Dhana ya Mabadiliko
Dhana
ya Mabadiliko, ni uwingi wa nomino Badiliko ambalo kwa mujibu wa TUKI (2004).Ni
hali inayokuwepo baada ya kutokea mageuzo fulani.ni hali ya kuwa na tabia
tofauti na mwanzo.Kila kitu katika ulimwengu huwa kipo katika hali ya
mabadiliko.
Mabadiliko ya Maana,ni kubadilika kwa maana ya
neno katika lugha kutegemeana na
muktadha na matumizi ya neno husika katika lugha fulani,lugha zote ulimwenguni
hubadilika kutokana na wakati. Heiko Narrog (2012).
Kwa
ujumla mabadiliko ya maana ni muundo wa mabadiliko ya lugha kutegemeana na
maneno yanavyotumika katika lugha,pia hutegemeana na muktadha na matumizi ya neno husika katika
lugha.Mawazo ya Heiko Narrog (2012). Ya mabadiliko ya maana katika lugha ya
Kiswahili yanajitokeza kama ifuatavyo;
Heiko Narrog (2012). Anadai kuwa mabadiliko ya
maana huenda sambambana na dhana ya polisemia,
kuwa dhana ya
Polisemia hutumika pale neno moja lina maana zaidi ya moja kimsingi katika uzungumzaji wa binadamu. Mwanadamu hulazimika
kutafuta dhana zenye chimbuko moja au zinazohusiana
kimaana akazipa neno moja tu liziwakilishe. Hivyo katika lugha tunapata neno moja tu likiwakilisha
dhana kadhaa zilizo na uhusiano wa namna fulani. Pia unaweza kuchukua
maneno ambayo hapo zamani yalikuwa yakiwakiliza dhana fulani yakaweza sasa
kuwakilisha dhana mpya.
Mifano ya maneno; kichwa
Sehemu ya mwili
Dhana ya uongozi
Cha insha
Anadai kuwa mabadiliko ya maana hujihusisha
na upanuaji wa maana ya neno, Heiko Narrog (2012).anasema kuwa mabadiliko
ya kisemantiki au ya maana huenda sambamba na
kupanua wigo wa mpana wa maana ya neno na kutumika katika nyanja
mbalimbali ,mwanaisimu huyu alitoa mifano kutoka lugha mbalimbali kama vile
kingereza ,kihindi na kigiriki.mfano katika lugha ya kingereza;
Neno mbwa (dog) mala ya kwanza lilikuwa
linatumika ni kama jina la mndege mwenye nguvu,baadae maana likabadilika na
kutumika kwa ndege wote bila kujali nguvu hivyo ni kutokana na mabadiliko ya
maana.katika lugha ya Kiswahili mawazo haya yanadhihilika kutokana na neno kama
vile;
Shoga;kwa mala ya kwanza neno hili
lilitumika kama rafiki wa kike kutokana na kupanuka kwa maana tunapata maana
nyingine ambayo ni mwanaume anaejihusisha na mapenzi ya jinsia moja.
Anadai
kuwa mabadiliko ya maana hujihusisha na ufupishaji wa maana ya neno,
Haiko Narrog (2012).anasema kuwa mabadiliko ya kisemantiki au ya maana huenda
sambamba na kupunguza wigo wa mpana wa
maana ya neno na kutumika katika kiwango kidogo ,mwanaisimu huyu alitoa mifano
kutoka lugha mbalimbali kama vile kingereza na kigiriki.mfano katika lugha ya
kingereza;
Neno; undertaker,kwa mala ya kwanza
lilikua linatumika kama mtu mwenye nguvu nyingi sana kutokana na mabadiliko ya
maana wamefupisha na kupata mazishi.(funeral).Pia katika lugha ya Kiswahili
kuna msamiati ambao umefupishwa na kupata maana maana mpya mfano;
Discontinue ;kwa mala ya kwanza
walitumia kama kutoendelea na masomo ya chuo kutokana na kushindwa ,lakini
kutokana na mabadiliko huita Kudisko.
Heiko Narrog (2012). Anadai kuwa mabadiliko
ya maana hushughulika kubadili misamiati ya lugha inayohusika,,mwanaisimu
huyu katika kitabu chake anasema kwamba suala la mabadiliko ya maana linahusu
kubadili misamiati ya lugha husika kwani kila lugha ina misamiati mahususi
ambapo inapofanyiwa mabadiliko misamiati hiyo hubadilika na kupata maana
zingine katika neno hilohilo kwa mfano;
Kifaru;misamiati
au maana zake ni,kifaa cha kivita, kipande cha mti ,mnyama.
Mawazo ya Heiko
Narrog (2012). Anadai kuwa mabadiliko ya
maana yana uhusiano mkubwa na maisha na utamaduni wa wanajamii,mwanaisimu huyu husisitiza kuwa ili mabadiliko ya
maana yaweze kutokea ni lazima uwepo uhusiano na maisha mila na tamaduni ya
lugha maalumu ambayo inatumika sehemu husika hivyo mabadiliko ya maana ya lugha
ya Kiswahili hutegemeana na maisha na mila na desturi za watu wanaozungumza
lugha hiyo na wanaotumia kingereza hutegemea maisha na mila na desturi za
waingereza.
Anadai kuwa
mabadiliko ya maana hujihusisha na kuazima maneno kutoka lugha nyingine, uazimaji wa misamiati kutoka lugha nyingine hii ni
njia mojawapo ya uundaji wa misamiati mipya katika lugha mbalimbali mwanaisimu
huyu anadai kuwa unaweza kuchukua maneno
na kuyaingiza katika watumiaji wapya kwa maana mpya ya neno hilo pasipo kuzuwiliwa
na kitu chochote , Heiko Narrog (2012).
Ametoa mfano kuwa kitenzi wasili (arrive) kutoka lugha ya kingereza
kimeazimwa kutoka lugha ya kifaransa hivyo hata lugha ya Kiswahili hufanya
mabadiliko ya maana kutoka lugha zingine mfano misamiati kama vile;
ikulu,kimori,ng”atuka na kitivo.
Hivyo basi
Heiko Narrog (2012).ametoa mchango mkubwa sana katika lugha ya Kiswahili na zingine kwa ujumla kwani
amefanikiwa kuonesha mabadiliko mbalimbali ya maana katika lugha ya kingereza
na amejaribu kuangalia kwa upana kidogo lugha za kifaransa ,kihindi,na kigiriki
hivyo kutokana na mawazo yake pia katika Kiswahili yametusaidia kwa mapana
zaidi.
Narrog, H.( 2012). Modality, Subjectivity, and Semantic Change. A Cross-Linguistic
Perspective
TUKI(2004),Kamusi
sanifu ya isimu na lugha. Chuo
Kikuu Dar es salaam
Comments
Post a Comment