Bila kujali utata kati ya neon, kishazi, sentensi na kirai wanaisimu wa lugha ya Kiswahili wanaelekea kukubaliana kuwa muundo wa kirai kwa ujumla huwa na viambajengo viwili. Taja na kufafanua kwa mifano kutoka Kiswahili sanifu 4. Hoja kuwa sarufi ya lugha ya Kiswahili haiwezi kuruhusu wazungumzaji wake kutunga tungo kama vile mno mzuri mototo sana inatokana na sababu ipi inayobainika katika sarufi yake 5.Ni kwa namna gani kigezo cha kimofologia husibitisha kuwepo kwa kategolia za kileksika katika lugha ya Kiswahili. 7. Ni hoja gani katika ushahidi wa kimuundo hutumika kuthibitisha kuwa lugha ya kiwsahili ina kategoria za virai? .
3. Bila kujali utata
kati ya neon, kishazi, sentensi na kirai wanaisimu wa lugha ya Kiswahili wanaelekea kukubaliana kuwa muundo wa kirai
kwa ujumla huwa na viambajengo viwili.
Taja na kufafanua kwa mifano kutoka Kiswahili sanifu
4. Hoja kuwa sarufi ya
lugha ya Kiswahili haiwezi kuruhusu wazungumzaji wake kutunga tungo kama vile mno mzuri mototo sana
inatokana na sababu ipi inayobainika katika sarufi
yake
5.Ni kwa namna gani
kigezo cha kimofologia husibitisha kuwepo kwa kategolia za kileksika katika lugha ya Kiswahili.
7. Ni hoja gani katika
ushahidi wa kimuundo hutumika kuthibitisha kuwa lugha ya kiwsahili ina kategoria za virai?
.
1.a) Katika kielezo
KN na KT Ni viambajengo
Ni fundo mama vya fundo
S ambavyo vinawakilisha kirai Nomino na kirai kitenzi Katika mchanganuo wa
sentensi
B). Viambajengo
visotamati ni KN na KT
Mfano.mwanafunzi mgeni
anaandika
C).fundo S huitwa fundo
mzizi ambao hutawala KN na KT
D). viambajengo vilivyo
hatua moja chini au kulia mwa kiambajengo kingine vinaitwa kiima na
kiarifu, kiarifu huwa upande wa kulia
ndicho ambacho hukaliwa na kirai kitenzi.
2.Ushahidi wa
kifonolojia
Katika ushahidi huu
kigezo kinachotumiwa ni mkazo au shadda. Neno moja linakuwa katika kategoria
tofauti kutokana na uwekaji wa mkazo. Tutazame mifano ifuatayo:
1) Wanafunzi wote
wameadhibiwa barabara
2) wafanyakazi wamefanya Kaz za barabara
3) We need to imPORT
new technology
4) We need an IMport of
new technology .
Katika mifano hiyo hapo
juu, neno la mwisho katika sentensi 1 ni kielezi na katika sentensi 2 ni
nomino. Katika sentensi 3 neno la nne ni kitenzi na neno hilohilo katika
sentensi 4 ni nomino. Maneno ni yaleyale lakini yamekuwa katika kategoria
tofauti kutokana na uwekaji wa mkazo mahali tofauti. Hivyo Basi mkazo
unathibitisha kuwapo kwa kategoria za kileksika. Unathibitisha kuwa kuna
kategoria mbili za neno moja. Hapa tunaona kuwa kanuni fulani za kifonolojia
lazima zijue taarifa za kikategoria kabla ya kutumika.
5. Ushahidi wa
kimofolojia
Katika ushahidi wa
kimofolojia kinachoangaliwa ni
uambikatizi. Viambishi fulani vya kisarufi huweza kuambikwa kwenye maneno
yaliyo katika kategoria fulani tu na haviwezi kuambikwa kwenye maneno ya
kategoria tofauti.Kwa mfano,
O’Graddy (1996) anasema
katika lugha ya Kiingereza kiambishi cha wingi –s huambikwa kwenye maneno ya
kategoria ya nomino, kiambishi cha njeo iliyopita –ed na cha hali ya kuendelea
huambikwa kwenye vitenzi, na viambishi vya ukadirifu -er, -est huambikwa kwenye
vivumishi. Vivyo hivyo, katika lugha ya Kiswahili, viambishi vya idadi na ngeli
huambikwa katika nomino na vivumishi, viambishi vya njeo, kauli, na usababishi
huambikwa katika vitenzi n.k.
7.Ushaidi
wa kisintaksia ndio unaotumika kuthibitisha kwamba lugha ya kiswahili
inakategoria za virai.tunatazama kuwa
sintaksia yaani jinsi maneno yanavyotawanywa kwa kufuata luwadha fulan
kwa kigezo Cha kimofolojia au kisintaksia.
Kirai
Ni neno au fungus la maneno ambayo kwa pamoja hutoa taarifa fulani.kirai
huundwa kwa Aina kuu za maneno.
Mf.kirai
nomino-mfano: baba na mama
Kirai kivumishi-mfano:kikombe kizuri sana
Kirai
kitenzi-mfano:anapika chakula
Kirai
kielezi-mfano:kesho asubuhikirai kihusishi-kwa gari
Kirai
kiunganishi-mfano:walakini,isipokuwa
MAREJEO
Habwe,
J na P. Karanja (2007). Misingi ya Sarufi ya Kiswahili. Nairobi: Phoenix
Publishers Ltd.
Massamba,
D.P.B na wenzake (1999). Sarufi Miundo ya Kiswahili Sanifu: Sekondari na
Vyuo. Dar essalaam: TUKI.
Massamba
na wenzake (2009). Sarufi Miundo ya Kiswahili Sanifu: Sekondari na
vyuo.Dar essalaam: TUKI.
Matinde,
S. (2012). Dafina ya Lugha, Isimu na Nadharia: Sekondari na vyuo vya kati na
Vikuu. Serengeti Educational Publishers.
Kihore Y, na wenzake (2012). Safufi Maumbo ya
Kiswahili Sanifu. Chuo kikuu cha Dar es salaam.
Comments
Post a Comment