UZURI WA MJI WA KILWA
DOLA YA MRIMA (KILWA) ILIOKUWA TAIFA KUU AFRIKA KARNE
YA KUMI (1070 A.D)
Mjii wa Kilwa ni mji maarufu sana barani
afrika kwa sifa zake sio kwamba kwa sababu ya jina lake au ukarimu wa watu wake
bali ni kwa historia yaketoka zama za kale za historia ya
ulimwengu na habari za wanahistoriatokaduniani kote.
Bila shaka binafsi sina shaka kabisa na
hilii kwa sababu nilipata bahati ya kutembelea iliokuwa mijii kazaa ya Dola la
Mrima yani miji ya kilwa, Tanga( mta'nga'ta), Sadani, Kaole, Zanzibar,Mombasa
na Bagamoyo lakin pamoja na kujionea utajili wa kihistoria niliojionea sikusita
kabisa kukubaliana na historia hiyo ya Dola la Mrima lililokuwa likipatikana
pwani ya Azania na ndio Dola lililokuwa dola kuu Afrika kiuchumi, kijeshi,
kisiasa na kiteknolojia. Pia ndio dola lililokuwa na ushawishi katika ulimwengu
wa zama hizo uliokuwa ukiongozwa na Dola la Rumi na baadae Dola la Hermani
(ujerumani).
Taifa la Mrima ni Dola lililo kuwa likipatikana mashaliki ya bara la
Afrika iliokuwa pakiitwa "Azania" na ilikuwa na miji mikubwa iliokuwa
chini ya himaya ya dola hilo zaidi ya 36 kama Lamu(Amu), Mvita (mombasa),
Ofiri(Sofala), Rhapta, Mafia, Unguja na Cambula (pemba),
Ngozi(Mogadishu), Simayu(kisimayu) na makao
makuu ya dola ilikuwa Kilwa.
Historia ya utawala wa Dola la Mrima
kiutawala ilikuwa chini ya "mwinyi mkuu" (sulutani) ambaye yeye
alisaidiwa na mihimili mingine ya dola.
Pwani ya Azania ni pwani ilikuwa
inapatikana mashariki ya afrika kuanzia msumbiji ya leo mpaka Asmala(Eritria)
ya leo. Azania ni neno lenye asiri ya kiarabu yani "Ajania" ikiwa na
maana ya "isiyokuwa warabu". Historia ya mwambao huu imefahamika
tokea zama za mwanzo za mileniamu(1st millenia) katika kitabu cha "the
periplus of Arithrean sea" unaweza kupata maeelezo zaidi ya namna gani
dola ya Mrima ilivyo shamili duniani kote.
Pia wanahistoria kama Betram ThomasThomas
na M.H. Dorman ambao wote kwa pamoja wameeleza kwa pamoja namna Dola hilo
lilivyostawi sana.
CHANZO CHA DOLA LA MRIMA-665 AD
Hassani ibn Abduraufu (Mbega) ni moja ya
watu ambao historia inaowataja kuwa viongozi wa mwanzo kuanzisha dola ya Mrima.
Mbega inasadikika alikuja Azania kutokea Hijjaz na alifika mji wa mta'nga'ta
(Tanga) na aliishi hapo mpaka 665 na baadae alielekea katika milima ya Usambala
(kitabu cha zamani mpaka leo kilicho andikwa na taasisi ya utafiti wa kiswahili
1930) imejalibu kuelezea habali za mtuu huyu Mbega (Hassan ibn Abduraufu) kuwa
aliishi Nguu huko Zigua na baadaye alielekea Kilindi alipo amua kuoa Bumbuli na
baadae akawa kiongozi.
Huko "Kilindi" ilimfanya kuwa
kiongozi wao baada ya kuwasaidia wakazi wa hapo kuwaondolea tatizo sugu la
nguruwe pori kwani nguruwe hao walikuwa wanawatafuna watoto wachanga mpaka
ilipo fikia mpaka mtoto wa kiongozi wa eneo hilo alipoliwa na nguruwe ndipo
hassan ibn Abduraufu alipo fanikiwa kumaliza tatizo hilo na
Kuwafanya wenyeji kumpa jina la Mbega yani
mkombozi( leberator).
Mpaka kufikia mwaka 689 alifanikiwa
kusimamisha dola iliyojulikana kwa wakati huo kama Dola ya KILINDI. Makao makuu
ya Dola ya kilindi ilikuwa Andeni na Dola hii ilienea tokea kwenye safu ya
milima ya Usambala mpaka mombasa(mvita), Lamu(amu), mpaka Mogadishu(somalia).
Pia ilikuwa na mji mikubwa kama Saadani, Pete, Tongoni, Kaole na Rhapta. Na ilipokuwa
dola imara ilifahamika kama Dola la VEGA(Vega state) chini ya kiongozi alieitwa
Kimweri ambaye alikuwa mjukuu wa Hassan Mbega. Na taifa(Dola) hii ilikwenda
mpaka 1234 ilipo mezwa na dola jingine lililokuwa linajiimalisha (Mrima).
Dola ya Mrima ilipanuka kutokana na kile
kilichoitwa mgogoro wa "Muhawiya" uliotokea bara Arabu na kupelekea
idadi kubwa ya wageni kuhamia pwani ya Azania.
VITA YA MUHAWIYA-680 A.D-685 A.D (61-64
HIJIRIA)
Hivi ni vita iliyotokea katika imaya ya
Uthumani (OTTOMANI EMPIRE) mara baada kharipha Ally ibn Abuu Twribu kulitokea
utawala wa Banu Ummayya chini ya Muawiyya bin Abuu safiyani na baadae Yazid Bin
Muawiyya wakati wa utawala huu hasa wa Yazid ulikumbwa na vita vya wenyewe kwa
mda mrefu lakin wakati wa utawala huu ndio kipindi wakati dini ya uislam ilipo
ingia barani ulaya (Hispania) 705-715 A.D
Lakini vuguvugu la migogoro ilizidi
maradufu baina ya ukoo wa Abass kujitenga dhidi ya ukoo wa Abuu muslm ambaye
aliungwa mkono kwa kile alichodai kuwa ni utawala wa U-calipha lazima utoke
katika ukoo wa mtume muhamad (s.a.w) yani "Ahlul Bayt" lakin mwishoni
Abuu Abass alishinda vita na vita kwisha 750A.D.
Katika mgogoro hiyo ya vita idadi kubwa ya
wageni walihama bara Arabu na kuingia pwani ya Azania kupitia mji wa Asmara.
kundi hili liliongozwa na Hamza ibn Marwani aliwasili somalia na ndio chanzo
cha jamii ya (Polusa) ambaye ni miongoni mwa jamii (kabila) tatu zilizopo
Somalia leo yani Olmo, Polcano na Polusa (ukoo wa Malwani).
Kundi hili ndio lililo anzisha makazi
Asmara na mogadishu na baadae mwaka 780-900 A.D walipo anza kusogea mwambao wa
kusini mwa pwani na hatimaye badhi yao kutia makazi Kisimayu, Lamu, Galisa
katika Kenya na baadhi ya maeneo ya pwani ya Tanzania. (rejea kwenye andiko la
Feeman Granville uk 35 history of East coast of africa). ikulu ya husuni
inavyo onekana kwa sasa
DOLA YA MRIMA (KILWA) 1300 A.D
Ukipitia andiko la Walter Rodney katika
kitabu chake " Africa development before 15C" amejalibu kuandika kwa
undani namna gani dola la Mrima(kilwa) ilivyo kuwa na kuwa dola kubwa kabisa
barani Afrika hata kuzidi dola zingine za afrika kama Songhai, Mali, Benin,
Absinia na Ghana. Hii pia dola la Mrima ilikuwa kubwa mpaka dola kuu za dunia
zama hizo kama Dola ya Rumi, Dola ya Herman na Dola ya Ottoman kuitambua dola
ya Mrima kuwa ndio Dola kuu afrika. Na hata Hassan ibn Batuta alipo wasili
mwaka 1300A.D alikili kuwa
" nilipo fika kilwa nilimkuta mtawala
Wao na walinipokea kwa ukarimu mkubwa sana na walikuwa na kila kitu kama
tulivyo navyo kwetu (bara Arabu)". Hivi ndivyo kilwa ilikuwa maarufu sana.
Kwani Muundo wa utawala wa Dola ya Mrima ( kilwa) ilikuwa na muundo wa kipekee
ulioendana na mazingila ya kijografia ya wakati huo makao makuu ya dola la Mrima
ilikuwa Kaole-Bagamoyo lakin makazi ya utawala yalikuwa Kilwa kiswani mahali
ilipokuwa ikulu iliojulikana kama (Husuni) Na mtawala wake alijulikana kama
Hassan Sulyman kwa title ya Mwinyi Mkuu katika ikulu ya kilwa ndo iliokuwa
ikulu kubwa Afrika kwa wakati huo kwani ilikuwa na vyumba 100 ambavyo vilikuwa
vinatumika kama ofisi ya mwinyi mkuu na watumishi wake pia kulikuwa na idala
malumu kama idala ya...
1-Uvuvi
2-Masoko na biashara
3-Elimu
4- uchumi
Na Afya.
Katika Uvuvi ofisi zake za utendaji
ziliwekwa eneo la Mussa Hassan ( Msasani). Masoko na biashara ziliwekwa
bagamoyo(sadani). Idala ya Elimu ilikuwa Kilwa kiswani pia idala ya Afya
iilikuwa Bagamoyo na ndipo ilipojengwa kituo cha Afya cha Tumbatu(shapani) na
Makulunge kilichokuwa kikitoa tiba na kikiongozwa na Mtabibu Hamis mwinyi sembe
shomvu alie pata elimu ya tiba katika chou cha Aveccina (Iraq) ushahidi wa
habari hizi umeelezwa na Saleh Miskir toka iraq kwenye kitabu chake cha ( A
thousand and one night).
Katika Dola ya Mrima (Kilwa) kulikuwa na
bandali marufu iliokuwa katika mji wa Rhapta hapa ndipo wafanyabiashara kutoka
nje ya pwani ya Azania walifika kufanya biashara nao na pia katika uchumi dola
ya Mrima (kilwa) ilikiwa tayali imesha tengeneza pesa yake ilikiwa inatumika
katika biashara ya mabadilishano ya bidhaa na ndio dola pekee kwa wakati huo
ilikuwa imevumbua utalatibu huo barani Afrika. mfano ni Hassan Ibn Batuta
1331-1333 A.D huyu alikuwa mpelelezi, msafiri, mtaalamu na Misionari wa kiarabu
(kislam) aliefika pwan ya Azania katika karne ya 12C na alidhuru mji wa kilwa
na Rhapta katika safar yake ambaye binafisi aliueleze mji wa kilwa na dola ya
mrima kama dola kuu na kubwa iliokuwa imestalabika katika kiwango kikubwa na
kutumia sarafu ya pesa katika mfumo wa uchumi (curency economy Oriented theory)
kama sehemu ya mabadilishano ya bidhaa (rejea kitabu cha "Ibn Batuta"
uk 143-147 chapa ya Beiruti) au vitabu kama "introduction" cha
mohamed khadum, au kitabu "The incoherence for the incoherence" cha
Benmon Harph Herzre chapa ya Jerusalem. Pia mwaka 1498 alipo fika Vasco Dagama
pwani ya Azania alieleza namna Dola ya Mrima (kilwa) ivyo kuwa na nguvu.
sarafu ya Kilwa
SAFARI YA VASCO DAGAMA KUJA PWANI YA AZANIA
1497 A.D
Vasco Dagama safari yake kuja pwani ya Azania ilipelekea pakubwa na
uvumbuzi wa njia rahisi ya maji ya kufika India hii ilitokana na njia ya aridhi
kufungwa na adui yao mkubwaa wa Dola ya Othuman (Ottomani Empire) ambaye
alikuwa ametoka kushindwa kwenye vita ya msaraba (Crused War)
ya ulaya hali hii ilipelekea miliki ya
uthumani kupoteza makoloni yake ulaya kama Hispania jambo hili ilibidi mataifa
ya uraya magharibi kutafuta njia nyingine salama kwani waliofia wafanyabiashara
wake kutekwa iwapo wataendelea kutumia njia ya Constantinepoli mpaka india
kwani wakati huo consatatinepoli ilikuwa chini ya Dola ya Ottomani.
picha ya mwinyi mkuu Alli Hassan ibn
Shirazi
VITA YA MSALABA
Ni vita ilioanzishwa na Pope Urban II
katika karne ya 13 A.D na vita hivi ilikwenda awamu nne na ilipelekea nchi
nyingi zilizokuwa zinakaliwa na iliyokuwa Dola na himaya kubwa ya Uislam wakati
huu ya Othumani (Ottoman Empire) ambayo ilikuwa imekalia mataifa kazaa ulaya
kama Spain, Ugiliki, sehemu ya Ufaransa na sehemu ya kadha za ulaya ya kati
ziliweza kujipatia uhuru. Na baadae mataifa hayo huru kuluongezeka hali ya
kutokuwepo na Utengamano na kusababisha nchi hizo za ulaya kutafuta njia
mbadala ya kufika India.
Ndipo Vasco Dagama alipo tumwa kutafuta
njia nyingine na aliwasili pwani ya Azania mwaka 7/4/1497 alifika na merikebu
yake iliokuwa ikiitwa "San Raphael" mombasa na baadae Tongoni na
atimaye mji wa Kilwa. Pamoja na safari hii ya Vasco Dagama kilwa pia aliandika
kwenye andiko lake habari za Mrima ( kilwa) kilichoitwa "Sarade san
Raphael" yani 'milima ya raphael mtakatifu' inayopatika kwenye kitabu cha
Kesteloot uk 86. Ndai yake Vasco Dagama kaelezea wazi kuwa dola ya Mrima(kilwa)
ilikuwa dola kubwa na yenye pesa yake katika uchumi na utawala wake wenye
nguvu. Hali hii ilimfanya Vasco Dagama kupeleka taalifa nchini mwake Ureno
iliosababisha kuandaliwa kwa utaratibu ya utawala na uvamizi wa ureno pwani ya
Azania.
UVAMIZI NA KUANGUKA KWA DOLA YA MRIMA
(KILWA)
Kutokana na ujio wa Vasco Dagama uliopeleka
kuandaliwa utalatibu wa kupanua himaya ya Ureno ndipo Ureno ipo agiza jeshi la
uvamizi pwani ya Azania kikosi kilicho ongozwa na kamanda Fransisco D' Almenda
ambacho kilianza safari na kuwasili kilwa tarehe 22/7/1505 akiwa na merekebu 22
zilizo jaa wanajeshi 1500 na siraha za kutosha ikumbukwe kwamba safari hii ya
D' Almeida ilikuwa tayali imeshatanguliwa na ile ya mashushushu ambao walikuwa
tayali wapo mjini kilwa na tayali walikuwa wakiishi hapo mfano ni shushushu
mreno aliejulikana kama Antonio Fernandes ambaye aliishi Kilwa kwa mdaa na
kufanikiwa kuandaa wasaliti kazaa akiwemo mtu mzalendo wa kilwa aliejulikana
kama Mohamed Ankoni. (Rejea kitabu "History of Africa" uk 129-135,
Kelvin Shillington).
Kupitia ujasusi huu uliokuwa umeandaliwa na
wareno mapema ulifanikisha mpango wake wa uvamizi (rejea kitabu "history
of East Africa up to 19C. Uk 77)
1505 uvamizi ulianza katika miji mbalimbali
ya pwani ya Azania ikiwa ni sambamba na ujenzi wa ngome za Ureno mfano wa ngome
hizo ni ngome ya Ureno kilwa kiswani na Ngome ya Yesu iliopo Mombasa. Binafsi
nilipata bahati ya pekee kabisa kama ilivyo kasumba yangu ya kupenda kutembelea
(travelogy adventure) vivutio mbali mbali napokuwa ndani na nje ya nchi ili
angalau niweze kujifunza jambo (perspective analysis). Hivyo basi nilipo pata
fursa ya kutembelea mji wa Mombasa mwaka huu ilikuwa tarehe 16/1/2016 na nilifika
mahali ilipo ngome inayoitwa ngome ya yesu (Fort Jesus) mantiki ya kutoa kisa
hiki cha kuzuru mahari hapo ni kujalibu kukuonesha namna ya Dola la Mrima namna
lilivyo polomoka kwa usiku mmoja (siku chache) ukilinganisha na masiku
lilivyojengwa kwa miaka isiopungua 200. Katika safari yangu katika eneo hilo la
kihistoria mahali hapo panaofahamika kama Ngome ya Yesu (Fort Jesus) ndipo
aliekuwa mwanamakumbusho (museulogist) alipo nipa simlizi ya kusisimua na
iliyopelekea kudondoka kwa iliyokuwa dola ya Mrima (kilwa) ya pwani ya Azania.
Kwa mujibu wa maelezo ya msimulizi huyo
uvamizi huo ulikuwa na sura mbili (2) na ulifanyika kwa awamu nne (4) .
SURA YA 1
AWAMU YA I.
Ilikuwa ni mnamo mwaka 1506 ambapo jeshi la
ureno likiongozwa na kamanda fransisco D' Almeida akiwa na jeshi alivamia mji
wa kilwa mafia na baadae ZANZIBAR. Na ZANZIBAR kukawa eneo la kwanza la kireno
kuwa chini ya himaya yake chini ya capteni Ruy Lourenço Ravasço.
AWAMU YA PILI.
Awamu hii mnamo mwaka 1510 uvamizi
ulifanyika kutokea kusini yani Sofala kuja mpaka kwenye visiwa vya
"Mayote, Mororoni na Anjuani" jeshi hili liliongozwa na kapteni
Vermudezi. Kikosi hichi ndicho kilichoenda kutia nguvu baadae Mombasa.
AWAMU YA TATU.
Kikosi hiki kiliongozwa na kamanda D'
Almeida kufanya maangamizi eneo la kilwa, mafia na pemba (kamablu). Mwaka 1513
A.D
AWAMU YA NNE.
Hiki ndiko kilicho ongoza uvamizi kuanzia
Malindi, lamu, pate, kismayu, Barawa na Mogadishu. Mwaka 1509-1516 A.D
SURA YA 2
Katika sura hii ni ule vamizi wa mji wa
kilwa ambao kulitokea patashika ya mapambano. Na wanahistoria kadha pamoja na
wakazi ambao wamelithi habali toka kwa kizazi kilicho ishi hapa huelezea kuwa
baada ya uvamiz wa kilwa ndipo viongozi wa dini wakiongozwa na mtu aliefahamika
kama Hassani mwnyipembe walifanya maombi matakatifu kwa zaidi ya masaa 9 hali
iliyopelekea maajabu makubwa sana majabu hayo yapo yanaishi mpaka leo moja ya
maajabu hayo ni
1- zile merekebu zilizokuwa pale songo
mnara ziligeuka kuwa " Majabali" na mabaki ya merekebu hizo ambazo
ziligeuka kuwa majabali huonekana leo hasa ukiwa unatokea Dar es salam kuelekea
Mtwara ambapo siku hizi kumewekewa taa nyekundu ili kuwaongoza mabaharia
wasigonge miamba hiyo iliyokuwa merekebu na kugeuzwa kuwa Miamba.
2- pia kundi la wenyeji 100 ambao walikuwa
wasaliti pia wamegeuka kuwa "Vichuguu" na mpaka leo huonekana pale
msitu wa Mikoche ( mikoche historical site) pale kilwa kiswani ambapo hivyo
vichuguu 100 vinavyo aminika kuwa walikuwa wasaliti huonekana hadi leo. Na
ningependa kuwasihii kuwa iwapo utapata wasaa basi ebu tembele miji hii ikiwa
ni pamoja ha eneo hili ili ili uweze furahia wingi wa maajabu na historia hii
ambayo mimi Mbwana Allyamtu binafsi nilifarijika sana.
Lakin katika kipindi cha uvamizi huu Dola
ya Mrima ilajalibu kuomba msaada toka consatatinepoli lakin msaada haukufua
dafu kwani merikebu zao zilekuwa ndogo ukilinganisha na za wareno ambazo
walukuwa wamejipanga kiasi cha kutoshakutosha kwani mashambulizi haya yaliacha
athari kubwa na mbaya sana kama
- "vifo, uharibu wa miji na mali zao,
kuangamiza kabisa baadhi ya miji kama Rhapta ambao uliangamia na kupotea kabisa
mpaka ulipo kuja kuthibitika tena kwa mujibu wa kitabu (A Guide to Tongoni
Ruins cha A.A.Mturi) kinachosema "The ruins of Rhapta are yet to be found
though it is generally agreed tha the town was situated on Tanzania coast"
yani " mabaki ya mji wa Rhapta umeptikana tena kwa makubaliano ya pamoja
kwamba kunauwezekano mkubwa wa mji huu ulikuwa pwani ya Tanzania".
Mpaka kufika mwaka 1599 tayali ngome yote
ya Mrima (kilwa) ilikiwa tayali imekaliwa na Ureno na kuifanya ngome ya
Kiswahili ya Azania (Mrima) kuangushwa na kuwa chini ya Ureno ambapo utawala
huu ulidumu takribani kwa miaka 100 bila maasi ya kujikomboa mpaka mwaka 1698
mapambano ya kujikomboa yalipo anza tena na kuifanya Ureno kuanza kuachia
baadhi ya ngome za Mogadishu, Mombasa mpaka ZANZIBAR na kilwa na kuifanya Ureno
kuludi nyuma na kubakia Sofala- mozambiq( musa bin beq) na kuamua kujizatiti na
kujikita kiutawala huko amabapo utawala wake ulidumu kwa zaidi ya miaka 500
huko mpaka walipo kuja kuanza harakati za kujikomboa mwaka 2/6/1960 chini ya
Eduardo Mondlande nakujikomboa kabisa kuwa huru mwaka 1975 chini ya
"FRELIMO ya Samora Machel.
Watawala wa Dola ya Mrima (kilwa) kuanzia
mtawala wa kwanza mpaka mwsho pale ilipo dondoka dola ya mrima jumla walikuwa
ni "50" yani kuanzia mtawala wa kwanza Mwinyi mkuu Hassan bin
Ali.(Allyamtu) mpaka na wa mwisho (50) yani ambaye uvamizi na utawa wa kireno
ulipo shinda na kumuangusha alikuwa ni Mwinyi mkuu Said ibn Mwinyi.
MWISHO.
Naomba nitangulize shukrani zangu za dhati
kwa mwenyezi Mungu mwingi wa rehema (Allah) kwa utukufu wake kwa ulimwengu na
mbingu yote na vyoye vilivyomo ndani yake.pia na pamoja na shukurani hizo za
pekee kabisa pia naomba nipeleke shukurani zangu kwa wadau wangu wote ambao kwa
pamoja wamenipa ushilikiano wa kufanikisha kuandika Andiko hili langu kwa
kiwango kikubwa japo kwa uchache tu japo natambua kuwa ni wengi kwa idadi lakin
nyote nawashukuru kwa utukufu mkubwa kabisa ampapo mmefanya niweze
kulikamilisha jambo hili (andiko hili la nyumbani Azania) lenye mvuto na
msisimko wa pekee kabisa kwa wakati. Lakin pia naomba kuwashukuru Bwana Alfosi
wanjilu (Mombasa historical site) toka Kenya, Abdala msumbuko (Kaole historical
site) bagamoyo na bibi aisha zuberi kutoka kiliwa historical site. Ambapo kwa
pamoja mmefanya niandike makala hii kwa mvuto wa pekee kabisa kwani nimeandika
yale ambayo nimeyaishi na kuyashuhudia kutoka kwenye ziara ya kujionea na
kushuhudia historia ya miji hiyo.
Watafiti wengi na wanahistoria wengi sasa
wanakubaliana kuwa Dola ya Mrima (kilwa) kuanzia mnamo miaka ya 967 mpaka 1399
A.D ndio ilikiwa dola kubwa ukanda wa kusini wa bara la Arabu na Ulaya. Pia
ndio iliokuwa dola la 4 kwa "Ushawishi wa Dunia ya wakati Ule" ikiwa
nyuma ya Dola la Rumi (ROME EMPIRE) Dola la Sackxoni (HEREMAN EMPIRE) Dola la
Uthumani (OTTOMAN EMPIRE) na Dola la Mrima-(kilwa) (MRIMA EMPIRE) lakini
kutokana na hira au ubinafsi wa wasomi wa kizungu (Eurocentric views) kwa
makusudi wamefunika kabisa historia hii na kuifanya isaulike kabisa hata bila
soni moyoni mwao lakin pia hata nchi yetu imeshindwa kuitambua historia hii kwa
upana wake na kuifanya kuwa chanzo cha muhimili wa taifa letu la Tanzania katika
historia na uchumi. Pia kasumba hii imeathili mataifa yote yani Kenya, Somalia,
Msumbiji na hata Tanzania wote wameshindwa kuenzi historia hii ili iwe ni
urithi wa vizazi vyetu na duniani kwa ujumla kwani wenzetu Ugiliki na italia na
mataifa mengine ya ulaya wamegeuza historia kuwa ni moja ya muhimili muhimu
sana wa uchumi mfano tu kwa Ugilki kwani Ugiliki pekee huingiza Us$ 11.4
bilion( kalibu Tsh 26 Trilion) kwa mwaka kwajili ya ulithi wa tathinia nzima ya
historia.
Kwanin sis tusiwekeze kwenye hili? Natamani
sana kuendelea kuandika juu ya upembuzi yakinifu juu ya kile kinachoitwa
kuwekeza kwenye "Curiosity asset" yani vitu vyenye urithi na manufaa
ya pekee kabisa na vyenye mvuto wa hari ya juu. Hivyo basi itanibidi kwa naman
yoyote ili niishie hapa kwa maana ya kuwa nitatafuta wasaa mwingine wa
kuliandikia hili la kuwekeza kwenye "Urithi wa dunia" kwa upana wake.
Hiyo ni Ikulu ya Husuni iliyopo Kilwa.
Japokuwa kulieleza hili ni jambo la muhimu
sana itanibidi sasa niandae makala ambayo nitaishauli serekali yangu tukufu ya
Tanzania namna ya kuwekeza kwenye eneo hili ili tuweze kunufaika na historia ya
Dola la Mrima (kilwa) kupitia kwenye nyanja za kiuchumi, kisiasa, kielimu na
kifahali kama Taifa.
Sasa ningependa kuitua kalamu yangu kwa
nukuu ya Mtawa (mwasisi) wa Dola la Rumi (Roma Empire) JURIUS KAISAR alisema
" Enzi ni fahali kwa jamii kama itakukumbusha ufahali wako kwa jamii
nyingine na ukubwa wa jamii(Dola) yako kwani hukufanya uwe na sauti kwa jamii
nyingine iwapo kama utaenzi iyo hadithi kipindi ambacho hauko nayo tena huo
umiliki wako lakini utawafanya muwe mafahali kwa vizazi vingi vijavyo" 368
BC
Comments
Post a Comment