Kategoria za kimuundo
Katika kazi hii kuna mgawanyo katika vipengele
mbalimbali ikiwemo utangulizi ambao utajikita kutoa nini maana ya kategoria ya
muundo ,pia kuna kiini cha swali ambacho kimefafanuliwa kwa kugusa kipengele
cha uhusiano uliopo baina ya kategoria
za kimuundo za sarufi miundo ya Kiswahili ,mwisho ni hitimisho la kazi husika.
Kategoria za kimuundo ,kwa mujibu wa khamisi
na Kiango (2002:9) dhana ya kategoria ilitumiwa na wanasarufi mapokeo kwa namna
tofauti na inavyotumiwa na wanasarufi mamboleo . dhana ya kategoria kama
ilivyotumika katika sarufi mapokeo ya akina Aristotle limetokana na neno la
kigiriki na kutafsiliwa kama ualifu (predication) .wao walitumia dhana ya
kategoria kuwa nis sifa bainifu zinazoambatana au zinazo ambikwa kwenye aina za
maneno kama vile idadi, nafsi, kauli ,ngeli ,njeo na kadhalika.
Kategoria kwa mtazamo wa kisarufi mambo leo ni jamii,
seti ,kundi au makundi yanayofanya kazi ya kufanana.aidha darajia yeyote ya
vipashio inayotambuliwa katika uchambuzi wa lugha Fulani huitwa kategoria. Kwa
sasa kategoria zipo katika viwango au darajia mbili, zifuatazo;
Kategoria za kikazi
Kategoria za kimuundo.
Kategoria za kimuundo,massamba na wenzake (2009)
anaeleza kuwa kategoria za kimuundo ni darajia inayojihusisha na mpangilio wa
maneno kstika sentensi na vipashio vyake kwa kua ngalia sharia na kanuni
zinazotawala miundo ya Kiswahili.
Miongoni mwa kategoria za kimiundo ni muundo kirai , muundo kishazi na
muundo sentensi.
KIRAI, kwa mujibu wa massamba na
wenzake (2009) anasema kirai ni kipashio cha kimuundo chenye neno moja au zaidi
lakini hakina muundo wa kiima na kiarifu.
Matei (2008) anafasili kirai kama fungu la maneno
ambalo hufanya kazi kama neno moja .kilai hudokeza maana lakini maana hiyo si
kamili na hakina muundo wa kiima na kiarifu.
Kutokana na wataalamu hawa tunmabaini kua kirai
kinaweza kuwa sehemu ya kiima au kiarifuhivyo tunaweza kuhitimisha kwa kufasili
kirai kama ni kipashio cha kimuundo kinachoanzia neno moja na kuendelea ambacho
hakina muundo wakiima na kiarifu.
KISHAZI ,kwa mujibu wa massamba na
wenzake (2001) wanasema kishazi ni tungo ndogo yenye uoanifu ndani yake .ambayo
ni kubwa kuliko neno lakini iliyo sehemu ya sentensi kubwa.
Matinde (2012)anafasili dahana ya kashazi kuwa ni neno
au kifungu cha maneno chenye kiima na kiarifu au kiarifu pekeyake ambacho ni
sehemu ya sentensi kuu.
Matei (2008) anafasili kuwa kishazi ni kundi la maneno lenye kiima kimoja
na kialifu kimoja .
Kwa ujumla
tunaweza kusema kuwa kishazi nitungo ambayo ina kiima na kiarifu na inaweza
kusimama pekee na kukamilisha maana au inaweza isisimame yenyewe na kukamilisha
maana.
Wahiga (1990) anasema sentensi ni tungo iliyo kamili
kisarufi ambayo inajitegemea kimaana. Kwahiyo kutokana na fasili hiyo tunaweza
kusema kwamba ,sentensi ni tungo kubwa yenye muundo wa kiima na kiarifu
inayojitosheleza kimaana.
Baadhi ya hoja zinazoonesha uhusiano wa kategoria za
kimuundo za sarufi miundo ya Kiswahili ni kama zifuatazo;
Hukamilishana kimuundo,taaluma ya sarufi
miundo huzingatia uhusiano uliopo wa kategoria za kimuundo ili kujenga tungo
yenye mantiki au mtiririko mzuri wa kimawazo mfano, “baba analima” tungo hii imeundwa na kategoria mbili za yaani kategoria ya kirai nomino “baba” na kategoria ya kishazi kitenzi “analima”.
Pia kategoria za kimuundo hukamilishana
kimaana, uhusiano mkubwa katika sarufi miundo ya Kiswahili huzingatia sana swala la uhusiano wa maneno
yaliopo katika tungop na namna yanavyo poangiliwa kwa kuzingatia sharia na
kanuni za lugha husika mfano, “wanafunzi wanasoma “ tungo hii imekamilika kimaana kutokana
na mpangilio mzuri wa maneno kimuundo yaani wanafunzi ni kirai na wanasoma ni
kirai kitenzi au tunaweza kuita kishazi kwa ujumla .kwa kawaida tungo ya Kiswahili katika uundaji wake wa tungo wenye
maana kama hioyo huzingatia huizingatria uhusiano wa kategoria za kimuundo.
Uhusiano
wa kategoria za kimuundo pia huzingatia uhusiano wa kisarufi, kwa kawaida
kategoria za kimuundo za sarufi miundo ya Kiswahili huzingatia zaidi upatanisho wa kisarufi uliopo kati ya nomino na kiambishi awali cha kitenzi,mfano
“ Motto anakula chakula.” Katika
tungo hiyo nomino inahusiana moja kwa moja na kiambishi awali cha kitenzi ankula
hivyo endapo kiambishi cha kitenzi kitabadilika kitapoteza uhusiano
baina yake kati ya nomino na
kitenzi.Mfano , Mtoto wanakula chakula.
Tungo hiyo haina kabisa upatanisho wa kisarufi ,hivyo basin i wazi kusema
kwamba sarufi miundo ya Kiswahili huundwa kwa kjuzingatia uhusiano wa kategoria
za kisarufi miundo.
Hukamilishana katika uhundaji wa tungo zenye mantiki, neno mantiki ni
neno lenye maana ya mtiririko na mpoangilio
katika kuunda tungo yenye maana inayojitosheleza.hivyo uhusiano wa
kategoria za sarufi miundo ya Kiswahili ni pamoja na kuwezesahna katika kuandaa
tungo zenye mantiki , mfano “mwalimu atasafili kesho asubuhi” katika tungo hii upo mtiriliko mzuri
unaokamilisha tungo kimantiki. Lakini pia tungo hii inaweza kukosa mantiki
endapo mpangilio wa kategoria za kimuundo hazitawekwa katika mpangilio mzuri au
kuto kuwepo kabisa .mfano “mwalimu atasafili” bado kuna kuwa na maswali mengi
ya kimantiki miongoni m,wa wasomaji kama muda atakaosafili , na kadharika.
Kwa ujumla sintaksia taaluma ya sintaksia ni taalauma
ya sarufi ambayo ndio msingi wa taaluma ya juu kabisa ya sarufi ambayo ni
semantiki kwani semantiki ambayo huchunguza maana ya maneno katika tungo ,maana
hizo haziwezi kuwa na mantiki endapo uchambuzi wa kina wa miundo wa maneno
hautazingatiwa katika taaluma ya sintaksia.
Comments
Post a Comment