TUKI

 

Kazi yetu imegawanyika Katia sehemu tatu, ambapo Kuna utangulizi, kiini cha swali na hitimisho. Pia Katika utangulizi tumeelezea maana ya lugha, Katika kiini cha swali  tumeonyesha  jinsi usemitiki wa lugha ya binadamu unavyojitokeza na mwisho tumemalizia na hitimisho la kazi.

UTANGULIZI

Lugha imeweza kufasiliwa na wataalam mbalimbali kulingana na uelewa wa kila mmoja kuhusu dhana ya lugha. Baadhi ya wataalam hao ni kama wafuatao;

Sapir. (1921) anaeleza dhana ya lugha kuwa, ni mfumo ambao binadamu  anajifunza ili atumie kuwasilisha  mawazo na  maoni . Anasema mfumo huu hutumia ishara  ambazo hutolewa kwa hiari, na anaendelea kusema kuwa ili binadamu waweze kuwasiliana iliwabidi wabuni  mfumo Fulani wa ki ishara ambao wangetumia  kuwasiliana miongoni mwao katika jamii. Fasili hii ina udhaifu katika kufasili dhana ya lugha

Kwa  kuwa imeegemea zaidi katika matumizi ya ishara na hivyo kuonesha kwamba suala la sauti halikutiliwa maanani ilihali sauti ndio msingi mkubwa katika lugha.

Pia TUKI (2004), wanatoa fasili kuwa lugha ni mpangilio wa sauti na maneno unaoleta maana ambao hutumiwa na watu wa kabila au taifa Fulani kwaajili ya mawasiliano.Tuki nao wana  udhaifu katika kueleza maana ya lugha kwani  wamejikita zaidi katika kuzingatia suala la sauti na maneno na kusahau matumizi ya ishara kuwa ni sehemu ya lugha katika mawasiliano.

Kwa ujumla kutokana na fasili hizo tunaweza kusema kwamba lugha ni mfumo wa ishara na sauti za nasibu ambazo zimekubaliwa na watu wa jamii Fulani ili ziweze kutumika katika mawasiliano yao ya  kila siku katika nyanja mbalimbali za maisha, kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni.

SEMITIKI 

Kwa mujibu wa  Lyons,J. (1977), anafasili semitiki kuwa ni sayansi ya alama, ishara au na mfumo wa mawasiliano.

Pia tunaweza kufasili semitiki kuwa ni taaluma ya ishara,alama na mawasiliano.

wazo la msingi katika fasili ya semitiki ni matumizi ya ishara, alama na sauti  katika kukamilisha mawasiliano.

Ferdinand  de  Saussure (1974), anaeleza kuwa  ishara ndio kipashio cha kimsingi cha mawasiliano katika jamii, ambapo yeye aliita ishara ya neno kiashiria na aliita maana ya ishara hiyo kiashiriwa,dhana au kitajwa.

          Mfano.

                     a)  -(kiashiria)  kipepeo-(kiashiriwa)

                 b) -(kiashiria) maua-(kiashiriwa)

Uhusiano uliopo baina ya dhana hizi mbili siyo wa moja kwa moja bali ni wa kidhahania tu. Maana haiwezi kuwepo bila umbo linalohusIshwa nalo. De Saussure alisisitiza kwamba maana ya neno kama ishara ya kiisimu  hujengwa kutokana na mahusiano ya  maana iliyopo .

Mtu anayejifunza semitiki anakuwa anahusika na mambo matatu ambayo ni;

i)Semantiki,  yaani uhusiano baina ya  ishara, alama na vitu vinavyorejelewa na ishara hizo.

ii)Sintaksia, hii inahusisha uhusiano baina ya ishara pamoja na alama katika muundo maalum.

iii)Pragmatiki, ni mahusiano baina ya alama, ishara na fasili zake kwa watumiaji wa ishara na alama hizo.

USEMITIKI WA LUGHA YA MWANADAMU

Usemitiki wa lugha ya mwanadamu unaweza kuthibitika kwa  kurejelea fasili za wataalam mbalimbali ambao wameelezea dhana ya lugha  kwa namna ifuatayo;

A)Sapir (1921), ) anaeleza dhana ya lugha kuwa ni mfumo ambao binadamu  anajifunza ili atumie kuwasilisha  mawazo na  maoni . Anasema mfumo huu hutumia ishara  ambazo hutolewa kwa hiari, na anaendelea kusema kuwa ili binadamu waweze kuwasiliana iliwabidi wabuni  mfumo fulani wa ki- ishara ambao wangeutumia  kuwasiliana miongoni mwao katika jamii.

B)Barton D. (2004 ),  Lugha ni mfumo wa ishara ambao huunganisha yaliyomo akilini au kichwani mwa mtu na nje ya mazingira ya kawaida.

Kwa kurejelea fasili za wataalam hao,tunaona vitu vya msingi vinavyojitokeza ni matumizi ya sauti(maneno) na alama au ishara katika mawasiliano.

Pia, kwa mujibu wa Charles  F. Hockett (1948), usemitiki wa lugha unatokana na matumizi ya ishara au alama za kinasibu na sauti zitumikazo katika mawasiliano kama ifuatavyo;

Hivyo basi usemitiki wa lugha ya mwanadamu upo katika matumizi ya Sauti na alama au ishara katika mawasiliano.

Sauti (maneno); Data za utafiti wa semitiki kiisimu ni maneno, binadamu wanapowasiliana huweza kutumia maneno au sauti.kwa mujibu wa Wood,(2019) maneno (sauti) hizo zitumiwazo ni alama za kiisimu(fonetiki),na hivyo ndivyo unavyotokea usemitiki was lugha ya mwanadamu.

           Mfano,I)-kiswahili.

        Sauti za kawaida   Alama za sauti hizo kifonetiki

t  [t]

d [d]

k [k]

ii)kiingereza:

                      See/si:/

                       Say/seI/  

     Katika mifano hapo juu sauti na maneno katika lugha huweza kuandikwa kawaida au huweza kuwakilishwa na alama za kiisimu ambazo kwa kawaida hurejelea kitu kimoja,matumizi ya alama hizo za kiisimu ndio usemitiki wenyewe.Lakini pia zipo sauti ambazo hazihusishi matamshi au maneno nazo huashiria kitu husika,mfano ni kupiga mluzi,filimbi na hata ngoma pia nI njia mojawapo ya kuwasiliana.                     

Matumizi ya ishara;

Radford pamoja na Seeger (2008) wanasema,  ishara inahusisha mielekeo na mienendo ya viungo katika mwili wa binadamu, kama vile mikono, mabega, kichwa, uso na pia sehemu nzima ya mwili badala ya kuhusisha sauti.Upo uwezekano wa wanadamu kuwasiliana kwa kutumia ishara na wakaelewana vizuri pasipo kutoa sauti.

      Mfano;

Kutikisa mabega,    ni ishara ya kukataa kitu au jambo Fulani.

Kupunga mkono,  huashiria ishara ya kutoa salamu au kuagana .

Kutikisa kichwa,  hii ni ishara ya kukubali au kukataa.

Namna ya uwekaji wa macho, inaonesha kusitisha au kulificha jambo Fulani lisitamkwe au kitu Fulani kisifanyike.

Pia uso , unaweza hali ya  kufurahi au kukwazika na jambo au   kutokubaliana.

Matumizi ya alama ;

 Usemitiki wa lugha ya mwanadamu pia unajidhihirisha  katika matumizi ya alama kama nyenzo mojawapo ya mawasliano . Alama hujumuisha kitu, mchoro, au kifaa ambacho hutambulisha kingine au kutoa tarifa juu ya jambo fulani. Kama vile tukio au kuonesha sehemu. Alama zinaweza kuwa za kiuandishi au maandishi na alama za kuchorwa.

a)Alama za maandishi au uandishi , hizi hujumuisha alama zinazotumika katika uandishi. Mfano

nukta ( . ), alama ya mshangao ( ! ), alama ya kuuliza ( ? ) na alama zinazoandikwa sehemu mbalimbali kwa lengo la kutoa taarifa fulani au kuonesha mahali kama vile ofisini, chooni na kadhalika.

b)Alama za michoro; Hizi huchorwa  kwa lengo la kutoa taarifa fulani au kuzuia au kukumbusha jambo fulani. Mfano wa alama au michoro ni kama vile alama za usalama barabarani ambazo zinakusudia kutoa taarifa kwa watumiaji wa barabarani na kutoa maelezo  ili kuepusha ajali. Pia alama zinazochorwa katika nguo ambazo zinakuwa na lengo la kumtarifu dobi nguo hiyo ipigwe pasi kwa moto mkali au kwa moto wa kawaida  au kwa moto mdogo au isipigwe pasi kabisa. 

 


Hii ni Alama ya mshale am ;

bayo unatumika kuonesha sehemu au mahali mtu anapotaka kwenda kama vile chooni, ofisini na sehemu nyininezo kutokana na sifa Fulani. Hivyo Katika Alama hutoa taarifa Fulani pasipo kuhusisha sauti Katika muktadha hiyo.

pembe nane

a)      Simama kabisa kwenye mstari mweupe, kwenye njia ya wanaopita kwa mguu au usawa wa kibao. Subiri

b)      magari yapite, na watu wapite kabla ya kuendelea.

c)      Kuna junksheni zingine ni FOUR WAY STOP, kuna vibao vya kusimama kila kona. Kwenye junksheni hizo,

d)      lazima magari yote yasimame kabisa. Kama magari mawili au zaidi yanafika kwa pamoja, lazima

e)      usimame kabisa na gari lilipo mkono wako wa kulia ana haki ya kupita kwanza.

 Pembe tatu

a)      Lazima upunguze mwendo, uwe tayari kusimama.

 

 

b)      Achie magari, mabaiskeli na wanaopita kwa mguu wapite kwanza, halafu uendelee.

Pembe nne ndefu, Sheria na Taarifa

a)      Kama kibao kimesimama ina maelekezo ya sheria.

b)      Kama kibao kimelala ina maelekezo ya taarifa.

 

Pembe nne

a)      Tahadhari, mabadiliko au hatari iko mbele

b)      Punguza mwendo na uwe tayari kusimama.

 Pembe tano

 

a)      Eneo ya shule- zinatoa taarifa ya eneo ya wapita kwa mguu karibu na shule

Hitimisho

Kwa ujumla, taaluma ya semitiki ina mchango mkubwa sana katika lugha ya mwanadamu, haskatika lengo kuu la kurahisisha mawasiliano kwa mbinu mbalimbali kama vile ishara,alama na sauti,kulingana na mawasiliano yenyewe na wahusika wa mawasiliano hayo,mfano iwapo wahusika wa mawasiliano hayo ni bubu au viziwi ishara na alama zitatumika kuwasilisha ujumbe uliokusudiwa kufikiwa na wahusika hao.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

MAREJELEO;

Barton D. (2013), Language Online Canada; Routledge

Ferdinand  de Saussure,  (1974), Course  in General  Linguistic ; Semiotic  London; Sage             Publications.

Radford G. & F. Seeger (2008); Semiotics in Mathematics Education; Epistemology, History,      Classroom and Culture. Serve Publisher

Sapir  E. (1921),  Language ; An Introduction to the Study of  speech New York ; Harwat Bracea   company  Publishers

TUKI, (2004),  Kamusi ya Kiswahili Sanifu, Dar-Es-Salaam; Oxford University Press.

Wood S.K (2019), Sign Languages Structures and Contexts; Boutledge.

Comments

Popular posts from this blog

Information technology

MKATABA WA KUPANGA NYUMBA

Unominishaji,