UTANGULIZI, Fanani ni mtendaji wa kazi za za sanaa za maonesho. Vilevile fanani ni msani katika fasihi simulizi ambaye anasimulia hadithi, methali, vitendawili, anacheza ngoma na anatumia lugha kueleza dhamira ya kazi yake ya fasihi. Hivyo fanani anaweza kuwa msimulizi kama ilivyo katika ngano, mwimbaji wa nyimbo au manju katika maghani, mtegaji katika vitendawili, mpiga ngoma katika ngomezi au mlumbi katika ulumbi. Fanani aghalabu huwa msimulizi na vilevile mshiriki katika fasihi simulizi (TATAKI 2014). Mtambaji ni mtu anayesimulia hadithi au ngano. Vilevile mtambaji ni mtu mwenye tabia ya kujisifu au kwenda mwendo wa matao (TATAKI 2014). Mikakati ni mipango maalumu inayoandaliwa kwa ustadi mkubwa ili itumuke kama njia za kufikia malengo Fulani (TATAKI 2014). Kwa ujumla tunaweza kusema kuwa fanani ni mtendaji wa kazi za fasihi simulizi mbele ya hadhira yaani kama vile maonesho, masimulizi ya hadithi na kuhusisha m...