SWALI: “Ili pawe na Riwaya ya Kiswahili hapana budi pawepo na jamii yenye lugha hiyo’’.Huku ukizingatia kauli hiyo,ijadili hali ya riwaya nchini Tanzania. 1.0: UTANGULIZI.


SWALI: “Ili pawe na Riwaya ya Kiswahili hapana budi pawepo na jamii yenye lugha hiyo’’.Huku ukizingatia kauli hiyo,ijadili hali ya riwaya nchini Tanzania.
1.0: UTANGULIZI.
Riwaya;          
Ni hadithi ya kubuni na iliyojengwa juu ya tukio la kihistoria na kuandikwa kwa mtindo wa ushairi iendayo katika mfululizo wa kinaganaga katika kuelezea maisha ya mtu,watu na hata taifa .
Kutokana na maana ya Riwaya wataalamu mbalimbali  wameweza kutoa fasili tofauti tofauti juu ya dhana nzima ya Riwaya nchini Tanzania kama ifuatavyo,
Riwaya, ni kazi ya sanaa ya kubuni yenye nathari (ujazo) yanayosimulia  hadithi ambayo kwa kawaida ina uzito, upana na urefu wa kutosha mara nyingi huwa wahusika mbalimbali, wahusika wanatabia aina nyingi,huwa na migogoro mikubwa na midogo ndani yake.Mbunda M.(1992).
            Wamitila,(2003), Riwaya ni hadithi ya kinathali au bunilizi ambayo huwa na urefu wa kutosha msuko uliyojengeka vizuri, wahusika wengi waliondelezwa kwa kina yenye kuchukua muda mwingi katika maandalizi yake ikihusisha madhari maalumu.
            Madumulla, (2009), Riwaya ni masimulizi ya kubuni yaliyo katika mtindo wa kubuni yakisawili mtindo maalumu na madhumuni maalumu.Mhusika katika riwaya anakuwa kipaza sauti cha maandishi.
 Kwa ujumla;
Riwaya, ni masimulizi ya kubuni ya kinathari yenye msuko au mpangilio fulani wa matukio au ploti inayofungamana na wakati au kusawili wakati na yenye visa vyingi vinavyotendeka  katika wakati Fulani na yenye mawanda mapana yenye mchangamano wa dhamira visa na wahusika pia riwaya ni hadithi ndefu yenye uwezo wa kutosha kufanya kitabu kimoja au zaid.i
Riwaya ya Kiswahili,ni Riwaya  ambayo inayofungamana na utamaduni wa jamii wa Kiswahili katika lugha ya Kiswahili asili ambayo hupatikana katika nchi ya Afrika mashariki,pia ni ile Riwaya ambayo inawahusu waswahili wenyewe.

1.2 Historia katika  Riwaya ya Kiswahili;
Tanzu za asili zinaonyesha kuwa Riwaya  ndio zilichangia kwa kiasi kikubwa riwaya za Kiswahili.kuna wataalamu mbalimbali wamejadili kuhusu historia ya riwaya kama ifuatavyo,
 Madumilla(2009), ameeleza kuwa chimbuko la  riwaya lilitokana na nathari bunifu simulizi kama vile hadithi, hekaya  na ngano inayosimuliwa kwa mdomo.Anaendelea kusema kuwa fasihi ilitokana na maandiko ya fani ya ushairi hususani ni   tendi za Kiswahili katika hati za kiarabu kwa sababu ndiyo maandishi yaliyotamba katika pwani ya Afrika mashariki,wazungu na waarabu hawakubadilishana maarifa kwa urahisi na hivyo pakapelekea kuwa na majilio ya taratibu za maandiko ya kinathari,mwanzani Riwaya zilitafsiriwa toka katika lugha za ulaya na kufanya Riwaya za za Kiswahili kutokea.Mfano wa riwaya hizo ni kama vile,Habari za mlima iliyoandikwa na Sheikh Ali Bin Hemed (1980).
Mulokozi,(1996) anaeleza kuwa riwaya Kiswahili ipo katika mambo makuu mawili ambayo ni fani za kijadi za fasihi mfano Riwaya za kingano,tendi,hekaya,visakale,historia,sira,masimulizi ya wasafiri,insha na tafsiri.Pia riwaya ya kiswahili imetokana na mazingira ya kijamii mfano njaa,migogoro,masuala ya kisiasa pamoja na kiuchumi.
 Hali ya riwaya nchini Tanzania kisiasa,
 Waandishi  mbalimbali wameandika kazi mbalimbali zinazozungumzia maswala ya kisiasa riwaya zinazoeleza hali ya watu kutaka kupinga au kukubaliana na uongozi fulani mfano, Shabani Robert katika riwaya yake ya Kusadikika ameeleza dhamira mbalimbali zinazohusika katika jamii mfano, uongozi mzuri.amemtumia Bunihari kama kiongozi  bora anayesimamia haki za jamii.uongozi mbaya pia  katika riwaya ya Kusadikika, amemchora waziri mkuu kama kiongozi mbaya. Hivyo ndivyo  hali riwaya ilivyo kisiasa katika nchi ya Tanzania.
Kiutamaduni;
 Hali ya riwaya ya Kiswahili nchini Tanzania kiutamaduni, riwaya mbalimbali zimeandikwa kueleza hali mbalimbali za kiutamaduni nchini Tanzania ambapo riwaya hizo zimeelezea uhusiano baina ya mila na desturi , mfano Mung’ong’o,C.G. katika kitabu chake cha Mirathi Ya Hatari k ameelezea mila na tamaduni za jamii katika kurithisha tamaduni  amemtumia mhusika wake  Guston ambae ameeleza kuhusu mila na tamaduni za kichawi baada ya wazazi wake kufariki hii inaeleza uhalisia hata watu watanzania walio wengi wanarithishana tamaduni hizo mfano kabila la Wasukuma,Wamasai  huwarithisha mila zao ili waweze kuishi na kuuenzi utamaduni wao.
Kijamii;
  Riwaya mbalimbali zimeandikwa kuelezea hali ya matatizo yanayowakumba wananchi katika maisha halisi ya kila siku mfano ukosefu wa maji, hali duni ya maisha, mazingira magumu ya kufanyia kazi, mazingira mabaya ya kuishi na hali ya umaskini.mfano, mwandishi Muhammed S. Abdulah katika kitabu chake cha Mzimu wa Watu wa Kale,(1996) ameeleza masuala mbalimbali ya kijamii. mwandishi ameeleza maisha ya bwana Musa ambae anaishi katika hali duni pia anaishi kwa kujibana, nyumba anayoishi ni ya kimasikin vitu vimejipanga ovyo ovyo hii inaonesha uhalisia wa maisha na kuonesha watanzania wanavyo pambana na kutokana na hali ngumu ya maisha kujiweka katika hali nzuri ya maisha.
Hali ya riwaya kiuchumi;
Riwaya nchini Tanzania imeonesha pia maendeleo makubwa katika nyanja mbalimbali za kiuchumi.mfano katika kitabu cha Mzimu wa Watu wa Kale kilichoandikwa na Mohammedi S. Abdullah amejaribu kuonesha suala la kiuchumi jinsi lilivyo katika jamii, mfano, tunamuona Bwana mussa alipokuwa akiishi maisha duni kama vile kukosa chakula pia hata nyumba aliyokuwa anaishi haikuwa bora .pia tunamwona bwana Alli alimposa mwanamke akashindwa kutoa mahari na kuishia kutoa ahadi tu, hivyo basi imenajidhihirisha wazi kuwa hali ya kiuchumi haikuwa nzuri.
           
Mandhari au mazingira; Riwaya nyingi za Kiswahili zinaandikwa kwa kuzingatia mazingira ya jamii husika ya watanzania .pia katika matumizi ya madhari riwaya nyingizinatumia madhari ya kubuni riwaya nyingi zinatumia madhari kama maisha mbani mito makaburi jangwani mfano katika riwaya ya nagona ametumia madhari ya kubuni na halisi kama makaburi jangwani na za kimaujiza.
            Matumizi ya lugha ; riwaya nyingi za Kiswahili zinatumia lugha ya Kiswahili ambayo inaeeleweka na jamii nyingi za watanzania katika kufikisha ujumbe wakusudiwa kwa jamii husika mfano riwaya za Kusadikika,Mzimu wa Kale na Moto wa Mianzi zimetumia lugha ya Kiswahili ambayo inaeleweka na jamii za watanzania.

Kutokana na hali ya riwaya nchini Tanzania kwa miaka kadhaa iliyopita na tokea muda wa kupata uhuru riwaya ya Kiswahili imeweza kuleta mabadiliko mbalimbali katika nyanja za kijamii,kisiasa,kiutamaduni pamoja na kiuchumi.Japokuwa riwaya ya Kiswahili imeweza kuleta mabadiliko hayo lakini zipo changamoto mbalimbali ambazo zinaikumba riwaya ya Kiswahili nchini Tanzania matatiza hayo hujitokeza kupitia suala la uandaaji,uchapishaji,usambazaji pamoja na usomaji wa kazi mbalimbali za riwaya ya Kiswahili.





Comments

Popular posts from this blog

Historical Background Of Tanzania Revenue Authority (TRA)

It's true that agriculture is a change agent in Tanzania development due to the following reasons;