Shaaban Robert
UTANGULIZI
Shaaban
Robert alikuwa mwandishi mashuhuri wa kazi za fasihi ambazo ni Ushairi na nathali. Alizaliwa tarehe 01-01-1909 huko vibambani
kusini mwa machui mkoani Tanga,Tanzania .Alifariki
tarehe 22-06-1962 na akazikwa mwachui.ni miongoni mwa watanzania waliokuza na kueneza lugha ya
Kiswahili kupitia kazi zao za kifasihi. Alipata elimu ya dini ya kiislamu hukohuko
mkoani Tanga mpaka alipohamia Dar es salaam wakati huo ikijulikana kama
Mzizima.Alijiunga na kisomo cha darasani kuanzia mwaka 1922-1926 na akafaulu
vizuri katika masomo yake na kupewa
shahada ya kuhitimu.
Kutokana
na juhudi zake aliweza kuwa mwanachama wa kamati ya lugha ya Afrika Mashariki,
bodi ya lugha Tanganyika, chama cha wanafasihi wa Afrika mashariki, pia
mwanachama wa mamlaka ya jiji la Tanga,.katika maisha yake pia aliwahi kufanya
kazi idara ya forodha Pangani, idara ya Wanyama ofisi ya Mkuu wa Jimbo Tanga na
ofisi ya kupima nchi.
Kazi
iliyompa jina ni kazi ya uandishi wa natharina ushairi,
Wamitila
(2003:43), anaeleza kuwa falsafa ya mwandishi ni mawazo au wazo alilonalo juu
ya kile anachokiamini kuwa kina msingi
unaotawala maisha. Tunapotaja falsafa tunarejelea juu ya mawazo aliyonayo juu ya maisha ambayo
yanajitokeza katika maandishi yake.
Sadipo
(1973), anaeleza kuwa mawazo,fikra na udadisi kuhusu dhana na kanuni zinazotusaidia kuongeza udhaifu kuhusu
maadili,dini,maisha ya kisiasa,sheria, saikolojia, historian na sayansi na
jamii.
Kwa
ujumla tunaweza kueleza kuwa, falsafa ni
mawazo ya busara yenye kutawaliwa na misingi mahususi juu ya asili na maana ya
ulimwengu na maisha ya mwanadamu. Ni msimamo wa msanii katika maisha juu ya
utatuzi wa matatizo katika jamii.
Kwa
kutumia diwani mbili ambazo ni Mapenzi bora na Pambo la Lugha zilizoandikwa na
Shaaban Robert. Falsafa ya mwandishi inajadiliwa kama ifuatavyo kwa kuanza na diwani ya mapenzi bora;
Mapenzi
bora ni utenzi ulioandikwa na Shaaban Robert mwaka 1958. Utenzi huu una beti
700 lengo lake ni kujadili jamii juu ya maana, sifa, faida na hasara za kukosa
mapenzi bora. Mwandishi wa kitabu hiki anasema kusudi ni kuandalia mahitaji ya
watu waliofikia fahamu ya kuwaza na kuhoji neno au kitu au tendo kwa akili
ingawa haitakuwa vibaya kikisomwa na watu wowote ambao hawajafikia upeo kama
huo wa kupenda kujiweka tayari kwa zamu yao pia kwa watu amabo wanadhani kwamba mapenzi si kitu cha maana wanaonywa
kuwa wanapata hasara kubwa kwa kupitwa na bila kujua uzuri wa fahari, heshima na utukufu ambao hustahili wao wenyewe.
Anawaandikia watu wanaodai kuwa mapenzi karaha kuzungumzwa anadai wanachekesha
si kidogo mwisho anasisitiza kuwa mapenzi ni jambo moja kati ya mambo yaliyo
muhimu katka wajibu wa mwanadamu. Falsafa ya Shaaban Robert katika diwani ya mapenzi bora;
Mwandishi
anaamini kuwa mapenzi bora yaani mapenzi ya kupendana wanajamii wote bila
kujali tofauti zetu za rangi, dini, kabila na tofauti nyingine pamoja na
kumpenda mwenyezi Mungu yataifanya dunia iwe mahali pazuri sana pakuishi na pia
mwenyezi Mungu atatupatia thwawabu,
Mfano,
Mwandishi
anasema katika ubeti wa 123
“Tupendane
na wenyewe
Tofauti tuondoe
Amani itushukie
Mapenzi tufanye ngazi”
Pia
katika ubeti wa 467 anasema,
“Mapenzi
pambo la moyo
Ni furaha kuwa nayo
Mapenzi hushinda cheo
Hata pato la ghawazi”
Hivyo
mapenzi ni kitu cha thamani kubwa na endapo tukiyapoteza tutaingiwa na gharama
kubwa sana kuyarudish.
Kwa
kutumia diwani nyingine ambayo ni pambo la lugha. Pambo la lugha ni miongoni
mwa diwani iliyoandikwa na nguli wa fasihi za Kiswahili Shaaban Robert (1946),
katika utangulizi wake anasema kuwa kitabu chaitwa Pambo la Lugha kwa vile
ambavyo mashairi yasimulivyo habari zake kwa maneno ya vina au mlingano wa
sauti ipendezayo masikio.
Diwani
hii ina mashairi 43 yanayozungumzia kuhusu maisha, lugha na siasa.Katika diwani
hii mwandishi anaamini kuhusu ukombozi wa mwanamke na kifo ni masula ambayo
hatuwezi kuyaepuka kwa kuwa kifo kwa mwanadamu hakiwezi kukwepeka na suala la
ukommbozi wa mwanamke ni suala muhimu katika jamii zetu. Falsafa ya Mwandishi
katika diwani ya Pambo la Lugha mwandishi anaamini Suala la Kifo na Ukombozi wa Mwanamke
Suala
la kifo, Mwandishi hakusita kujadili suala la kifo kwani ni sehemu anayopitia
kila mwanadamu katika maisha yake. Pia mwandishi hakusita kutumia ufundi wake
kuongelea suala kifo katika shairi lake la “mauti” anasema
“Ugonjwa
hutibika, mauti hayana dawa
Kizima huharibika, kuja na kupotea
Umbile likuweka, mauti yanaondoa
Hili hufanyika pote, katika dunia” Uk 3
Katika
shairi hili mwandishi anatilia mkazo kuwa kifo hakikwepeki mahali popote
duniani na kuona kuwa kila nafsi itaonja mauti.
Ukombozi
wa mwanamke, falsafa ya mwandishi juu ya ukombozi wa mwanamke imejitokeza sana
katika ushairi. Yeye anamuona mwanamke ni kiumbe dhalili anayehitaji kusaidiwa
kuthaminiwa na kuheshimiwa. Hali hiyo ya unyanyasaji wa mwanamke imekithili
sana katika jamii nyingi ulimenguni, katika pambo la lugha mwaandishi anamtetea
mwanamke anasema
“Mwanamke anahaja, ya usawa wa hali
Mke hazai kiloja, ila kwa mbegu dhalili”
HITIMISHO
Hivyo,
Mwandishi Shaaban Robert katika diwani yake ya Mapenzi bora, ameweza kuonesha
kuwa mapenzi ndio kila kitu katika maisha sababu kukiwa na mapenzi bora
hakutokuwa na wizi, usaliti, vita, uongozi mbaya, rushwa. Hivyo mapenzi ni kitu
muhimu katika maisha ya wanadamu. Pia katika diwani yake ya “pambo la lugha”
falsafa yake kuu ni ukombozi dhidi ya ya mwanamke ambayo ni kweli kuwa mwanamke
akikombolewa dunia nzima imekombolewa. Hivyo
ni muhimu kuachana na mila potofu za kumnyanyasa mwanamke.
MAREJEO
Gibbe,
AG (1974).Shaaban Robert Mshairi,dar
es S alaam, Taasisi ya uchunguzi
Wamitila
K.W (2003).kichocheo cha fasihi, simulizi
na andishi;Nairobi focus publication ltd
Samwel,
M na wenzake (2013).Ushairi wa Kiswahili,mwongozo kwa walimu wa Kiswahili na
diyani ya MEA, Dar es Salaam mevailli, publishers and method Samweli
Robert
S, (1958).Mapenzi bora,Dar es Salaam;Mkuki
na nyota publishers limited
Sadipo
(1973).Woman and Afrikan society,
france strabourg
Robert
S, (1966).pambo la lugha,Nairobi;Oxford
university press ,1966
Comments
Post a Comment