. Semantiki
Kazi hii imegawanyika katika sehemu kuu tatu, sehemu ya
kwanza ni utangulizi, sehemu ya pili ni kiini cha kazi na sehemu ya tatu ni
hitimisho la kazi kwa ujumla.
Massamba (2004:75) anafasili dhana ya semantiki kuwa ni
taaluma ya isimu inayojishughulisha na uchunguzi na uchambuzi wa maana za
maneno na tungo katika lugha. Semantiki imegawanyika katika makundi manne
ambayo ni leksika, mantiki, muundo na nadharia.
hata hivyo hakuna ufafanuzi wa kutosha kuhusu maana ingawa
katika hali ya kawaida tunaishia kutoa sifa za kitu na siyo maana.
Kwa mujibu wa Crystal, D (1987) semantiki ni utanzu wa isimu
unaochunguza maana katika lugha. Kwa mukhtasari, semantiki hutalii maana katika
vipashio vyote vya kiisimu katika viwango vyote vya lugha mathalan fonolojia,
mofolojia na sintakisia.
Aidha, semantiki inaweza kufasiliwa kwa namna mbalimbali
jinsi ifuatavyo:
Maana anuwai za dhana ya semantiki
1.
Semantiki ni stadi ya maana
2.
Semantiki ni utanzu wa isimu unaongalia maana ya
maana.
Semantiki ni taaluma katika isimu ambayo hushughulikia maana
ya maumbo au sentensi katika lugha. Taaluma hii ilianza enzi za Aristotle na
Plato ambao walizingatia zaidi sifa za maana, katika kipindi hicho walitaka
kujua sifa na tabia za maana. Leech (1981).
Habwe na Karanja wakimnukuu Richard na Wenzake (1985)
wanasema “Semantiki ni stadi ya maana. Semantiki ni utanzu unaochunguza maana
katika lugha ya mwandamu”. Wanaendelea kusema semantiki hutafiti maana za
fonimu, mofimu, maneno na tungo. Hivyo kutokana na fasili hii maana
hushughulikiwa katika vitengo au viwango vyote vya lugha ambavyo ni fonolojia,
mofolojia na sintaksia.
Hivyo kutokana na maana zilizotolewa na wataalamu mbali mbali
happy juu wanakundi tumetoa maana ya semantiki kuwa,
Semantiki.ni utanzu wa isimu ambao unajishugulisha na
uchunguzi,uchambuzi na kutafiti maana za lugha ya binadamu kutoka kiwango Cha
neno mpaka kiwango Cha tungo.
Hivyo kwa ujumla Semantiki ni taaluma katika isimu ambayo
hushughulikia maana ya maumbo au sentensi katika lugha. Taaluma hii ilianza
enzi za Aristotle na Plato ambao walizingatia zaidi sifa za maana, katika
kipindi hicho walitaka kujua sifa na tabia za maana. Hii inamaanisha kwamba
semantiki hutalii maana katika vipashio vyote vya kiisimu katika viwango vyote vya lugha yaani fonolojia,
mofolojia na sintakisia.
Kwa sababu hii ni sawa kusema kuwa maana hujishugulikiwa katika
tanzu za isimu Kama fonolojia ,mofolojia,na sintaksia .semantiki inakuwa ndio makutano
ya taaluma nyingine
Semantiki kama taaluma nyingine ina mahusiano na taauma
nyingine kama ifuatavyo katika mchoro na hatimaye katika maelezo yanayo eleza
vipengele mbalimbali vya lugha:-
Mchoro kuonesha
mahusiano ya semantiki na vipengele vingine vya lugha kama
sintaksia,mofolojia na fonolojia.Kuwepo kwa semantiki katikati inamaana kwamba
tawi hili ni muhimili wa matawi mengine.
Fonolojia ni tawi la
isimu ambalo hujishughulisha na uchunguzi na uchambuzi wa mfumo wa sauti katika
lugha, huchunguza jinsi ambayo vitamkwa au sauti za lugha zinavyoungana ili
kujenga maneno yanayokubalika katika lugha ya mawasiliano. Ili lugha ya
mawasiliano iwe kamili ni dhahiri kwamba mpangilio wa sauti lazima uwe na maana
ili kufikisha ujumbe, hivyo semantiki inauhusiano mkubwa na fonolojia.
Mfano: Neno “UA” linamaanisha sehemu ya mmea maalumu kwa kutoa mbegu na kuvutia wadudu kwa
ajili ya uchavushaji lakini ikibadiliswa vitamkwa na kuwa ‘au’ huleta maana
tofauti na maana ya awali.
Mofolojia ni taaluma
inayoshughulikia vipashio vya lugha katika kuunda maneno. Tawi hili la isimu
huchunguzi na kuchambuzi wa maumbo ya maneno na jinsi maumbo hayo yanavyotumika
katika lugha. Jukumu la neno husika katika sentensi hubainika vyema kulingana
na uhusiano baina ya maneno mengine katika tungo. Maumbo ya kimofolojia
huathiri vipengele vingine vya kisemantiki. Hivyo semantiki ina mahusiano na
taaluma ya mofolojia kwa kuwa ili lugha iweze kueleweka lazima iwe na mpangilio
na muundo mzuri wa vipashio vya sentensi ili kuleta maana katika mawasiliano.
Mfano: Mwalimu
anaimba
Walimu wanaimba
Katika mfano huu katika upande wa kiima kiambishi m
kinaashiria umoja na wa inaashiri wingi, katika upande wa kiarifu viambishi a katika upande
wa kiima vinaashiria nafsi ya tatu umoja na wa vinaashiria nafsi ya tatu wingi,
hivyo maumbo ya maneno lazima yawe na maana.
Sintaksia, ni utanzu
wa sarufi unaojihusisha na uchunguzi wa mpangilio wa maneno katika sentensi na
uhusiano wa vipasho vyake. Utanzu huu huchunguza sheria au kanuni zinazofuatwa katika kuyapanga
maneno ili yalete maana inayokubalika na kueleweka katika lugha husika, . Kwa
mantiki hii, kwa kuwa semantiki hushughulikia viwango vyote vya lugha, basi
hushughulikia pia kiwango cha sintaksia ambapo huangalia maana za tungo, kwani
tungo lazima ikubalike kwa wazungumzaji pia tungo lazima ilete maana.
Kwa mfano,
Pana huimba vizuri akiwa mubashara
Mubashara huimba vizuri akiwa pana.
Vizuri huimba pana akiwa mubashara.
Katika mifano hii sentensi (1) inampangilio sahihi katika
lugha ya Kiswahili hivyo inamaana na inawezesha mawasiliano, na sentesi
zilizobaki hazijafuata mpangilio sahihi wa kimuundo wa lugha ya Kiswahili hivyo hazina maana na
hazifanikishi mawasiliano.
Kwa ujumla semantiki ni tawi la isimu kama matawi mengine ya
isimu ambalo haliwezi kujikamilisha lenyewe pasipo kuhusiana na matawi mengine
ili kukamilisha mawasiliano. Lakini semantiki inaweza kutofautiana na matawi
mengine kwa kuanza na tafsiri yake ambayo inajieleza na imetofautiana kabisa
kidhima na matawi mengine ambayo ni fonolojia, sintaksia, na mofolojia. Pia
dhima zake hazifanani na matawi mengine ya isimu.
MAREJEO
Habwe, J na P. Karanja (2004). Misingi ya Sarufi ya
Kiswahili. Nairobi: Phoenix Publishers Ltd.
Massamba P. B. D (2004) Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha.
Dar es Salaam: TUKI
Massamba, D.P.B na wenzake (1999). Sarufi Miundo ya
Kiswahili Sanifu: Sekondari na Vyuo.
Dar essalaam: TUKI.
Massamba (2004) anafasili dhana ya semantiki kuwa ni taaluma
ya isimu inayojishughulisha na uchunguzi na uchambuzi wa maana za maneno na
tungo katika lugha.
Comments
Post a Comment