SEMITIKI
Kazi yetu
imegawanyika Katia sehemu tatu, ambapo Kuna utangulizi, kiini cha swali na
hitimisho. Pia Katika utangulizi tumeelezea maana ya lugha, Katika kiini cha
swali tumeonyesha jinsi usemitiki wa lugha ya binadamu
unavyojitokeza na mwisho tumemalizia na hitimisho la kazi.
UTANGULIZI
Lugha imeweza kufasiliwa na wataalam mbalimbali kulingana na
uelewa wa kila mmoja kuhusu dhana ya lugha. Baadhi ya wataalam hao ni kama
wafuatao;
Sapir. (1921) anaeleza dhana ya lugha kuwa, ni mfumo ambao
binadamu anajifunza ili atumie
kuwasilisha mawazo na maoni . Anasema mfumo huu hutumia ishara ambazo hutolewa kwa hiari, na anaendelea
kusema kuwa ili binadamu waweze kuwasiliana iliwabidi wabuni mfumo Fulani wa ki ishara ambao
wangetumia kuwasiliana miongoni mwao
katika jamii. Fasili hii ina udhaifu katika kufasili dhana ya lugha
Kwa kuwa imeegemea
zaidi katika matumizi ya ishara na hivyo kuonesha kwamba suala la sauti
halikutiliwa maanani ilihali sauti ndio msingi mkubwa katika lugha.
Pia TUKI (2004), wanatoa fasili kuwa lugha ni mpangilio wa
sauti na maneno unaoleta maana ambao hutumiwa na watu wa kabila au taifa Fulani
kwaajili ya mawasiliano.Tuki nao wana
udhaifu katika kueleza maana ya lugha kwani wamejikita zaidi katika kuzingatia suala la
sauti na maneno na kusahau matumizi ya ishara kuwa ni sehemu ya lugha katika
mawasiliano.
Kwa ujumla kutokana na fasili hizo tunaweza kusema kwamba
lugha ni mfumo wa ishara na sauti za nasibu ambazo zimekubaliwa na watu wa
jamii Fulani ili ziweze kutumika katika mawasiliano yao ya kila siku katika nyanja mbalimbali za maisha,
kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni.
SEMITIKI
Kwa mujibu wa Lyons,J.
(1977), anafasili semitiki kuwa ni sayansi ya alama, ishara au na mfumo wa mawasiliano.
Pia tunaweza kufasili semitiki kuwa ni taaluma ya
ishara,alama na mawasiliano.
wazo la msingi katika fasili ya semitiki ni matumizi ya
ishara, alama na sauti katika
kukamilisha mawasiliano.
Ferdinand de Saussure (1974), anaeleza kuwa ishara ndio kipashio cha kimsingi cha mawasiliano
katika jamii, ambapo yeye aliita ishara ya neno kiashiria na aliita maana ya
ishara hiyo kiashiriwa,dhana au kitajwa.
Mfano.
a)π¦ -(kiashiria) ➡️
kipepeo-(kiashiriwa)
b)πΊπΈπ΅️
-(kiashiria) ➡️ maua-(kiashiriwa)
Uhusiano uliopo baina ya dhana hizi mbili siyo wa moja kwa
moja bali ni wa kidhahania tu. Maana haiwezi kuwepo bila umbo linalohusIshwa
nalo. De Saussure alisisitiza kwamba maana ya neno kama ishara ya kiisimu hujengwa kutokana na mahusiano ya maana iliyopo .
Mtu anayejifunza semitiki anakuwa anahusika na mambo matatu
ambayo ni;
i)Semantiki, yaani
uhusiano baina ya ishara, alama na vitu
vinavyorejelewa na ishara hizo.
ii)Sintaksia, hii inahusisha uhusiano baina ya ishara pamoja
na alama katika muundo maalum.
iii)Pragmatiki, ni mahusiano baina ya alama, ishara na
fasili zake kwa watumiaji wa ishara na alama hizo.
USEMITIKI WA LUGHA YA
MWANADAMU
Usemitiki wa lugha ya
mwanadamu unaweza kuthibitika kwa kurejelea
fasili za wataalam mbalimbali ambao wameelezea dhana ya lugha kwa namna ifuatayo;
A)Sapir (1921), ) anaeleza dhana ya lugha kuwa ni mfumo
ambao binadamu anajifunza ili atumie
kuwasilisha mawazo na maoni . Anasema mfumo huu hutumia ishara ambazo hutolewa kwa hiari, na anaendelea
kusema kuwa ili binadamu waweze kuwasiliana iliwabidi wabuni mfumo fulani wa ki- ishara ambao wangeutumia kuwasiliana miongoni mwao katika jamii.
B)Barton D. (2004 ),
Lugha ni mfumo wa ishara ambao huunganisha yaliyomo akilini au kichwani
mwa mtu na nje ya mazingira ya kawaida.
Kwa kurejelea fasili za wataalam hao,tunaona vitu vya msingi
vinavyojitokeza ni matumizi ya sauti(maneno) na alama au ishara katika
mawasiliano.
Pia, kwa mujibu wa Charles
F. Hockett (1948), usemitiki wa lugha unatokana na matumizi ya ishara au
alama za kinasibu na sauti zitumikazo katika mawasiliano kama ifuatavyo;
Hivyo basi usemitiki wa lugha ya mwanadamu upo katika
matumizi ya Sauti na alama au ishara katika mawasiliano.
Sauti (maneno); Data za utafiti wa semitiki kiisimu ni maneno,
binadamu wanapowasiliana huweza kutumia maneno au sauti.kwa mujibu wa
Wood,(2019) maneno (sauti) hizo zitumiwazo
ni alama za kiisimu(fonetiki),na hivyo ndivyo unavyotokea usemitiki was lugha
ya mwanadamu.
Mfano,I)-kiswahili.
Sauti za
kawaida Alama za sauti hizo kifonetiki
t
d
k
ii)kiingereza:
See/si:/
Say/seI/
Katika mifano
hapo juu sauti na maneno katika lugha huweza kuandikwa kawaida au huweza
kuwakilishwa na alama za kiisimu ambazo kwa kawaida hurejelea kitu
kimoja,matumizi ya alama hizo za kiisimu ndio usemitiki wenyewe.Lakini pia zipo
sauti ambazo hazihusishi matamshi au maneno nazo huashiria kitu husika,mfano ni
kupiga mluzi,filimbi na hata ngoma pia nI njia mojawapo ya kuwasiliana.
Matumizi ya ishara;
Radford pamoja na Seeger (2008) wanasema, ishara inahusisha mielekeo na mienendo ya
viungo katika mwili wa binadamu, kama vile mikono, mabega, kichwa, uso na pia
sehemu nzima ya mwili badala ya kuhusisha sauti.Upo uwezekano wa wanadamu
kuwasiliana kwa kutumia ishara na wakaelewana vizuri pasipo kutoa sauti.
Mfano;
Γ
Kutikisa mabega, ni ishara ya kukataa kitu au jambo Fulani.
Γ
Kupunga mkono,
huashiria ishara ya kutoa salamu au kuagana .
Γ
Kutikisa kichwa,
hii ni ishara ya kukubali au kukataa.
Γ
Namna ya uwekaji wa macho, inaonesha kusitisha
au kulificha jambo Fulani lisitamkwe au kitu Fulani kisifanyike.
Γ
Pia uso , unaweza hali ya kufurahi au kukwazika na jambo au kutokubaliana.
Matumizi ya alama ;
Usemitiki wa lugha ya
mwanadamu pia unajidhihirisha katika
matumizi ya alama kama nyenzo mojawapo ya mawasliano . Alama hujumuisha kitu,
mchoro, au kifaa ambacho hutambulisha kingine au kutoa tarifa juu ya jambo fulani.
Kama vile tukio au kuonesha sehemu. Alama zinaweza kuwa za kiuandishi au
maandishi na alama za kuchorwa.
a)Alama za maandishi au uandishi , hizi hujumuisha alama
zinazotumika katika uandishi. Mfano
nukta ( . ), alama ya mshangao ( ! ), alama ya kuuliza ( ? )
na alama zinazoandikwa sehemu mbalimbali kwa lengo la kutoa taarifa fulani au
kuonesha mahali kama vile ofisini, chooni na kadhalika.
b)Alama za michoro; Hizi huchorwa kwa lengo la kutoa taarifa fulani au kuzuia
au kukumbusha jambo fulani. Mfano wa alama au michoro ni kama vile alama za
usalama barabarani ambazo zinakusudia kutoa taarifa kwa watumiaji wa barabarani
na kutoa maelezo ili kuepusha ajali. Pia
alama zinazochorwa katika nguo ambazo zinakuwa na lengo la kumtarifu dobi nguo
hiyo ipigwe pasi kwa moto mkali au kwa moto wa kawaida au kwa moto mdogo au isipigwe pasi
kabisa.
Hii ni Alama ya mshale ambayo unatumika kuonesha sehemu au
mahali mtu anapotaka kwenda kama vile chooni, ofisini na sehemu nyininezo
kutokana na sifa Fulani. Hivyo Katika Alama hutoa taarifa Fulani pasipo
kuhusisha sauti Katika muktadha hiyo.
pembe nane
Mchoro
✓Simama kabisa kwenye mstari mweupe, kwenye njia ya
wanaopita kwa mguu au usawa wa kibao. Subiri
✓magari yapite, na watu wapite kabla ya kuendelea.
✓Kuna junksheni zingine ni FOUR WAY STOP, kuna vibao vya
kusimama kila kona. Kwenye junksheni hizo,
✓lazima magari yote yasimame kabisa. Kama magari mawili au
zaidi yanafika kwa pamoja, lazima
✓usimame kabisa na gari lilipo mkono wako wa kulia ana haki
ya kupita kwanza.
pembe tatu
Mchoro
✓Lazima upunguze mwendo, uwe tayari kusimama.
✓Achie magari, mabaiskeli na wanaopita kwa mguu wapite
kwanza, halafu uendelee.
Pembe nne ndefu, Sheria na Taarifa
Mchoro
✓Kama kibao kimesimama ina maelekezo ya sheria.
✓Kama kibao kimelala ina maelekezo ya taarifa.
Pembe nne
Mchoro
✓Tahadhari, mabadiliko au hatari iko mbele
✓Punguza mwendo na uwe tayari kusimama .
Pembe tano
Mchoro
✓Eneo ya shule- zinatoa taarifa ya eneo ya wapita kwa mguu
karibu na shule
Hitimisho
Kwa ujumla, taaluma ya semitiki ina mchango mkubwa sana
katika lugha ya mwanadamu, haskatika lengo kuu la kurahisisha mawasiliano kwa
mbinu mbalimbali kama vile ishara,alama na sauti,kulingana na mawasiliano
yenyewe na wahusika wa mawasiliano hayo,mfano iwapo wahusika wa mawasiliano
hayo ni bubu au viziwi ishara na alama zitatumika kuwasilisha ujumbe
uliokusudiwa kufikiwa na wahusika hao.
MAREJELEO;
Radford G. & F. Seeger (2008); Semiotics in Mathematics
Education; Epistemology ,History, Classroom and Culture. Serve Publisher
Sapir E. (1921), Language ; An Introduction to the Study
of speech New York ; Harwat Bracea
company Publishers
TUKI, (2004), Kamusi
ya Kiswahili Sanifu, Dar-Es-Salaam; Oxford University Press.
Ferdinand de
Saussure, (1974), Course in General
Linguistic ; Semiotic London;
Sage Publications.
Barton D. (2013), Language Online Canada; Routledge
Wood S.K (2019), Sign Languages Structures and Contexts;
Boutledge.
Comments
Post a Comment