Fonimu
Fonimu Ni kipande kidogo kabsa katika mfumo wa sauti za lugha ambacho kina sifa pambanuzi na kuweza kukitofautisha na vipande vingine vya aina yake. ( Massamba, 2004).
Habwe na karanja, (2007). Wanasema kuwa fonimu Ni kipande sauti ambacho hutumika katika kujenga maneno ya lugha kwa mfano vitamkwa Kama /p/, /b/, /u/, /m/, /t/, /d/, /a/, /k/ na /n/. Tunaweza kujenga maneno Kama pumba, tunda, taka, muda, dunda, kama na kuta.
Hivyo kwa ujumla fonimu tunaweza kufasili Kama kipashio kidogo kabsa Cha kifonolojia ambacho huwa na uwezo wa kujenga neno mfano /k/, /a/, /a/, fonimu hizi zinajenga neno "kaa", /t/, /I/, na /a/ zinajenga neno "tia".
TUKI, (1990) wanasema fonolojia ni tawi la isimu ambalo hushughulikia uchambuzi was mfumo wa sauti zinazotumiwa katika lugha Fulani
Habwe na karanja (2004), wanasema fonolojia ni utanzu unaochunguza jinsi sauti za lugha zinavyopangwa na kuungana katika lugha mahsusi ili kuunda utungo wenye maana kimawasiliano.
Kwa ujumla tunasema fonolojia ni tawi la isimu ambalo hushughulika na kuchunguza sauti za lugha mbalimbali au sauti za lugha mahsusi ambazo huunda maneno yenye maana kimawasiliano.
Trubezkoy, katika kitabu chake Cha "Principles"(uk 36) anafasiri dhana ya fonimu Kama jumla ya sifa za sauti ziliO na umuhimu wa kifonolojia. Anasisitiza kuwa fonimu isitambuliwe kwa kuangalia sifa halisi za sauti yenyewe bali kwa kuangalia na kuzingatia zile sifa zake ambazo zina umuhimu wa kifonolojia. Trubezkoy ana madai yake kwamba dhana ya upambanuzi huchukulia pia kuwa Kuna na dhana ya ukinzani na kwamba sifa ya sauti inaweza tu kuwa pambanuzi kiuamilifu iwapo tu inakinzana na sifa nyingine.
Kwa mujibu wa Trubezkoy, ukinzani wa sauti unaoweza kuleta tofauti ya maana katika lugha ni ukinzani wa kigonolojia. Huu ni ukweli mwingine ambapo tunaona kwamba Trubezkoy anasisitiza ukweli wa kifonolojia wa fonimu. Tumeigawa kazi yetu katika sehemu tatu yaani utangulizi ambao umebeba maana ya istilahi mbili ambazo ni fonimu na fonolojia zilizojadiliwa na wataalamu mbalimbali. Sehemu ya pili ni kiini cha kazi ambacho kimebeba vigezo muhimu vinavyotetea hoja ya kwamba fonimu ni ukwel wakifolojia Kama tulivyojadili, pia sehemu ya mwisho Ni hitimisho.
Tunaichukulia fonimu Kama ukweli wa kifonolojia kwa kuangalia vigezo vinavyotufanya tuseme hivyo. Vifuatavyo ni vigezo vinavyotetea hoja hii ya kwamba fonimu ni ukweli wa kifonolojia.
Kwanza, Ni kwamba haileti maana yoyote kuzungumzia fonimu pasipo kuihusisha na mfumo wa lugha fulani wa lugha. Fonimu ni lazima zihusishwe na lugha maalumu. Kila lugha in fonimu au sauti zake ambazo hushughulikiwa na tawi la isimu ambalo ni fonolojia, sauti ya lugha moja inaweza kutofautiana na katika lugha nyingine sauti hizo huitwa fonimu, pia fonimu ni kipashio Cha kifonolojia ambacho huchunguza sauti za lugua mahsusi. Kwahyo ni kweli kwamba fonimu Ni ukweli wa kifonolojia Kwan hushughalikia sauti za lugha fulani.
Pili, sauti inayopewa hadhi ya fonimu katika lugha moja si lazima ipewe hadhi ya fonimu katika lugha nyingine. Kuna baadhi ya fonimu huwa na hadhi katika baadhi ya lugha na haina hadhi katika baadhi ya lugha. Mathalani fonimu /ph/ yaweza kuwa na hadhi katika baadhi ya lugha Kama vile kimtang'ata lakini isiwe na hadhi ya kifonimu katika lahaja nyingine za kiswahili.
Tatu, hata kama sauti fulani inaweza kujitokeza katika lugha zaidi ya moja kama fonimu, thamani yake inaweza isiwe sawa katika hizo lugha zote inamotokea. Tuchukulie mfano wa sauti /s/ ambayo hutokea katika kiswahili na katika ekikwaya. Wakati katika kiswahili fonimu /s/ inakinzana na fonimu /z/ . Katika ekikwaya hakina ukinzani wa aina hiyo si tu kwamba fonimu /s/ haikinzani na /z/ bali pia ni kwamba sauti /z/ haimo kabsa katika mfumo wa sauti wa lugha hiyo. Kwahiyo thamani ya /s/ katika kiswahili haiwezi kuwa sawa na thamani ya /z/ katika ekikwaya.
Hitimisho; Cha kusisitiza hapa ni kwamba ili watu waielewe fonimu ni lazma aitazame uamilifu wa fonimu hiyo katika fonolojia ya lugha hisika.
MAREJEREO.
Habwe, J & Karanja, P.(2007). Misingi Ya Sarufi Ya Kiswahili. Nairobi: Phoenix.
Habwe, J & Peter, K (2004). Misingi Ya Sarufi Ya Kiswahili. Nairobi: Phoenix.
Massamba na wenzake, (2004). Fonolojia Ya Kiswahili Sanifu. Dar es salaam: TUKI.
TUKI, (1990). Kamusi Sanifu Ya Isimu na Lugha. Chuo kikuu Cha Dar es salaam.
Comments
Post a Comment