiano baina yao na kupunguza utoro
mashuleni.
HITIMISHO
Kulingana
na mipango ya kuboresha elimu tuliyoipanga ni matarajio yetu kwamba adhabu ni
chachu pekee inayoweza kumfanya mwanafunzi kubadilika katika mtazamo chanya na
kuwa mzuri kinidhamu taaluma na maadili na hatimaye kuja kuwa mtendaji bora
hapo baadae kwa ajili yake na taifa kwa ujumla ikizingatia adhabu hasi au
chanya.
MAREJEO.
Pletty
rogic.(2009) usimamizi wa nidhamu na maadili kazini.Zanzibzar
Eriyo
I.(2018) Umuhimu wa kuwepo kwa adhabu mashuleni.Stemmuco Mtwara.
Comments
Post a Comment