Mofimu
UTANGULIZI.
Mofimu
Kihore (2017), akimnukuu Kamusi San if u ya Isimu na
Lugha (1990). Mofimu ni kipashio kidogo amilifu katika maumbo ya maneno.
Kipashio kidogo kina maana ya umbo la neno au umbo katika neno ambalo haliwezi
kugawika katika sehemu nyingine ndogo zaidi. Mfano mtu ni kipashio kidogo
kabisa katika neno mtu ni 'm'.
Aidha kipashio kuwa amilifu maana yake ni kwamba kina
kazi maalumu kisarufi kazi hizo zinaweza kuwa kubeba maana ya msingi katika
neno au kiambishi kinachowakilisha dhana au kipashio cha kisarufi kwa mfano
mtoto, 'M' ni mofimu yenye kazi ya kwanza kuonesha umoja, pili kubainisha kundi
la nomino ambamo nomino hiyo imo wakati kipashio toto ni mofimu inayobeba maana
ya msingi.
ALOMOFU.
Matinde, 2012. Alomofu ni maumbo mawili au zaidi yanayowakilisha
mofimu moja na hutokea katika mazingira maalumu ya utokeaji. Kwa mfano mti,
mchawi, mtoto, hizo ni alomofu, pia mwana, mwenge, mwangaza, muuguzi, muungano,
muumba, hiyo ma, mwa na mu ni Alomofu zinazowakilisha mofimu kiambishi Mu
katika mazingira tofauti ( Kihore, 2007).
MOFU.
Matinde, 2012, akimnukuu TUKI, 1990. Wanasema mofu ni
kipashio cha isimu maumbo kiwakilishacho mofimu. Hivyo basi mofu ni kipashio
cha kimuumbo au umbo ambalo huwakilisha mofimu, huweza kuandikwa au hata
kuandikwa na linalitumiwa kuwakilisha maana fulani katika neno. Mofu ndio umbo
ambalo hubeba mofimu. Mofu hubainishwa vizuri kwa kuzingatia maumbo ya maneno
ya ndani badala ya maumbo ya nje. Hii kwa sababu maumbo ya nje yanaweza
kuathiriwa na mifanyiko ya kifonolojia na kimofolojia ambayo inaweza kudondoa,
kuchopeka au hata kuunganisha viambishi katika neno. Mofu huwakilishwa na
ishara ya mabano { }. Mfano
Neno Mofu
Mtu { m }, { tu }
Analima { a } { na }
{lim } { a }.
Ubainisho wa mofimu katika lugha umetegemezwa katika
dhana kwamba umbo la neno huweza kugawanyika katika vipande ( Kihore, 2007).
Seti, ni kundi la vifaa au
vitu vya aina moja vinavyohusiana katika kukamilisha shughuli ( TUKI, 2014).
Hivyo basi mofimu zilizosetiliwa katika mofu au alomofu ni kwamba kundi la
vipashio vidogo amilifu katika maumbo ya maneno. Kimsingi kundi hilo la mofimu
( mofimu zilizosetiliwa ) huwa na uamilifu fulani katika maneno.
Kwakua, mofimu huweza kusetiliwa katika maumbo ya
maumbo ya maneno hivyo pia huweza kugawika ( Kihore, 2007 ) anadai kuwa
ubainisho wa mofimu katika lugha umetengenezwa katika dhana kwamba umbo la neno
huweza kugawanyika katika vipande. Kwa kuzingatia maelezo hayo ya Kihore hivyo
basi tunaweza kubaini mofimu zilizosetiwa katika mofu au alomofu za maneno kwa
kugawanya maneno hayo katika vipashio vidogo zaidi vya kiuamilifu katika neno
kama inavyojidhihirisha katika maneno yafuatayo:
( a) Mkono = m- kono
Hili neno ni nomino
Hili neno lina mofimu mbili m- kono
M - imetumika kuonyesha umoja
- kubainisha
kundi la nomino ambayo nomino hiyo imo. Nomino hii ipo kwenye kundi la
nomino U - I
mfano Mkono umevunjika - mikono imevunjika.
Kono
- hubeba maana ya msingi.
(
b ) Ujana = U - Jana
Ujana - ni nomino dhahania kwa maana
hufikirika tu hauwezi kushikika.
Neno hili lina mofimu mbili U -
jana
U - Ni
mofimu tegemezi ambayo imesetiliwa katika mofu jina na kubadilisha kategoria ya
neno kutoka kielezi cha wakati na kuwa nomino dhahania.
Jana - maana
ya msingi.
( c ) Uzeeni = u- zee - ni
Ni
kielelezo cha hali
U - ni
mofu inayoonesha hali ya kuzeeka
-
imetumika kubadilisha kundi la nomino ambayo nomino hiyo imo. Nomino hii ipo
katika kundi la U - U ( Matinde, 2012 ).
Zee =
hubeba maana ya msingi
ni =
mofu inayobadilisha neno kuwa kielezi.
(d ) Wachezaji = wa - chez - a - ji
Ni
nomino
Wa - hudokeza
nafsi ya tatu wingi yaani wao
Chez - ni mzizi wa neno
a - ni mofu
tamati kijenzi cha shina
ji - ni mofu
tamati kijenzi cha maana
- ni
kiambishi cha nomino. Mofu tamati 'ji' huingiza dhana kama vile kurudiwarudiwa
kwa tendo ( Kihore, 2007 ).
( e ) Anatupenda = a - na - tu - pend - a
Ni
kitenzi
a - ni
mofu ambayo hudokeza nafsi ya tatu umoja
na - ni
mofimu ambayo hudokeza njeo au wakati ( wakati uliopo endelevu )
tu -
ni mofimu ambayo hudokeza urejeshi wa mtenda yaani anayetupenda sisi
pend
- ni mzizi wa neno anatupenda
a
- mofimu tamati maana
(
f ) Ogofya = ogo - fy - a
Neno hili ni tendo au kitenzi
Ogo -
ni mofimu ambayo hubeba maana ya msingi
fy - ni mofimu kiambishi cha utendeshi
a -
kiambishi tamati maana
( g ) Levya = le - vy - a
Neno hili
ni kitenzi
le -
mzizi wa neno
vy - ni
mofimu kiambishi ambayo hubeba dhana ya utendeshi
a - ni
mofimu kiambishi tamati
( h ) Vitabu = vi - tabu
Ni
nomino
Vi -
mofimu kiambishi cha wingi
-
hubainisha kundi la nomino ambalo nomino vitabu imo ( KI - VI )
tabu - ni mofu ambayo hudokeza maana ya msingi ya neno
HITIMISHO
Hivyo basi maneno
haya yamesetiliwa kwa kuzingatia mofu na alomofu kwa kuzingatia uamilifu au
kazi ya kila neno na kuligawanya neno katika vipande kuanzia kipashio kikubwa
mpaka kipashio kidogo kabisa cha neno.
MAREJEREO.
Kihore, M. na Wenzake (2007). Sarufi\ Maumbo ya Kiswahili Sanifu ( SAMAKISA ) Sekondari na Vyuo. Dar es salaam: TUKI
Matinde, R. S. ( 2012 ). Dafina ya Lugha, Isimu na Nadharia: Kwa Sekondari, Vyuo vya Kati na
Vyuo Vikuu. Mwanza: Serengeti
Educational Publishers ( T ) Ltd.
TUKI ( 2014 ). Kamusi
ya Kiswahili Sanifu. Oxford University Press.
Comments
Post a Comment