Zifuatazo ni hoja zinazoonesha hali ya riwaya nchini Tanzania.
Riwayani
hadithi ndefu ya kubuni yenye wahusika wengi na yenye kueleza maisha ya watu
katika jamii yenye mazingira maalumu yanayochaguliwa na mwandishi, kwa kawaida
huwa na visa vingi na hutumia lugha ya kinathari. Ili hali riwaya ya Kiswahili
ni riwaya ambayo imeandikwa kwa lugha ya Kiswahili, huandikwa katika utamaduni
wa mswahili na katika eneo la mswahili. Chimbuko la riwaya ya Kiswahili
lilitokana na mambo makuu mawili ambayo ni fani za kijadi na mazingira mahususi
ya kijamii, hizi ni riwaya zinazohusisha fani mbalimbali za kijadi kama vile
ngano, hekaya, utendi, visasili, insha, sira na masimulizi ya kihistoria. Hivyo
riwaya ziliendelea kutoka masimulizi hadi kuandikwa, hivyo basi riwaya ya
kwanza kuandikwa ni riwaya ya UHURU WA WATUMWA (Mbotela 1934). Kwa ujumla ni
kweli kuwa ili pawe na riwaya ya Kiswahili hapana budi pawepo na jamii ya lugha
hiyo.
Zifuatazo
ni hoja zinazoonesha hali ya riwaya nchini Tanzania.
Wahusika
ni viumbe hai au visivyohai ambao hutumika kuwakilisha matendo, mwenendo au
tabia za binadamu wa kweli katika jamii, viumbe hawa ni wale wanaopatikana
katika kazi ya fasihi. Mfano: fisi anaweza kuwa mhusika katika kazi ya Fasihi
ambapo huweza kuwakilisha binadamu waroho na wajinga, waandishi wengi wa riwaya
ya Kiswahili hutumia wahusika ambao majina yao hupatikana katika jamii ya
watanzania na kuweza kusawiiri yaliyomo katika jamii. Pia matendo yao na majina
yao ni yale ambayo yanapatikana katika jamii ya Tanzania. Mfano: Katika riwaya
ya “rosa mistika” iliyoandikwa na Euphrase Kezilahaba pamoja na riwaya ya “MIRATHI
YA HATARI”iliyoandikwa na C.G Mung’ong’o waandishi hawa wametumia majina ya
wahusika ambayo yapo katika jamii zeu, kama vile, Rosa,
Nandi, Rina, Gusto, Zakaria, Deogratius ambapo wahusika hawa wamebeba uhasika
wa kutenda mambo yanayo sawiri katika jamii. Pia riwaya ya “WATOTO WA
MAMANTILIE” iliyoandikwa na Emmanuel Mboga, tunapata wahusika kama Musa,
Zainabu, Kurwa na Doto, Peter na mzee Lomolomo kupitia uhusika wao tunaweza
kupata dhamira inayo sawiri hali halisi ya jamii ya Tanzania.
Hivyo
basi riwaya za sasa zinazidi kuendelea kutokana na kwamba huonyesha moja kwa
moja tofauti na riwaya za zamani ambapo zilikuwa zinatumia wahusika wa mficho
ambao si wa moja kwa moja. Mfano: katika riwaya ya “KUSADIKIKA” Mwandishi
ametumia wahusika kama “Mizimu” wakati riwaya za Kiswahili zilizo kuwa
zinaandikwa zamani zilikuwa zinaandikwa kusawiri maisha ya jamii ya kipindi
hicho na jinsi zilivyokuwa zinaathiri maisha yao. Mfano: riwaya ya
“KUSADIKIKA(1957)” ilikuwa inaelezea jinsi watu walivyo kosa uhuru wa
kuzungumza au kuhoji kuhusu masuala mbalimbali ya nchi kama vile kupata nyazifa
za uongozi au kuhoji matumizi ya rasilimali za nchi lakini baada ya uhuru,
riwaya zinazoandikwa saizi zinaendana na wakati na mabadiliko ya jamii za sasa.
Mfano: riwaya ya “ROSA MISTIKA (1997) Inaelezea masuala ya mapenzi na ulevi
ambayo ukiyaona yameshamiri jamii zetu za leo. Hivyo waandishi wengi wa riwaya
za Kiswahili nchini Tanzania huandika kazi zao za riwaya kulingana au kufuatana na hali halisi inayoendalea katika
kipindi hicho au wakati huo wa maisha ya watanzania. Vipindi hivyo vinaweza
kuwa vya kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni.
Mandhari ni sehemu ambayo tukio
linafanyika katika kazi ya fasihi. Katika kazi ya fasihi mandhari yanaweza kuwa
halisi au ya kubuni. Riwaya mbalimbali za Kiswahili hutumia mandhari tofauti
tofauti ambayo husadifu mazingira halisi ya Waswahili, waandishi mbalimbali wa
riwaya za Kiswahili wametumia madhari mbalimbali. Mfano: mwandishi wa riwaya ya
KUSADIKIKA (Shaban Robert 1957) ametumia madhari ya kaburi kama vile madhari ya
mbinguni, ambayo yalitokea katika nchi ya kusadikika pia mwandishi wa riwaya ya
WATOTO WA MAMA N’TILIE (Emmanuel Mboga 2002) ametumia mandhari halisi
yanayopatikana katika jamii ya waswahili nchini Tanzania, mwandishi ametumia
madhari ya jiji la Dar es salaam na mitaa yake mbalimbali kama vile kisutu,
manzese, kiwanda cha urafiki na dampo la Tabata, hivyo Emmanuel Mboga
amefanikiwa kujadili matatizo yanayoikabili jamii kwa kutumia mandhari halisi
yaliyojitokeza katika riwaya hiyo. Kwa hiyo hali ya riwaya za Kiswahili nchini
Tanzania ni nzuri ukilinganisha na riwaya za zamani kwa sababu waandishi wa
riwaya za sasa wanatumia mandhari ambayo yanaendana na utamaduni wa waswahili.
Ubunulizi ni ujuzi alionao mtunzi
kwa kubuni na kuigiza au kutumia kazi yake ili ilete mvuto kwa hadhira. Mbinu hii
huakisi kipawa cha utunzi alichonacho mtunzi na kumtofautisha na watu wengine katika riwaya za Kiswahili
waandishi wametumia ubunifu katika kazi zao za fasihi. Mwandishi wa MIRATHI YA
HATARI (C.G.Mung’ong’o) ametumia dayalojia katika ukurasa wa 19, mazungumzo
kati ya Gusto na Mzee Mavengi yanayohusu usihiri (ushirikina)
Mzee
Mavengi: “unaziona shanga hizi?”
Gusto:
Ndiyo
Pia
mwandishi ametumia methali, nahau, matambiko na vyakula asilia kama vile mboga
ya kuchemsha na viazi vya kuchemsha (uk. 03). Vilevile katika riwaya ya WATOTO
WA MAMA N’TILIE (E. Mboga) katika
kukamilisha kipengele cha ubunifu ameweza kutumia Nahau “kupiga usingizi”
tamathali za semi kama vile Tashibiha mfano: akaanguka chini kama mzigo (uk 12)
Kwa hiyo waandishi wa riwaya za
Kiswahili kwa sasa wanaubunifu kama riwaya za
mwanzo hivyo riwaya hizi zimeweza kuwa mwanzo hivyo kutokana na juhudi
za waandishi kuwa wabunifu katika kazi zao.
Usawilishaji ni namna ambayo
waandishi wa riwaya za Tanzania wanavyoonesha uhalisia wa maisha ya watu katika
jamii mbalimbali mfano: Hali ngumu ya maisha, ulevi, Dhuluma, Unyonyaji,
Mapenzi, Matabaka, Mambo ya kisiasa. Mfano: tukiangalia katika riwaya ya Rosa
Mistika mwandishi amezungumzia suala la mapenzi jinsi mtu anavyoharibika kutokana
na mapenzi. Mfano: Rosa ambaye anajiingiza katika mapenzi na kumletea athari
mbalimbali katika masomo yake. Pia katika riwaya ya watoto wa Mama Ntilie
(2002) mwandishi anazungumzia hali ngumu ya maisha ambapo wazazi wanashindwa
kuwalipia watoto wao ada ya shule pamoja na
kuwanunulia sare za shule, ambapo imepelekea watoto kukosa elimu na
kujiingiza katika masuala ambayo yanawaletea athari katika maisha yao. Pia
suala la ulevi katika riwaya hii ya Watoto wa Mama ntilie mzee Lomolomo
anajihusisha na ulevi na anashindwa kulea familia yake kwa sababu pombe
zimemtawala na mwisho wa siku pombe hizohizo zinakuja kumuua. Hivyo waandishi
wa riwaya za kitanzania wanasawili maisha halisi ya kitanzania.
Mawanda
mapana, riwaya nyingi za Kiswahili huandikwa kwa kuangalia vipengele vingi
katika jamii kama vile masuala ya
kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni na kijamii. Ili kufikisha ujumbe uliokusudiwa
kwenye jamii husika na katika Nyanja zote za maisha katika jamii kwa mfano
riwaya ya kusadikika mwaka (1957/58) iliandikwa ili kulenga Nyanja zote za
kimaisha kama vile ujenzi wa miundombinu (kiuchumi), ujenzi wa zahanati
(kijamii) na kuhusu masuala ya kiutawala (kisiasa) katika masuala ya kiuchumi
hii imedhihirishwa katika ukurasa wa 43 mandishi anasema kuwa hii kusadikika
ilikuwa haina haja ya kutengeneza bandari wala viwanja kwa ajili ya vyombo ya
aridhi. Pia katika riwaya sasa kama vile watoto wa mama Ntilie (2002) mwandishi
ametumia mawanda ya kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni katika kuandika kazi yake
kwani amesawiri hali ngumu za maisha, ulevi ana uchezaji wa ngoma za
kiutamaduni, hivyo basi ni dhahili kuwa riwaya ya Kiswahili kwa sas inaandikwa
kwa kuangalia Nyanja zote za kimaisha.
Kwa
ujumla riwaya ya Kiswahili nchini Tanzania imeendelea kwa kasi sana baada ya
kugunduliwa kwa mashine za uchapishaji na kuwepo kwa taasisi mbalimbali za
uchapishaji wa kazi hizo. Mbali na kuwepo kwa changamoto mbalimbali ,kwa
waandishi kama vile kuyumba kiuchumi na kutumia maneno mengi ya lugha za
kigeni, ili hali kazi zinaandikwa kwa watumiaji wa Kiswahili.
REJEA.
Kezilahabi
E. (1988) Rosa mistika: Kenya
literature Bureau
Mbogo
E. (2002) watoto wa mama ntilie: Heko
Mung’ong’o
C. G (1977) mirathi ya hatari:
Tanzania Publishing house.
Robart
S. (1957/58) kusadikika: Mkuki na
nyota
Comments
Post a Comment