KAZI YA KISWAHILI SINTAKSIA

 

KAZI YA KISWAHILI SINTAKSIA

kazi yetu imegawanyika katika sehemu kuu tatu  zifuatazo; sehemu ya utangulizi ambavyo inahusu maana ya urejeo, maana ya viambajengo na maana ya tungo. Sehemu ya pili ni kiini cha kazi yetu ambavyo inahusu namna ambavyo viambajengo vya lugha vinavyorejeleana ili kukamilisha tungo ya kiswahili.. Sehemu ya tatu ni hitimisho La kazi yetu.

Kwa mujibu wa kamusi ya kiswahili (2013), inaeleza kwamba neno Urejeo limetokana na neno rejea lenye maana nenda tena mahali ulikotoka.

Kwa mujibu wa Habwe na Karanja(2012), wanaeleza kwamba viambajengo ni maneno madogo madogo au vipashio vidogo vidogo ambayo  au  ambavyo huungana na kujenga kipashio kikubwa zaidi ambacho ni tungo.

Kwa mujibu wa Massamba na Wenzake (2012) ,wanaeleza kwamba Tungo ni nomino ambavyo hutokana na kitenzi tungo ambacho kina maana ya kushikanisha vitu pamoja kwa kupitisha kitu kama Uzi ndani mwake.  Kwa Mujibu wa Sintaksia Massamba na Wenzake wanaeleza kwamba Tungo ni kuweka pamoja au kupanga pamoja vipashio ili kujenga kipashio kikubwa zaidi.

Katika sehemu hii ya pili tunaangalia jinsi au namna viambajengo katika Tungo vinavyorejeleana kati ya kiambajengo kimoja na kingine  au kiambajengo kimoja kinavyosaidia kujenga viambajengo kinachofuatia. Viambajengo tunavyoviangazia katika kazi yetu ni Neno, virai, Vishazi na Sentensi, viambajengo hivyo katika kujenga tungo huwa vinarejeleana au kutegemeana kama ifuatavyo;

Tungo neno, katika kufasili neno au kutoa maana ya neno kimekuwa ni tata kwa wataalamu wengi kwa hiyo kwa mantiki hii tunaanza kuangalia namna gani neno linaundwa katika Lugha ya kiswahili,

Kwa Mujibu wa Massamba na Wenzake (2012), wanaeleza kwamba vijenzi vinavyohusika katika kiwango cha tungo neno ni vitamkwa , silabi na silabi hujenga mofimu. Mofimu moja au zaidi hujenga tungo neno. Ili kupata tungo neno katika lugha ya kiswahili taratibu mbili za muhimu hazina budi kufuatwa . utaratibu wa kwanza ni mpangilio wa vitamkwa ili kupata silabiambazo kutegemea mazingira zinamotoka huweza kuwa mofimu. Utaratibu wa pili ni mpangilio wa mofimu hizo ili kupata tungo neno.

Vitamkwa ni vipande sauti vinavyoundwa na ala za kutamkia sauti kwa mujibu wa taratibu za matamshi ya lugha husika kama vile /t/, /d/, /m/, /a/, /b/, /e/, /I/, silabi da, ma, ba, ta, kwa mujibu wa Massamba na Wenzake (2002) wanasema mofimu ni kipashio kidogo kabisa chenye uamilifu wa maana katika maumbo ya maneno. Viambishi kwa hakika ni mofimu ambazo huambatana na mzizi katika muktadha mbalimbali ili kuunda tungo neno.

Kwa mfano.

A-na-chez-a                              Anacheza

Kwa mujibu wa Masamba na wenzie (2012),wanasemaaina hii ya tungo kirai uhusisha maneno mawili au zaidi ambayo huwekwa pamoja katika mpangilio maalumu unaozingatia uhusiano uliopo baina ya neno kuu na maneno mengine.

Mfano:mwalimu hodari .Hapa neno kuu ni mwalimu  ambalo ni nomino hivyo   mwalimu ni kirai nomino.

Katika tungo kirai tunaona urejeleo umejidhihirisha  kwenye neno hodari ambalo ni kivumishi  kimerejelea nomino mwalimuno kirai nomino

Hivyo tungo kirai kinarejelea tungo neno ili kuweza kukamilisha muundo wake

Kwa mujibu wa Massamba na wenzie  (2012),wanasema aina hii ya tungo kishazi ni matokeo ya kuweka miundo miwili au zaidi yenye kirai nomino na  kirai kitenzi ndani ya tungo au sentensi kwahiyo  tungo kishazi  kinarejelea  tungo kirai ili kukamilisha muundo wake.

Kwa mfano Bibi/ aliyekuja ameondo.

aliyekuja ni kishazi tegemezi  kinachorejelea kirai nomino Bibi hivyo tunaona tungo kishazi ili kukamilisha muundo wake no lazima kurejelea tungo kirai na tungo neno

Kwa mujibu wa Massamba na Wenzake (2012), wanasema Sentensi ni kipashio kikubwa chenye maana kamili. Muundo wa sentensi huhusisha vipashio vingine vidogo vidogo kimuundo ambavyo ni neno, virai, vishazi.Hivyo  muundo wa sentensi ili ukamilike  no lazima kurejelea tungo neno ,tungo kirai, na tungo kishazi

Kwa mfano.

Mwanafunzi/aliyechelewa ameadhibiwa.

 

 

             KN               kish Tg           KT

Hapa tunaona kishazi tegemezi  ni aliyechelewa kimerejelea kirai nomino  ambachoni mwanafunzi  na mwanafunzi ni neno.

HITIMISHO.

Kwa ujumla kuna urejeo katika kiambajengo kimoja na  kingine ili kuweza kukamilisha maana katika tungo kama ilivyoonekana  hapa juu.

 

 

 

Comments

Popular posts from this blog

International Law

KATIBA YA KIKUNDI