Riwaya ya kiswahili
UTANGULIZI
Riwaya ya kiswahili ni ile ambayo inafungamana na
utamaduni wa jamii ya kiswahili maana watunzi wengi wamekuwa wakiandaa kazi zao
wakirejea utamaduni na Mila wanazozifuata au kuziamini (wamitila,2003).
Kanar,(2001) amesema kuwa usimulizi ni mtindo wa
mpangilio unaotumiwa na waandisui wa hotuba,habari na utunzi wa kibunilizi
kueleleza matukio.Anaendelea kufafanua kuwa unahusisha hadithi inayosimuliwa na
msimulizi kulingana na mtaalamu huyu Kuna kaidu muhimu ambazo sharti msimuliaji
azitilie maanani wakati wa kutoa masimulizi yake Kwan kuwa hadhira yake
huzitarajia na huwa wanazisaka wanaposoma au kusikiliza kiss nazo ni kina Nani
wanaohusika ni Nini kinatokea ni oini yanatokea na kwanini yanatokea.
Msimulizi ni wakala au nyenzo inayotumiwa na mtunzi
kusimulia hadithi.kwahiyo Kila Hadithi in msimulizi ambaye anaweza kuwa mtunzi
au mtu mwingine ambaye ameteua awe msimulizi.Hadithi inamfikia msomaji kupitia
kwa msimulizi.msimulizihumpitisha msomaji au mskilizaji katika masafa
,maeneo,nyakati,na katika mawasiliano ya wahusika,hali na saikolojia zao.kwahyo
msimulizi kupitia usimuliaji anajenga mkabala ambao unamwezesha msomaji au
mtazamaji kuyatazama yanayotendeka na kuyasikia yanayosimuliwa(Msokile,1993).
Mtunzi wa Hadithi,ni mtu yeyote anayejishughulisha
na utunzi au uandishi wa kazi za Hadithi mfano hekaya,Ngano,Tarihi,soga,Visa
sili na nyinginezo.
Tunajibu swali let Kwa kutumia vitabu vya riwaya ya
kiswahili ambazo ni MZIMU WA WATU WA KALE kilichoandikwa na
M.S.Abdullah,KUSADIKIKA kilichoandikwa na Shabaan Robert na NGOMA YA MIANZI
kilichoandikwa na mulokozi M.M. Hoja ya kwanza tumeanza na kitabu au riwaya ya
"ngoma ya mianzi",hoja ya pili tumetumia"mzimu wa watu wa
kale"na hoja ya mwisho tumetumia"kusadikika"kutetea hoja hii.
Ni kweli kwamba katika riwaya ya kiswahili
anayedhaniwa kuwa ni msimulizi na msimulizi mwenyewe mara nyingi huchanganywa
na mtunzi wa Hadithi kwa sababu zifuatazo.
Katika kujibu swali hili tunajikita katika kuangalia
aina za usimuliaji wa riwaya ya kiswahili.
Mwandishi hujifanya ndiye msimulizi/msimuliaji,
usimulizi huu hujikita au hutumia nafsi ya tatu pale mwandishi hutumia mtindo
was insha kufafanua Jambo kwa jinsi atakavyo yeye na kuweka au kutumia ubunifu
kujitenga na Hadithi mfano katika riwaya ya"Ngoma ya mianzi"katika
riwaya hii mwandishi amejifanya kuwa ndiye msimulizi kwani hueleza wazo la
mhusika mkuu Kama vile yeye ni muhusika.katika riwaya hii ya Ngoma ya mianzi
mwandishi ndiye msimulizi/msimuliaji mfano katika (uk 1-3) mwandishi anasimulia
jinsi muhusika chulu anaota ndoto ambayo ni ya hatari,anafanikiwa kukimbia
yeye,mbuni na Bibi yake ili kujihami na hatari hiyo.kwahyo usimulizi huu
mwandishi ndiye huchukua uhusika katika matukio yote kwa kutumia nafsi ya
tatu.kwahiyo ni kweli msimulizi na msimulizi mwenyewe huchanganywa na mtunzi wa
Hadithi.
Mmoja wa wahusika kuwa ndiye msimulizi, usimulizi
huu huusisha nafsi ya tatu ambapo muhusika mkuu husimulia matukio yote katika
Hadithi pia tunamjua wahusika wengine kupitia yeye.katika riwaya ya "
mzimu wa watu wa kale"mhusika mkuu ambaye ni bwana Musa amekuwa msimulizi
katika riwaya hii pia kupitia yeye tunapata kumjua mhusika Najum mfano (uk 13)
bwana Musa anasema kumwambia Najum kuwa "bwana musa akaendelea kusema na
tuseme anapanda mwilini na rohoni kwa wakati mmoja lakini kama mlivyosema
binadamu ni kiwiliwili na roho pamoja.mimi naona kwahiyo shetani ni yeye
mwenyewe binadamu, lakini wakati anapachagawa labda huwa amerukwa na roho hujua
analosema wala analofanya. Hapa Najum alipata kipengee kidogo". Kwahiyo
tunaona hapa bwana Musa ambaye ni muhusika mkuu huwa ni msimulizi ambaye
anasimulia kiss hiki najum. Kwahiyo msimulizi na msimulizi mwenyewe
huchanganywa na mtunzi wa hadithi.
Mwandishi na msimulizi wanakua kitu kimoja. Katika
hoja hii mwandishi na msimulizi huwa kitu kimoja kwani mwandishi anakuwa karibu
na msomaji lakini pia msomaji anakuwa karibu na mwandishi pia mwandishi au
msimulizi anakuwa na uwezo wa kujipa jina lolote katika riwaya au hadithi
ambayo huwa na sifa ya kitawasifu. Usimulizi huu hutumia nafsi ya Kwanza ambapo
mwandishi au msimulizi hujisimulia yeye binafsi. Mfano katika riwaya ya
"kusadikika" ya shabaan Robert. Mhusika karama ndiye ana sifa hii ya
kitawasifu kwani anajisimulia yeye kama yeye.mfano wa ushahidi huu tunaupata
katika (uk 11) ambapo karama anajaribu kujitetea mahakamani baada ya kufungwa
na mfalme majivuno kwa kosa la kusambaza sheria kwa wananchi ili watambue haki
zao. Mfano katika kitabu karama anasema "Ninazo sababu ya kusema.sababu ya
Kwanza iliyotia azima katika moyo wangu ya kuanzisha uanasheria katika nchi hi
labda itaelezeka vema Sana kama nikitaja mkasa wa wajumbe wa kaskazini
................................". Hi ni sifa ya kitawasifu ambayo
hujaribu kuelezea maisha ya mtu binafsi kwa kutumia nafsi ya Kwanza.
Hitimisho,aina hizi za usimulizi Zina changamoto
zake katika hadithi au riwaya.mfano msimulizi na mwandishi kuwa kitu kimoja,
changamoto yake ni kuwa mwandishi au msimulizi husimulia Yale yaliyo mazuri tu
kwa sababu yumo ndani ya .mmoja wa wahusika kuwa ndiye msimulizi wa hoja hii ni
changamoto kwani msimuliaji lazima awe na ramani vinginevyo atapotea.
REFERENCES
Abdullah, M.S. (1971). Mzimu Wa watu Wa Kale. Dae es
salaam: East African Liteture Bureau.
Msokile, M.
(1993). Kunga Za Fasihi na Lugha. Indian University: Educational
Publishers and Distributors, Limited.
Mulokozi, M.M (2003). Ngoma Ya Mianzi. Dar es
salaam: Tanzania Publishing House.
Shaaban, R. ( 1991). Kusadikika. Dar es salaam:
Mkuki na Nyota Publisher.
Wamitila, K.(2003). Kamusi ya Fasihi. Nairobi,
Kenya: focus Publication.
B
STE/BAED/164098 |
|
|
ALEX LEONARD |
STE/BAED/164400 |
|
BARAKA G MALAMBUGI |
STE/BAED/164158 |
|
GHANIMA S. PONGWA |
STE/BAED/164192 |
|
HAPPYNESS CHARLES |
STE/BAED/164005 |
|
LILIAN F. NGOWI |
STE/BAED/164652 |
|
LUCY B MKONDYA |
STE/BAED/164081 |
|
MICHEAL JOSEPH |
STE/BAED/16437 |
|
NOELY G. NGONYANI |
STE/BAED/164243 |
|
|
|
|
|
|
|
CHUO KIKUU KISHIRIKISHI CHA STELLA
MARIS MTWARA
(Chuo Kishirikishi cha
Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino-Tanzania)
IDARA:
KISWAHILI
KITIVO:
ELIMU NA SAYANSI
KOZI:
USHAIRI WA KISWAHILI
MSIMBO WA KOZI: SW 312
AINA YA KAZI: KAZI YA KUNDI
NAMBA YA KUNDI NAMBA 17
JINA LA MHADHIRI: MWL, CHITIMBE
Na |
MAJINA |
NAMBA ZA USAJILI |
SAHIHI |
1. |
s |
|
|
2. |
|
||
3. |
|
||
4. |
|
||
5. |
|
||
6. |
|
||
7. |
|
||
8. |
|
||
9. |
|
||
10. |
|
Swali:
Tunga
shairi kutoka bahari yoyote ile lenye kichwa cha habari “KUMBE NI UZANDIKI”
lenye beti 20 na kipande kimoja kwa kuzingatia urari wa vina na mizani.
Comments
Post a Comment