FASIHI KWA UJUMLA
FASIHI KWA UJUMLA
Fasihi inajumuisha kazi mbali mbali za Sana'a ikiwemo sanaa za maonyesho na mengine meng.fasihi imejadiliwa kwa mapana zaidi na wataalamu mbalimbali, kwa ujumla wao wamejaribu kuonesha maana ya jumla ya fasihi.
MAANA YA FASIHI
Fasihi ni kazi ya sanaa ambayo hutumia lugha katika kufikisha ujumbe kwa jamii husika au kwa hadhira husika, fasihi Mara nyingi hutumia lugha ya mdomo au ya lugha ya maandishi katika kufikisha ujumbe mahususi kwa walengwa wake.
AINA ZA FASIHI
kuna aina mbili za fasihi ambazo ni fasihi simulizi na fasihi andishi.
FASIHI SIMULIZI
ni aina ya fasihi ambayo hutumia mdomo katika kufikisha ujumbe kwa hadhira iliyokusudiwa. Fasihi simizi Mara nyingi huwa na sifa kama vile ni Mali ya jamii mzima, hulenga kuelimisha jamii, pia fasihi simulizi huwasilishwa kwa njia ya masimulizi ya mdomo.
FASIHI ANDISHI
ni aina ya fasihi ambayo hutumia maandishi katika kufikisha ujumbe kwa hadhira iliyokusudiwa. Fasihi andishi huwasilishwa kwa njia ya maandishi yaweza kuwa ni maandishi yakwenye vitabu. Na Mara nyingi inakuwa rahisi katika uhifadhi wake
Vipera vya fasihi simulizi
Kuna vipera kadhaa vya fasihi simulizi. vipera hivyo ni kama vilivyonyeshwa hapo chini yaani
Hadithi
Tamathali za semi
ushairi
Nyimbo
Hadithi: ni masimulizi ya kisanaa ambayo husimulia visa vya kubuni.Mara nyingi hadithi hutumia masimulizi ya kinadharia tyu na huongezwa chumvi nyingi lengo LA hadithi ni kuelimisha na kuonya jamii mfano wa hadithi ni kama zile za sungura na fisi
Nyimbo: ni aina ya sanaa katika fasihi ambayo hutumia lugha teule, sauti na kiimbo maalumu, nyimbo huwa na mpangilio mzuri wa sauti yaani kupanda na kushuka kwa sauti
Maigizo:Mara nyingi huelezea visa vya kweli maigizo yanaweza kufanyika hadharani na lengo la kufanya maigizo ni kuelimisha na kuonya jamii
VIPERA VYA FASIHI ANDISHI
Vipera vya fasihi andishi vipo vitatu yaan
Mashairi
Riwaya
Tamthiliya
Mashairi; ni utungo wa kisanaa unaotumia lugha teule na mpangilio Fulani wa maneno, mashairi yanakuwa katika mishororo.mfano wa mashairi ni mashairi ya chekacheka
Riwaya, ni hadithi ndefu za kubuni yenye mawanda mapana, Luna riwaya ambazo huwa zina maneno mengi sana hadi kufikia maneno 50000 mfano wa riwaya ni riwaya ya watoto wa mama nitilie
Tamthiliya ni mojawapo ya vipengele vya fasihi andishi ambapo huwasilishwa kwa njia ya maandishi kwa kawaida riwaya huwa ni majibizano baina ya mtu zaidi ya mmoja tamtiliya inaweza kuigizwa jukwaani au inaweza kuandikwa kwenye maandishi, mfano wa tamtiliya ni kama vile kilio chetu na ngoswe penzi kitovu cha uzembe.
TOFAUTI KATI YA FASIHI ANDISHI NA FASIHI SIMULIZI
kuna utofauti mkubwa kati ya fasihi andishi na fasihi simulizi ambazo ni kama zifuatazo
1Uwasilishwaji, fasihi simulizi huwasilishwa kwa njia ya masimuizi ya mdomo lakini fasihi andishi huwasilishwa kwa njia ya maandishi
2.Umiliki, Fasihi simulizi ni mali ya jamii mzima lakini fasihi andishi ni baguzi kwa sababu inamilikiwa na watu wanaojuwa kusoma na kuandika tu
3. Ukale, fasihi simulizi ni ya kale zaidi lakini fasihi andishi imekuwepo baada ya kugundulika kwa maandishi
4. Uhifadhi, fasihi simulizi huhifadhiwa kichwani lakini fasihi andishi huhifadhiwa kwa njia ya mandishi.hizo ni baadhi ya tofauti kati ya fasihi andishi na fasihi simulizi
5.gharama, fasihi andishi ina ghrama katika kuiandaa kwa mfano lazima uandae peni na daftari hii ni kwasababu inaandikwa lakini fasihi simulizi haina gharama.
6. Muda, fasihi simulizi hutumia mda mchache katika uwasilishaji wake Tofauti na fasihi andishi.
UMUHIMU WA FASIHI
fasihi ina umuhimu kwa jamii, zifuatazo ni dhima za fasihi kwa jamii
-Kuelimisha jamii
-Kufurahisha au kuburudisha jamii
-Fasihi hulenga kukosoa jamii mfano hadithi
-Fasihi huonya jamii inayotuzunguka
UFANANO KATI YA FASIHI SIMULIZI NA FASIHI ANDISHI
- zote ni tanzu za fasihi
- zote hutumia lugha ya kisanaa kufikisha ujumbe kwa hadhira
DHIMA ZA FASIHI KWA UJUMLA
Fasihi kwa ujumla ina dhima nyingi kwa jamii zikiwemo kuelimisha, kukosoa, kuburudisha na kuonya jamii hivo fasihi ni chombo pekee kitumikacho katika ujenzi wa jamii mpya.
Comments
Post a Comment