Riwaya
Wamitila (2002) na
Senkoro (2011), wanasema Riwaya ni kisa mchangamano ambacho uweza kuchambuliwa,
kwa mapana na marefu kifani na maudhui.Madumla (2009) Riwaya ni masimulizi
marefu ya kubuni yalio katika mtindo wa kubuni ya kisawili mtindo maalumu na madhumuni
maalumu.kwa ujumla ni masimulizi ya kubuni ya kinathari yenye msuko au
mpangilio wa matukio au ploti unaofungamana na wakati au kisawili wakati na
yenye visa vingi vinavyotendeka katika Riwaya fulani na yenye mawanda yenye
mchangamano wa dhamira, visa na wahusika.Riwaya ya kiswahili ni ile
inayofungamana na utamaduni wa waswahili katika lugha ya kiswahili ambayo
inapatikana katika nchi ya Afrika Mashariki pia ni Riwaya inaowahusu waswahili
wenyewe.Kusadikika ni Riwaya iliyoandikwa na mwandishi Shaaban Robertna
kuchapishwa Mkuki wa nyota mwaka 1991.Ngoma ya mianzi imeandikwa na mwandishi
M.m.Mulikozi na kuchapishwa na Tanzania pub.House in Dare s salaam mwaka 1991
Mzimu wa watu kale hii ni Riwaya iliyoandikwa na Muhammed Said Abdullah na
kuchapishwa na East Africa literature Bureau Nairobi Dare s salaam Kampala
mwaka 1960.
Kwa
kuzingatia swali linalosema "katika Riwaya ya kiswahili anayedhaniwa kuwa
ni msimulizi na msimulizi mwenyewe mara nyingi huchanganywa na
mtunzi".yafuatayo no maelezo yanayodhibitisha dai hili kwa kutumia vitabu
mbalimbali Kama vile Kusadikika, Mzimu wa watu wa kale na Ngoma ya mianzi.
Nikianza na Kusadikika naeleza kama ifuatavyo
Kwa kutumia Riwaya ya Kusadikika nikweli kwamba
mwandishi ndio msimulizi wa Riwaya kuanzia ukurasa wa (1)mpaka ukurasa wa (10)
mfano pale aliposema "wazili wa Kusadikika alikua mtu mwenye haiba kubwa
na uhodari mwingi.uwaziri wake ulianza zaman sana .alikua waziri wa wafalme
watatu katika nyakati mbalimbali"hivyo kupitia hayo maelezo inaonesha
dhairi kuwa mwandishi ndio msimulizi lakini pia kupitia hii Riwaya mwandishi
anoenekana kupotea na mhusika anakua ndio msimulizi wa Riwaya kwa mfano kuanzia
(uk)11hadi wa 49 tunamuona mhusika Karama ndiye anakuwa msimulizi rejea pale
anaposema ninazo sababu sita za kusema.ya kwanza iliyotia azima katika moyo
wangu wa kuanzisha uanasheria katika nchi hii labda itaelezeka vema sana Kama
nikitaja mkasa wa mjumbe wa kaskazini". Kupitia hayo malejeo na dhairi
kuwa Karama ndie alikua ndio msimulizi wa Riwaya na usimulizi wake ulikoma
baadae baada ya kutaka kutoa hukumu ndio mtunzi alionekana tena anasimulia kwa
kumuonesha mfalme anatoa hukumu kwa kusema kuwa Karama atakua huru
kwanibameshinda kesi.
Ni kweli kwamba msimulizi wa hadithi amechanganywa
na mtunzi mfano katika Riwaya ya mzimu wa watu kale msimulizi wa hadithi
amechanganywa na mtunzi pale nafsi ya kwanza na nafsi ya tatu katika usimulizi
wake hii unadhihirisha pale kipwerere alipandwa na shetani na kueleza kwa lugha
isiyofahamika na bwana musa.hivyo bwana Musa alisema tofauti yetu hasa labda ni
hii kwamba wewe unadhani kwamba wanavyodhani watu wengine kwamba mtu akichagawa
hujiwa na shetani au uoandwa na pepo alietoka bahari ya sabaau aridhi ya Saba
yaani yule binadamu kwa wakati hule huwa kama kiti chake.vyema lakini kiti Cha
shetanini binadamu na pia binadamu ana sehemu mbili kiwiliwili na roho. Sasa
mtu akichagawa shetani hukaa wapi hasa mwili au rohoni mwake anaulizwa na
najumu.najumu aliduwaa hakuwa na kusema. bwana Musa akaendelea kusema
"natuseme anampanda mwilini na rohoni kwa wakati mmoja. lakini Kama
nilivyosema binadamu ni kiwiliwili na roho pamoja.mimi aona kwa hiyo shetani ni
yeye meenyewe binadamu labda wakati anapochanganywa labda huwa amerukwa roho
hujua analosema Wala analofanya.hapa najumu alipata kipengele kidogo akaruka na
kusema yaani yule Bibi alikua anasema maneno ovyo tu siyo? Bwana Musa alijibu
Aaa! nimesema ameruka roho na roho ikiruka Najum hufika mbali hivyo kwa
majibizano hayo kati ya bwana Musa na Najum hudhihirisha kuwa kuwa bwana Musa ni
msimuliaji lakini muda mwingine huwa muhusika wa hadithi lakini pia mtunzi wa
hadithi yenyewe kwa sababu Kuna muda anasimulia matukio kwa kutumia nafsi ya
kwanza na muda mwingine anasimulia kwa nafsi ya pili.
Matumizi ya nafsi ya kwanza . Mwandishi ameonesha
matumizi. ya kwanza katika kitabu cha ngoma ya mianzi ambapo mtunzi na msimulizi wanaposema
tulienda tukajificha tulipowaona hiii inadhihirisha uwepo wa nafsi ya kwanza
pia katika Riwaya hii tunamuona mtunzi amesimulia yeye peke mwanzo adi mwisho
wa riwaya.
Hivyo basi ni dhairi kwamba katika Riwaya ya
kiswahili anayedhaniwa ni msimulizi na mwandishi wanachanganywa Kama
ilivyoelezwa katika maelezo hapo juu na sio mara zote kwamba msimulizi na
mtunzi wanachanganywa bali Kuna vitabu au riwaya msimulizi na mtunzi
huchanganywa.
Comments
Post a Comment