Saruf
Saluhaya
(2010). Anasema dhana ya sarufi ni kanuni, sheria na taratibu zinazotawala
lugha katika matumizi yake ambayo hujumuisha matamshi, maumbo na maana
Masamba
(2004 ) Sarufi ni taaluma ya lugha inayohusu uchunguzi na
uchanganuzi wa kanuni za vipengele
mbalimbali vya lugha.
Masamba na wenzake ( 1999 ).Sarufi ni kanuni
na sheria au taratibu zinazo tawala kila moja katika viwango vine vya lugha
yaani;Fonolojia (umbo sauti ) umbo neon ambayo huitwa Mofolojia, Miundo maneno ( sintakisia ) na
Umbo maana ambayo ni Semantiki.
Sarufi ni taaluma ya lugha inayochunguza na
kuchanganua vipashio na kanuni mbalimbali zinazo tawala muundo wa lugha (Matinde 2012 ).
Sarufi inaweza kuelezwa kama kanuni,sheria na
taratibu zinazomwongoza mzungumzaji au mwandishi kuzungumza au kutunga tungo
sahihi zinazoeleweka kwa msikilizaji wa lugha ileile.
Kwaujumla sarufi inaweza kuelezwa kama kanuni,
sheria na taratibu zinazo muongoza mzungumzaji au mwandishi kuzungumza au
kuandika tungo au sentensi sahihi zinazoeleweka kwa msikilizaji wa lugha
husika.Kama ni mzawa wa lugha, mtumiaji huwa tayari anazo kanuni hizo ( hata
katika uzungumzaji), yaani kanuni anakuwa nazo akilini baada ya kusoma au
kuishi na watu wanaozungumza lugha hiyo.
Kwamujibu wa Masamba na wenzake (1999 )
wameeleza kuwa sarufi mapokeo ni sarufi elekezi ikisisitiza usahihi wa lugha ikionyesha sheria ambazo
hazina budi kufuatwa, mathalani kufanya muundo fulani wa sentensi usomeke kwa
usahihi au sheria ambazo hazina budi kufuatwa ili kufanya matamshi Fulani
yakubalike kuwa ndio sahihi.
Sarufi mapokeo inaainisha aina tatu za
sentensi kwa kuzingatia uamilifu wake ambao aina hizo ni , sentensi taarifa,
sentensi ulizi na sentensi agizi. Mfano, sentensi taarifa; Baba ameondoka leo
asubuhi, Sentensi ulizi; Nani amekula chakula changu?. Sentensi agizi;Lete hiyo
kalamu!. wakati sarufi ya kileo
inaainisha aina nne za sentensi kwa kuzingatia muundo au umbo la sentensi hiyo,
sentensi hizo ni sentensi sahili, mfano; James anacheka. sentensi ambatano, mfano, wanachuo wa mwaka
wa kwanza wanafagia viwanja huku wanachuo wa mwaka wa pili wanafyeka. sentensi
changamani, mfano; Aliporudi nyumbani alitukuta tumelala. na sentensi shurutia
mfano;Angekuja leo tungeondoka leo..
Wanasarufi mapokeo wanasema kuna aina saba za
maneno na wengine wanasema kuwa kuna aina kumi za maneno. Mfano; Habwe na
Karanja (2004 ) wao wanaainisha aina kumi za maneno ambazo ni nomino, vitenzi,
viwakilishi, vivumishi,vielezi, vihusishi, viunganishi, vionyeshi,vihisishi na
vibainishi.Wakati wanasarufi wa kileo/muundo wao wanaainisha aina saba kama
vile; nomino, viwakilishi, vihusishi, vitenzi, vielezi, viunganishi na
vihisishi.
Kwamujibu wa
Khamisi na Kiango ( 2002 ). Sarufi mapokeo ni sarufi ya kale, wataalamu
wanaohusishwa na mkabala huu walijitokeza kuanzia karne ya tano kabla ya Kristo
na katika karne ya 18 na 19 baada ya Kristo.Mfano; wataalamu hao ni Plato,
Aristotle Panin na Plotagoras, wakati sarufi ya kileo imekuja baada ya sarufi
mapokeo na wafuasi wa sarufi ya kileo na miongoni mwa wafuasi wa sarufi ya
kileo ni Noam Chomsky.
Utofauti
katika uchanganuzi wa sentensi. katika sarufi mapokeo sentensi huchanganuliwa
katika kiima na kiarifu pia hutumia istilaihi chagizo badalaya kirai
kielezi(KE), shamilisho badala ya kirai nomino(KN) na prediketa badala ya kirai
kitennzi (KT). wakati sarufi za kileo huchanganuliwa sentensi katika kundi
nomino na kundi kitenzi na pia hutumia istilahi za kawaida za virai. Mfano wa
uchambuzi wa sentensi kama ifuatavyo
Mwalimu
aliyefukuzwa jana shuleni amerudi kwao.
(a) Uchanganuzi wa kimuundo au kileo
S.Changamano
|
|||||||||
KN
|
KT
|
||||||||
N
|
βV
|
T
|
E
|
||||||
Mwalimu
|
|
Amerudi
|
Kwao
|
||||||
N
|
Ts
|
E1
|
E2
|
T
|
E
|
||||
(b) Uchanganuzi wa kimapokeo.
S.changamano
|
|||||
K
|
A
|
||||
N
|
βV
|
Pr
|
Ch
|
||
Mwalimu
|
aliyefukuzwa
|
Jana
|
shuleni
|
Amerudi
|
Kwao
|
N
|
Ts
|
E1
|
E2
|
T
|
E
|
Utofauti
katika lengo. katika sarufi mapokeo lengo lilikua ni kuelekeza watu jinsi ya
kutumia lugha pia zilisisitiza kanuni na nini cha kusema na wajua lugha wakati
katika sarufi za kileo lengo lao lilikuwa ni kufafanua vipengere vyote vya
lugha fulani kama vilivyo na wanafafanua jinsi watu wanavyozungumza lugha na
sio kuwaelekeza waizungumze vipi lugha yao.
Sarufi
mapokeo ilikua baguzi kwani ilijikita zaidi katika lugha za kiulaya kama vile
kiyunani na kilatini. Wakati sarufi za kileo/muundo zimejikita katika lugha
zote zinazotumiwa na mwanadamu kama vile kiswahil,kinyakyusa, na kimakonde.
Sarufi
mapokeo ilijikita zaidi katika taratibu na kanuni za uchanganuzi wa lugha kwa
kuzingatia hasa lugha ya maandishi na kutozingatia lugha ya mazungumzo. Hivyo
basi ni dhahili kwamba mkabala huu ulikua na mitazamo ya kifalsafa, kidi,
nafasihi Habwe na Karaja (2004). wakati sarufi za kileo/ sarufi muundo yenyewe
imejikita katika uchanganuzi wa lugha kwa kuzingatia kanuni na taratibu zinazo
husisha aina zote mbili za lugha yaani lugha ya mazungumzo na lugha ya
maandishi.
Hivyo
basi mbali na kuwepo kwa utofauti kadha wa kadha baina ya sarufi za kimapokeo
na za kileo pia hufanana katika nyanja mbalimbali kama vile mikabala hii miwili
yote imekua ikijihusisha na kanuni, sheria pamoja na taratibu za uchanganuzi na
uchambuzi wa lugha.
Habwe,
J. na Karanja, P. ( 2004 ). Misingi ya Sarufi ya
Kiswahili. Nairobi. Phonex Publisher.
Habwe,J.
na Karanja P. ( 2007 ). Misingi ya Sarufi ya Kiswahili. Nairobi. Phonex Publisher.
Masamba
na wenzake ( 1999 ) Sarufi Miundo ya
Kiswahili Sanifu .( SAMIKISA ):Sekondari na
Vyuo,Dar es Salaam.TUKI.
Matinde,R,S. (2012 ). Dafina ya Lugha,Isimu na Nadharia:Kwa
Sekondari,Vyuo vya Kati na
Vyuo Vikuu. Mwanza: Serengeti Publishers.
Saluhaya (2010 ). Nadharia
ya Lugha: Kidato cha Tano na Sita.Dar es Salaam. Children Education Society
( CHESO ).
.
Comments
Post a Comment