mfano barua ya kaz Call & Vision Secondary school
Klement
Lambe
S.L.P
777,
MTWARA
23/09/2019
Mkurugenzi,
Call & Vision Secondary school
P.O.Box 524,
MTWARA
Yah: Ombi la nafasi ya kazi
Rejea kichwa cha habari hapo juu.
Mimi ndugu Klement Lambe Mwalimu niliyehitimu mafunzo yangu
ya Shahada ya kwanza ya Ualimu katika Chuo kikuu cha Stella Maris Mtwara
(STEMMUCO) na kufaulu kwa daraja la juu (Upper Second) kama inavyoonesha katika
matokea yaliyoambatanishwa na barua hii.
Kwa heshima kubwa, ninapenda kuomba nafasi ya kazi ya
kufundisha katika shule yako ya Call & Vision ili kuweza kusaidiana nanyi katika kuinua
kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi na kuitangaza shule.
Ni matumaini yangu kuwa ombi langu litakubaliwa.
Naambatanisha barua hii pamoja na Nakala za vyeti vyangu vya elimu ya secondari
ya awali na ya juu , pamoja na wasifu wangu kwa taarifa zaidi.
Wako katika ujenzi wa Taifa
Klement Lambe
Simu: 0787999578
Comments
Post a Comment