SW111: UTANGULIZI WA MISINGI YA ISIMU
CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA STELLA MARIS
MTWARA

|
|

KITIVO CHA ELIMU
IDARA YA KISWAHILI
SW111: UTANGULIZI WA MISINGI YA ISIMU
SEMISTA YA KWANZA: 2019/2020
Utangulizi
Hii ni kozi ya utangulizi inayoweka msingi wa kumwezesha mwanafunzi
kuielewa isimu kama taaluma; muundo wa mfumo wa lugha na jinsi lugha
inavyofanya kazi. Ni kozi inayolenga hasa kumwezesha mwanafunzi kuelewa
uchangamano wa lugha ya binadamu kama mfumo unaoongozwa na kanuni za lugha kwa
jumla na kanuni za lugha maalumu.
Malengo ya Kozi
Kozi hii imenuiwa kumwezesha mwanafunzi:
a) Kuieleza isimu kwa kufafanua viwango na
matawi yake.
b) Kueleza kitaaluma maana ya lugha, sifa
zake, na kutathmini nadharia mbalimbali za asili ya lugha.
c) Kuchambua, kuchanganua na kuziainisha
sauti zinazopatikana katika lugha za binadamu; usikiaji na utamkaji wake.
d) Kuchunguza kuchambua na kuainisha sauti
pambanuzi ambazo hutumika katika mifumo mbalimbali ya sauti za lugha za
binadamu.
Matokeo ya Ujifunzaji
Kufikia mwisho wa kozi hii, mwanafunzi ataweza:
a) Kueleza kitaaluma maana na sifa za lugha.
b) Kufafanua viwango na matawi ya isimu.
c) Kutathmini nadharia mbalimbali za asili ya
lugha.
d) Kuainisha sauti zote za lugha ya binadamu
katika makundi na kuzitolea sifa ambazo zinaweza kutofautisha sauti moja na
nyingine.
e) Kuainisha sauti pambanuzi ambazo hutumika katika
mifumo mbalimbali ya sauti za binadamu.
Kiunzi cha kozi
1.0 Utangulizi
1.1 Maana na sifa za lugha
1.2 Asili ya lugha
1.3 Sifa bia za lugha
1.4 Maana na malengo ya Isimu
1.5 Usayansi wa Isimu
1.6 Historia ya taaluma ya Isimu
2.0 Tanzu za Isimu
2.1 Viwango vya simu
2.1.1 Fonetiki
2.1.2 Fonolojia
2.1.3 Mofolojia
2.1.4 Sintaksia
2.1.5 Semantiki na
Pragmatiki
2.2. Matawi ya
Isimu
2.2.1.Isimu Historia
a) Isimu Elekezi
b) Isimu Elezi
2.2.2 Isimu Jamii
2.2.3 Isimu Linganishi
2.2.4 Isimu Tumizi n.k
3.0 Fonetiki
3.1 Dnana ya
Fonetiki
3.2 Matawi ya
Fonetiki
3.3 Fonetiki
Matamshi
3.4 Ala za
Matamshi
3.5 Uanishaji
wa sauti za lugha
3.6 Alfabeti ya
Kifonetiki ya Kimataifa (AKIKI)
4.0 Fonolojia
4.1 Dhana ya
Fonolojia
4.2 Vipashio
vya kifonolojia: Fonimu na Alofoni
4.3 Majukumu ya
Fonolojia
4.4 Uhusiano
kati ya Fonetiki na Fonolojia
4.5 Tofauti
kati ya Fonetiki na Fonolojia
Marejeo
Habwe, J.H. na Karanja, P. (2004), Misingi ya Sarufi ya Kiswahili.
Nairobi: Phoenix Publishers
Massamba, D.P.B., Kihore, Y.M., & Msanjila,
Y.P. (2004). Fonolojia ya Kiswahili Sanifu. Dar es Salaam: TUKI.
Mdee, J.S. (1988). Sarufi ya Kiswahili: Sekondary na Vyuo. Dar es Salaam: Dar es
Salaam University Press.
Mohammed, M.A. (2001). Modern Swahili Grammar. Dar es Salaam: East African Educational
Publishers.
Mgullu, R. S. (2002). Mtalaa wa Isimu, Fonolojia, na Mofolojia ya Kiswahili.
Nairobi: Longhorn.
Njogu, K. et al. (2006). Sarufi ya Kiswahili: Uchanganuzi na Matumizi. Nairobi: The Jomo
Kenyatta Foundation.
Nkwera, F. (1978). Sarufi na Fasihi: Sekondari na Vyuo. Dar es Salaam: Tanzania
Publishing House.
O’Grady, W. et
al. (1996). Contemporary Linguistics:
An Introduction. London: Longman.
Oduor, J.A. (2012). Teaching Pronunciation in
Secondary Schools in Kenya: The Necessity to Use the Right Information and
Descriptive Tools. The University of
Nairobi Journal of Language and Linguistics, Vol. 2. June, 2012. Kurasa 1 –
41.
Robins, R. (1984). A Short History of Linguistics. New York: Longman.
TUKI (1990). Kamusi
Sanifu ya Isimu na Lugha. Dar es Salaam: Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili,
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Yule, G. (1996). The Study of Language. Cambridge: Cambridge University Press.
Tathmini
Tathmini ya somo itahusisha mahudhurio ya wanafunzi
katika mihadhara, insha, alama za majaribio (40%) na alama za mtihani wa mwisho
(60%)
Comments
Post a Comment