KAZI: Kutunga shairi lenye kichwa kiitwacho “Tatizo la ajira” lenye beti 20 zenye kipande kimoja katika bahari yoyote ile, kwa kuzingatia urari wa vina na mizani na kuonyesha madhara ya tatizo la ajira katika;

 

KAZI: Kutunga shairi lenye kichwa kiitwacho “Tatizo la ajira” lenye beti 20 zenye kipande kimoja katika bahari yoyote ile, kwa kuzingatia urari wa vina na mizani na kuonyesha madhara ya tatizo la ajira katika;

a)Ugaidi

b)Wizi

c) Umalaya

TATIZO  LA  AJIRA

  1. Jinamizi meingia,

Latikisa na dunia,

Vijana walilia,

Ajira meenda wapi.

 

  1. Jamii yajiuliza,

Kwa mliyotueleza,

Watu mkatuagiza,

Ajira meenda wapi.

 

  1. Ajira tukililia,

Wote twaikimbilia,

Maisha twavumilia,

Ajira meenda wapi.

 

  1. Nilisoma kwa bidii,

Nikose kazi vipii

Walimu niliwatii,

Ajira meenda wapi.

 

  1. Juhudi tuliziweka,

Kusoma bila kuchoka,

Mazuri tukiyataka,

Ajira meenda wapi.

  1. Saluti wahadhirii,

Nikapata digrii,

Vyeti vyangu vizurii,

Ajira meenda wapi.

 

  1. Nasi tukajisomea,

Ajira kutegemea,

Sasa mnatugomea,

Ajira meenda wapi.

 

  1. Vijana walalamika,

Hasa wanapokumbuka,

Kipindi wakihenyeka,

Ajira meenda wapi.

 

  1. Kwa wao kujiari,

Maovu yanakithiri,

Tena yasiyo nasiri,

Ajira meenda wapi.

 

  1. Ubongo unachemka,

Fikiri tulikotoka,

Vitabu vilisomeka,

Ajira meenda wapi.

 

  1. Kina dada na wakaka,

Sasa mchaka mchaka,

Ajira kuadimika,

Ajira meenda wapi.

 

  1. Wasomi shuka thamani,

Wadada uchochoroni,

Saka pesa kwa uhuni,

Ajira meenda wapi.

 

  1. Kijana yu mtaani,

Mitaani makonani,

Viroba kukabeni,

Ajira meenda wapi.

 

  1. Wizi Kama jeuri,

Imekuwa desturi,

Kwao ndo wataajiri,

Ajira meenda wapi.

 

  1. Wajua tatizo nini,

Ajira kuwa gizani,

Jiuliza akilini,

Ajira meenda wapi.

 

  1. Tanzania ya viwanda,

Wasomi kuranda randa,

Wengi wavuka Uganda,

Ajira meenda wapi.

 

  1. Lilikuwa kimbilio,

Kwa wasomi pata vyeo,

Sasa imekuwa sio,

Ajira meenda wapi.

 

  1. Za kunja Kama folio,

Kuwaza ajira leo,

Ajira si tazamio,

Ajira meenda wapi.

 

  1. Nimeuza yangu mbuzi,

Nyumbani sina makazi,

Natembea bila kazi,

Ajira meenda wapi.

 

  1. Ajira mboni ajiyo,

Ni nyenzo ukiwa nayo,

Popote ukiwa nayo,

Ajira meenda wapi.

                        

Comments

Popular posts from this blog

International Law

KATIBA YA KIKUNDI