.Neno Kileksika.
2.Neno
Kileksika.
Neno ni
kipashio kidogo cha Lugha chenye maana. Kwa maana hiyo neno lazima liwe na sifa
ya maana inayoeleweka kwa jamii inayotumia lugha hiyo.(Mdee,1977).
Mfano:Baba-Mzazi
wa kiume.
Kifaranga-Mtoto wa kuku.
Mama-Mzazi
wa kike.
Ndama-Mtoto
wa ngo'mbe.
Sifa hii
inamashiko kwa sababu maneno mengi katika Lugha yana sifa ya kueleweka kwa
watumiaji wake wa Lugha husika.
3.Kirai
ni aina ya tungo ambayo inakuwa haina muundo wa kiima na kiarifu. Virai huundwa
na viamba jengo.
Viambajengo
ni kikundi cha maneno au hata neno moja pia inayofanya kazi kama kitu
kimoja.kirai,kishazi au sentensi mkusanyiko wa viambajengo kadha.
Kirai ni
mkusanyiko wa viambajengo kuzunguka neno kuu kwa mfano, KN huundwa na nomino na
vivumishi vyake, kwahiyo muundo wa kirai ni maneno yanayokiunda yakiwakilishwa
na alama za kategoria za maneno hayo.
a)Baba
mdogo
Hiki ni
kirai nomino( KN) kilichoundwa na nomino na kivumishi kwa hiyo KN=N +V.
b)anacheza
mpira.
Hiki ni
kirai kitenzi (KT)chenye kuundwa na Kitenzi (T)na kirai nomino.
4.Sintaksia
ni kategoria mojawapo ya sarufi ambao huchunguza muundo na mpangilio
unaokubalika wa vipashio katika kuijenga Lugha. Sintaksia hujihusisha na tungo
neno,tungo kirai,tungo kishazi na tungo sentensi.
Ni
kweeli kwamba wazungumzaji wa kiswahili hawawezi kukubaliana na tungo
hii"Mno mzuri mtoto sana" Hii ni kutokana kwamba tungo hiyo haina
kwanza mpangilio mzuri wa viambajengo vilivyotumika kuinda sentensi hiyo pia ni
kutokana na ukweli kwamba sentesi nyingi za kiswahili huanza na nomino katika
kiima tatu imetumia neno "mno" na "sana" yote yanadokeza
dhana moja.
6.Sintaksia
ni aina ya sarufi ambayo hujishughulisha na muundo wa vipashio jinsi ambayo
vinaijenga Lugha.
Kilekiska
hujishughulisha na maana ya maneno katika Lugha. Ufuatao ni udhaifu wa
kisintaksia katika kuwepo kwa kategoria ya Kilekiska.
Katika
ngeli ya kwanza umoja ina viambishi viwili(Yu/A)
Bado
kuna ngeli za nomino zinazojirudia mfano ngeli ya 2,6 na 7 umoja zinatumia "U"
Bado
kuna nomino zenye kuleta migogoro katika ngeli mfano Makala,Jambazi,Marashi.
7.Ushahidi
huu wa kisintaksia unaonyesha mtawanyo wa virai. Hii inamaana kwamba ukitaka
kuhamisha maneno yaundayo virai,hauna budi kuhamisha kirai kizima na si sehemu
tu kirai hichp,kudondosha au kuunganisha kirai kizima.
Mfano:Kaka
yako mkubwa simpendi.
Simpendi
kaka yako mkorofi.
Mkubwa
simpendi kaka yako.
Mkorofi
kaka yako simpendi.
Kuunganisha
virai venye hadhi sawa.Mfano a)Baba analima
Mama
analima.
Baba na
mama analima.
a)Malambugi
anasoma.
Kiti
kimevunjika.
Malambugi
na kiti kimevunjik/anasoma
Tungo
hiyo haijaleta mana kwasababu hadhi siyo sawa pia katika ushahidi wa
kisintaksia kuna jaribio LA ubadala kulingana na wanaisimu kama Andrew(2007).
Jaribio
LA kiubadala hujihidhirisha pale baadhi ya maneno kuweza kusimama badala ya
kirai kizima au kundi la maneno hususani katika kirai nomino na kirai kitenzi.
Kwa hiyo sikweli kwamba hakuna kategoria ya virai katika uchanganuzi wa
kisintaksia. Kuna kategoria ya virai ambayo imejikita katika neno kuu ambalo
kuna aina mbalimbali za virai ambavyo ni kirai nomino,kirai kitenzi,kirai
kielezi na kirai kihusishi.
Marejeleo.
Besha,R.M(2007).Utangulizi
wa Lugha na Isimu.Dar es salaam:MacMillan Aidan Ltd.
Habwe,J&Karanja,P.(2007).Misingi
ya Sarufi ya Kiswahili.Nairobi:Phoenix publishers.
Massamba,D.P.B
na Wenzake .(2013).Fonolojia ya Kiswahili Sanifu.Dar as Salaam:TUKI.
Mdee,D.(2007).Nadharia
za Leksikografia.Dar es Salaam: TUKI.
Matinde
,R.S.(2012).Dafina ya Lugha Isimu na Nadharia:Kwa Sekondari,Vyuo vya kati na
vyuo vikuu.Mwanza:Serengeti Educational Publishers(T)Ltd.
Comments
Post a Comment