Tunga shairi kutoka bahari yoyote ile lenye kichwa cha habari “KUMBE NI UZANDIKI” lenye beti 20 na kipande kimoja kwa kuzingatia urari wa vina na mizani.

 

Tunga shairi kutoka bahari yoyote ile lenye kichwa cha habari “KUMBE NI UZANDIKI” lenye beti 20 na kipande kimoja kwa kuzingatia urari wa vina na mizani.

Katika mjadala wetu tumejikita katika utungaji wa ushairi bahari ya Utenzi unaoelezea mada kuu ambayo ni 'UNYANYASAJI', unaotendeka katika nyanja mbalimbali, kama vile katika elimu, afya, ofisi za umma, kwenye familia, na katika jamii kwa ujumla.

            UNYANYASAJI

1.       Janga we umeingia,

          Ndani na nje pia,

          Wala hupati tulia,

          Unyanyasaji twajionea.

2.        Unyanyasaji ni pigo,

           Huvuruga na mipango,

           Ndoa na yetu malengo,

           Unyanyasaji twajionea.

 

3.       Mayaya wa ndani kwetu,

          Hawana mambo ya utu,

          Mtoto mpa  upupu,

          Unyanyasaji twajionea.

 

4.      Usawa meutawanya,

        Unyanyasaji wapenya,

        Tanzania hata kenya,

       Unyanyasaji twajionea.

5.        Ofisini ukifika,

           Vitu vingi kavishika,

           Utaingiwa nashaka,

           Unyanyasaji twajionea.

 

6.        Polepole akuanzie,

           Mpaka  ajisikie,

           Je unamiadi nae,

           Unyanyasaji twajionea.

7.        Malishe wanyanyasika,

           Biashara kuvurugika,

           Hakika imesikika,

           Unyanyasaji twajionea.

8.       Hakika kuna mizungu,

          Shida zao na machungu,

          Kwao wanafunzi machungu,

          Unyanyasaji twajionea.

 

9.       Tena wengi wanalia,

           Madhira waugulia,

           Ni mengi utasikia,

          Unyanyasaji twajionea.

10.       Kwenye nyingi familia,

          Wanawake wanalia,

          Kichapo wavumilia,

          Unyanyasaji twajionea.

11.     Tena nyingi kadhia

          Waume waugulia,

          Unyumba kuulilia,

          Unyanyasaji twajionea.

12.     Wagonjwa hujililia,

          Wodini wakiingia,

          Vichapo vinatukia,

          Unyanyasaji twajionea.

13.      Machozi yabubujika,

            Kutwa wapo kwenye nyika,

            Masomo yamewakatika,

            Unyanyasaji twajionea.

 

14.       Mbugani wamechutama,

             Kama makinda yatima,

            Wawaza yao hatima,

            Unyanyasaji twajionea.

 

 

15.       Tena ni unyanyasaji,

            Usawa wa mfamaji,

            Huduma ukihitaji,

            Unyanyasaji twajionea.

 

16.      Utashinda barazani,

            Wao wamo ofisini,

            Utoe cha mfukoni,

            Huduma ukapateni.

 

17.      Nimengi matusi pia,

           Hakika tasimulia,

           Hatorudi takimbia,

          Maradhi kutorudia.

 

18.     Bado roho taabani,

          Mkulima na thamani,

          Mazao yao jamani,

          Unyanyasaji twajionea.

19.   Hawa wasomi jamani,

         Watuweka mtungani,

         Magonjwa mwaanzisheni,

         Unyanyasaji twajionea.

 

20.     Mwisho tumefikia,

           Mengi tumegusia,

           Ya moyo na hisia,

           Unyanyasaji twajionea.

 

Comments