KATIBA YA UMOJA WA WANACHUO STEMMUCO
KATIBA YA UMOJA WA MWANACHUO STEMMUCO 2018
1.
JINA NA OFISI
a.
JINA.
Katiba hii imaandikwa Kwa taratibu za uanzishaji na
uendeshaji wa vikundi na itajulikana kama Kikundi cha UMOJA WA WANACHUO
STEMMUCO katika Halmashauri/Manispaa ya mtwara mikindani
b.
LUGHA
Lugha rasmi itakayo tumika katika Kikundi hiki ni
Kiswahili na kiingereza
c.
MUHURI
Kikundi hiki cha UMOJA WA WANACHUO STEMMUCO kitakuwa na
muhuri ambao utatumika katika nyaraka zote za Kikundi.
2.
SHABAHA
2.
Kuanzisha na
kuendeleza mifuko ya kukopeshana ambayo ni mfuko wa hisa, Jamii na mifuko
mingine ambayo wanachama wataridhia kuianzisha ndani ya kikundi hiki.
1. Kutoa mikopo kwa wanachama kwa masharti nafuu kama
mfumo wa vikundi unavyo eleza.
2. Kutoa mafunzo ya kina kwa wanakikundi juu ya kuweka
fedha, kukopeshana na faida ya kurejesha mikopo kwa wakati.
3. Kutoa mikopo kwa wanachama kwa riba nafuu
4. Kuondoa umaskini wa kipato kwa kuhamasiha kukopa na
kurejesha mikopo hiyo kwa wakati.
5. Kuhamsisha wanakikundi kufanya shughuli zingine za
kijamii kama vile kutunza mazingira, kuwahudumia watoto yatima, kutoa mafunzo
kwa watu wanaoishi na mambukizi ya virusi vya Ukimwi, kudumisha mahusiano ya
dini mbalimbali na kudumisha amani na upendo katika jamii.
6. Kutafuta wafadhili mbali mbali ilikuweza kusaidia maendeleo
ya wanachama wa vikundi vya VICOBA.
7. Kuanzisha na kuendeleza
shughuli yoyote ya ki-uchumi na kijamii kwa manufaa ya kikundi kama itakavyo
kubaliwa na vikundi vyote.
8. Kutoa ushauri/elimu ya
ki-uchumi, kifedha, kibiashara kilimo, ufugaji na masuala mtambuka kwa vikundi
na hata jamii inayotuzunguka.
9. Kushirikiana na vikundi vingine na kuuanzisha umoja wa
kuimarisha nguvu na ushirikiano.
10.
Kushirikiana na
makundi mengine katika kuandaa na kuendesha makongamano na maonyesho mbalimbali
ya shughuli na miradi ya wanavikundi.
SEHEMU
YA TATU
3.
MAMLAKA
Kikundi kitakuwa na malaka yote ya kisheria ya kutunza
na kulinda fedha za wanachama wa kikundi hiki na hakutakuwa na chombochochote
cha juu kitakacho kuwa na uwezo wa kumiliki au kuhodhi sehemu ya mali za
kikundi.
Kikundi kitakuwa na mamlaka ya kupokea rasilimali
halali kutoka sehemu mbalimbali ikiwemo hisa za wanachama, mfuko wa jamii, bima
za mikopo pamoja na riba za mikopo.
Kikundi kitakuwa na mamlaka ya kuwekeza kwenye
kitegauchumi chochote na fedha za kuwekeza zitatokana na michango maalumu
kutoka kwa wanachama na makusanyo ya kila wiki ambayo ni Hisa na mfuko wa Jamii
hazitahusika katika uwekezeji maana ni fedha za mwanakikundi na atatakiwa
kurejeshewa pindi atakapo jitoa.
Kikundi pia kitakuwa na mamlaka ya kupokea msaada wa
kifedha, kuingia kwenye makubaliano yoyote ya kukopeshwa au kukopa au kupata
msaada kwa kuzingatia kwamba:
a.
Msaada au mchango
wowote ndani ya Kikundi hiki utatumika kwa manufaa ya wanaKikundi tu.
b.
Hakuna fedha
zozote au rasilimali zitatumiaka kwa maslahi ya mtu binafsi
c.
Kufanya shughuli
za maendeleo kwa manufaa ya wanachama
d.
Kutoa elimu
katika jamii kwa faida ya wanachama na wananchi kwa ujumla.
SEHEMU YA NNE
4.
WANACHAMA
Wanachama wa UMOJA
WA WANACHUO STEMMUCO ni watu waliojiunga katika kikundi hiki na ambao
watakuwa na jukumu la kufanya shughuli zao zote kwa kufuata kanuni na taratibu
za mfumo wa kikundi.
4.1.
SIFA ZA MWANACHAMA
4.1.1. Awe mwenye umri usio pungua 18+
4.1.2. Awe mwenye tabia nzuri mwaminifu na akili timamu.
4.1.3. Awe mwenye uwezo wa kununua hisa angalau moja kila
wiki na mwenye uwezo wa kuudhuria mikutano kila wiki
4.1.4. Awe tayari kufuata sheria na kanuni za kikundi hiki
4.1.5. Awe mwenye uwezo wa kusimamia mradi wake kikamilifu
4.1.6. Awe anahudhuria kila mwisho wa mwezi
4.2.
MAOMBI YA UANACHAMA
4.2.1. Kila mtu atakaye hitaji kujiunga na kikundi hiki cha umoja wa wanachuo stemmuco atatakiwa kuandika barua ya kuomba kujiunga
na kuwasilishwa kwa mwenyekiti wa kikundi.
4.2.2.
Baada ya maombi
kuwasilishwa katika Kikundi, Barua itasomwa na kujadiliwa na wanakikundi wote na
mhusika atapewa taarifa kama amekubaliwa au maombi yake yamekatataliwa na
sababu zake.
4.2.3.
Mwenyekiti
atamjulisha mhusika na kama atakubaliwa atatakiwa kulipia fedha za kujiunga
ndani ya mwezi mmoja tu.
4.2.4.
Mwanachama
atakayetaka kujiunga atalipia gharama zote za toka chama kimeanza.
4.3.
HAKI ZA
MWANAKIKUNDI
4.3.1.
Kushiriki katika
shughuli zote za Kikundi kwa kufuata kanuni na taratibu za Kikundi hii.
4.3.2.
Kuhudhuria na
kutoa maoni yake katika mikutano ya Kikundi.
4.3.3.
Kuchagua au
kuchaguliwa kuwa kiongozi katika Kikundi hiki
4.3.4.
Kumkataa
mwanakikundi anaye taka kujiunga kwa sababu za msingi ambazo atazieleza na
zitakazo wasilishwa kwenye mkutano.
4.3.5.
Kushiriki kwenye
mikutano yote ya mwaka
4.3.6.
Kushiriki kwenye
shughuli na matukio mbalimbali yatakayo andaliwa na Kikundi hiki.
4.3.7. Mwanachama anahaki ya kujitoa ambapo atarejeshewa 5%
ya uanachama wake
4.3.8.
4.4.
WAJIBU WA MWANAKIKUNDI
4.4.1.
Kulipa kiingilio,
kununua hisa kila mwezi, kuchangia mfuko wa jamii kila mwezi, kulipa bima kila
anapochukua mkopo, kumdhamini mwanakikundi mwenzake wakati wa kukopa na kulipa
deni la mkopaji iwapo atashindwa kulilipa kwa wakati na kwa mujibu wa taratibu
za kikundi.
4.4.2. Kupewa ripoti ya maendeleo ya Kikundi kila mwezi na
kila wiki kusoma majina ya wanakikundi wanaotakiwa kurejesha mikopo yao.
4.4.3. Kushiriki, kusimamia na kuendesha warsha mbalimbali
kwa niaba ya wanakikundi, na wananchi kwa ujumla.
4.4.4. Kuchukua mikopo na kuirejesha kwa muda wa kati ya
miezi mitatu, miezi sita na mwaka mmoja.
4.4.5. Kuhakikisha analipa kiasi cha fedha kila mwezi kama
ambavyo mfumo wa kikundi unaelekeza nah ii itwasaidia wengine nao wapate mikopo
kwa wakati.
4.1.
UKOMO WA MWANAKIKUNDI
4.1.1. Mwanachama yeyote atakaye hitaji kujiondoa atatakiwa
kuandika barua kwa mwenyekiti wa kikundi na mwenyekiti ataisoma kwa wanacahama
na kuomba mawazo yao.
4.1.2.
Mwanachama yeyote
atakaye shindwa kutimiza kanuni, taratibu na katiba au aliyeshindwa kulipa
michango yake kama wanachama walivyo kubaliana mwanachama huyo atakuwa
amejiondoa mwenyewe na mafao yake atapewa ndani ya siku tisini na iwapo
anadaiwa kikundi kitapanga utaratibu kwa kushirikiana na wadhamini wake jinsi
ya kulilipa deni lake.
4.1.3.
Mwanachama
atakaye fariki au kujiondoa atapewa mafao yake ndani ya siku tisini (90) na
ambayo ni Hisa na mfuko wa jamii ambazo ni 50%.
4.1.4.
Mwanachama
atakaye fukuzwa ndani ya kikundi hiki kutokana na wizi, kutoa siri za kikundi,
kusababisha ugonvi, ubishi wa mara kwa mara, kutofuata sheria na kutohudhuria
mara nne mfululizo kwenye vikao vya kikundi atakatwa asilimia 20 ya mafao yake
kama adhabu na mafao yatakayo salia atakabidhiwa ndani ya siku tisini.
4.1.5.
Mwanachama
atakaye kiuka kanuani na taratibu za mfumo wa kikundi kwa kwenda kinyume na
mwongozo unaotumika atakuwa amejiondoa.
4.1.6.
Mwanakikundi
atakaye ugua zaidi ya miezi sita kitandani atarudishiwa hisa zake na nafasi
yake itaachwa wazi hadi mwishoni mwa mwaka wa kikundi. Kama hali yake itaimarika na atapenda
kujiunga tena basi mwanakikundi huyo ataruhusiwa.
4.1.7.
Mwanachana atapomaliza chuo atapata michango yote aliyetoa na faida itakuwa kama
sehemu ya mtaji wake
4.5.
KUTEUA MRITHI
4.5.1.
Kila mwanakikundi
atamteua mrithi wake ambaye atakuwa na haki ya kulipwa hisa na mafao yote anayo
stahili.
4.5.2.
Mwananakikundi anayo
haki ya kubadilisha jina la mrithi kila mwaka na kila uteuzi utaandikwa katika
daftari la wanachama na mwanachama mwenyewe ataweka sahihi.
SEHEMU YA TANO
5.
MUUNDO WA UONGOZI NA MAJUKUMU YAKE
a.
Mkutano mkuu
b.
Kamati ya uongozi
5.1.
MKUTANO MKUU
Mkutano mkuu utahudhuriwa na wanachama wote na ambao
wanashiriki kwenye shughuli za kikundi na wanazifuata taratibu na kanuni ambazo
wamejipangia ilikuwaongoza.
Kutakuwa na kamati ya uongozi ya kikundi ambayo
itakuwa na wajumbe watano. Wajumbe hawa ni Mwenyekiti, Katibu, Mweka hazina na
Wahesabu fedha wawili. Majukumu yao ni kuongoza kikundi kila siku na kama
hawatakuwepo siku ya kikao mwanachama yeyote atateuliwa kushika nafasi iliyo
achwa wazi na atasimamia mambo yote na kikao hicho kitatambulika kuwa ni kikao
rasmi na halali.
5.2.
MAJUKUMU YA MKUTANO MKUU
5.2.1.
Kuchagua kamati
ya uongozi
5.2.2.
Kupitia na
kupitisha mipiango ya Kikundi
5.2.3.
Kupitia na
kukubaliana juu ya mapendekezo ya maboresho au mabadiliko ya katiba.
5.2.4.
Chombo cha
usulihishi zidi ya mambo yote yatakayojitokeza ndani ya Kikundi
5.2.5.
Kutoa ushaari na
maelekezo kwa kamati ya uongozi ya kikundi
5.2.6.
Kushughurikia
masuala mengine yote yanayo husu kikundi hiki.
5.3.
KAMATI YA UONGOZI
Kamati ya uongozi wa kikundi itaundwa na viongozi
watano na ambao ni Mwenyekiti, Katibu, Mwekahazina na Wahesabu fedha wawili.
Majukumu yao ni kama ifuatavyo:
5.3.1. MWENYEKITI
5.3.1.1.
Kuongoza kikundi
5.3.1.2.
Kuwakilisha
kikundi kwa watu wa nje na wasio wanakikundi
5.3.1.3.
Kuhakikisha sheria
za kikundi zinafuatwa nakuheshimiwa
5.3.1.4.
Kuwashauri
wanakikundi
5.3.1.5.
Kutafuta suluhisho la ugomvi miongoni mwa wanakikundi
5.3.1.6.
Kuhitimisha
mikutano
5.3.1.7.
Kufungua mikutano
na kutangaza agenda
5.3.1.8.
Kutangaza makusanyo yaliyo pita (uwekaji fedha) na baadae
kutoa mikopo.
5.3.1.9.
Kuhakikisha usalama wa mali zote za kikundi.
5.3.1.10.
Kushirikiana na wajumbe wengine wa kamati ya uongozi
kulipa mali pale inapobainika kuwa wao ndio wahusika wa upotevu wa mali hizo.
5.3.2.
KATIBU
5.3.2.1.
Kuandika na
kukumbuka shughuli zote zinazofanywa na kikundi katika kila mkutano.
5.3.2.2.
Kuita namba ya wanakikundi
wakati wa kununua hisa, uwekaji wa mfuko wa jamii na urejeshaji wa mikopo.
5.3.2.3.
Kutoa taarifa na shughuli za kikundi kwa mwezeshaji wakati
wa ufuatiliaji.
5.3.2.4.
Kulipa fedha zinazo potea ikibainika kuwa kamati ya
uongozi wa kikundi imehusika.
5.3.3. MWEKAHAZINA
5.3.3.1.
Kuweka fedha za
kikundi
5.3.3.2.
Kuhakikisha usalama wa fedha na mali za kikundi
5.3.3.3.
Kutayarisha mahesabu katika sanduku la fedha na kusimamia
mienendo yote ya shughuli za kibenki.
5.3.3.4.
Kuhakikisha sanduku limefungwa baada ya mkutano wa
kikundi
5.3.3.5.
Kuhakikisha
marejesho yanatolewa.
5.3.3.6.
Kutunza
kumbukumbu zote za fedha za kikundi
5.3.3.7.
Kugonga mihuri na kujaza reja ya mikopo kila wiki.
5.3.3.8.
Kutoa taarifa ya mapato na matumizi mwisho wa kufunga
mwaka wa kikundi.
5.3.3.9.
Kulipa fedha zinazo potea ikibainika kuwa kamati ya
uongozi wa kikundi imehusika.
SEHEMU YA SITA
6.
VYANZO VYA MAPATO NA MIFUKO MIKUBWA
a.
VYANZO VYA MAPATO
6.a.1.
Michango
kutoka kwa wanachama wa Kikundi kwa kulipa kiingilio, Hisa za kila wiki, ruzuku
kutoka kwa wafadhili mbalimbali, michango kutoka kwa marafiki na harambee
mbalimbali.
6.a.2.
Kupata
michango au misaada kutoka kwa watu wasio watanzania.
6.a.3.
Misaada na
michango mbalimbali kutoka katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
na mashirika rafiki.
6.a.4.
Kuuza
rasilimali za Kikundi.
6.a.5.
Kupata fedha
kutokana na ushauri na mafunzo mbalimbali yatakayo tolewa.
b.
HISA
6.b.1. Thamani ya hisa moja ni
shilingi 5,000/= Kiwango hiki kitakuwa kinabadilika kila mwaka kutokana na
maendeleo ya wanachama wa kikundi.
6.b.2. Hisa ni mali ya
mwanachama kwa hiyo hairuhusiwi kuchukua hisa za wanachama kununulia rasilimali
za kikundi.
6.b.3. Idadi ya chini ya hisa ni
moja na idadi ya juu ni hisa tano kila wiki
ya mkutano wa kikundi.
6.b.4. Kila mwanachama atapewa
kitabu cha hisa (excell sheet) na kuingizwa kwenye reja.
6.b.5. Faida ya kikundi
itakayopatikana kutokana na mikopo itakayochukuliwa itagawanywa kwa wanachama
kulingana na idadi ya hisa za wanachama. Mwanachama atakaye nunua hisa nyingi
atakuwa na faida kubwa na atakaye nunua hisa chache atapata na faida ndogo.
6.b.6. Iwapo mwanachama ana
mkopo, hisa zake hazitaruhusiwa kuchukuliwa hadi amalize deni lake au la
mwanachama aliye mdhamini ndani ya kikundi.
6.b.7. Mwanachama ambaye
hatanunua hisa katika kikundi atatakiwa kulipa faini sh 2000/=
6.b.8. Vitabu vya hisa vitakuwa
na namba zinazo fuatana na mwanachama atajulikana kwa namba katika Leja ya
kikundi.
6.b.9. Fedha zitakozowekwa
kwenye kikundi zitaletwa na mwanachama husika au mwanachama mwenzake. Mtu
ambaye siyo mwanachama hataruhusiwa kushiriki kwenye zoezi la kibenki ndani ya
kikundi
6.b.10.
Kitabu cha hisa
hakina budi kionyeshwe wakati wote wa kununua hisa au wakati wa kuchukua mkopo.
6.b.11.
Mkopo utatolewa
mara tatu tatu ya hisa za mwanachana lakini kwa kuangalia idadi ya wakopaji
mwezi huo na fedha zilizopo na uhitaji wa mwanachama.
c.
BIMA YA MIKOPO YA KIKUNDI
Kila mwanacha atatakiwa
kutoa 2% ya mkopo wake ilikuukinga mkopo wake dhidi ya janga la Kifo au ulemavu
wa kudumu. Mfuko huu utakuwa na jukumu la kuhudumia janga litakalotokea baada
ya mwanachama kukopa mkopo wa kuendeshea biashara/mradi.
Mwanachama akifariki au
kupata ulemavu wa kudumu ambao utamfanya asiweze kuendelea na shughuli za
kikundi, deni lake litafidiwa na mfuko bima ya kikundi na malimbikizo yake ya
Hisa na mfuko wa jamii atakabithiwa mrithi wake.
Mwanakikundi akijitoa
hatarejeshewa mfuko wa bima kwa kuwa mfuko huu utaendelea kulinda madeni miaka
hadi miaka na iwapo kikundi kitavunjika basi mfuko wa Bima atachanganywa na ziada
ya mikopo na kugawanywa kama gawio kwa wanahisa wote.
d.
MFUKO WA JAMII
Kila mwanachama
atachangia shilingi 5,000/= kwa ajili ya mfuko wa jamii na ambao utatoa mikopo
ya sherehe,kufiwa na afya. Mfuko huu utakopeshwa kwa wanachama kutokana na matatizo ya
afya pamoja na matatizo ya elimu. Mfuko huu utakopeshwa kwa muda wa miezi
mitatu na mkopaji atarudisha mkopo huo bila ziada/riba ya mkopo kwenye kikundi
chake kila mwezi.
Kikundi kitapanga kiwanga cha juu cha kukopeshana na kiwango hiki kitakuwa
kina badilika miaka hadi miaka kutokana na kukua kwa mfuko wenyewe au
kuongezeka kwa michango ya kila wiki. Mfuko huu ni mali ya wanachama na iwapo
mwanachama atajiondoa katika kikundi fedha zote alizochangia katika mfuko huu
atarejeshewa pamoja na mfuko wa Hisa.
SEHEMU
YA SABA
7.
AKAUNTI NA VITABU VYA FEDHA
7.1.
Fedha zote
zitakazo pokelewa na kikundi zitahifadhiwa kutokana na mfumo wa kikundi unavyo
eleza na kikundi kitakuwa na akaunti katika benki.
7.2.
Fedha zote za
Kikundi hiki zitatumika katika kukopesha wanachama, kusaidia katika matatizo ya
dhararu na kuwarudishia wanachama hisa zao wote ambao wamajitoa katika kikundi.
7.3.
Fedha zote
zitakazo pokelewa na kutolewa zitakuwa zinaingizwa kwenye excel sheet.
7.4.
Mwezeshaji
atashirikishwa kwenye jambo lolote litakalo fanyika ndani ya kikundi hasa kwa
ushauri na hii itatokea kutokana na uelewa wake mpana wa uendeshaji wa vikundi
hivi vya kikundi.
7.5.
Fedha zote
zitakazo potea wahusika watawajibika kuzilipa kutokana na mazingira ya wizi ulivyojitokeza.
7.6.
Mwaka wa fedha wa
kikundi hiki utakuwa ni mwezi Semptemba, tarehe 30 ambapo wanachama watagawana
faida na kufanya tafrija ndogo ya kupongezana jumapili ya mwisho wa mwezi
september.
7.7.
Kikundi kitaweka
kumbukumbu zote za fedha ikiwemo ripoti za fedha na za miradi na kuwasilishwa
kwa wanachama kila mwisho wa mwaka wa fedha.
7.8.
Akaunti ya kikundi
itafunguliwa na wajumbe watatu. Kati ya wajumbe hawa wajumbe wawili
wataruhusiwa kutoa fedha za kikundi baada ya kupitishwa katika kikao na
wanachama kuidhinisha utoaji wa fedha hizo za kikundi.
SEHEMU
YA NANE
8.
KUVUNJIKA KWA
KIKUNDI
8.1.
Kikundi hii kinaweza
kunvunjwa kwenye mkutano mkuu wa wanachama wote iwapo theluthi mbili ya
wanachama wakipiga kura.
8.2.
Wakati wa
kuvunjwa rasilimali zote ikiwemo mali na fedha zitagawanywa kwa kila mwanachama
kama alivyo changia na zitakzo baki zitagawiwa kama gawio la faida.
SEHEMU
YA TISA
9.
MABADILIKO YA KATIBA
a.
Baada ya
katiba hii kukubalika na kupata usajili wa kisheria hakuna mwenye ruhusa ya
kubadilisha katiba hii bila idhini ya wanachama wa kikundi hiki.
b.
Mabadiliko
yoyote yatakayotakiwa kufanyika katika katiba hii kamati ya uongozi wa kikundi
itayawasilisha kwenye ofisi ya maendelo ya wilaya.
c.
Maboresho
yakikubalika wajumbe watatakiwa kupiga Kura na thelusi mbili wakikubali basi
katiba hiyo itatakiwa kufanyiwa maboresho.
SEHEMU
YA KUMI
10.
MAKOSA MBALIMBALI NA ADHABU ZAKE.
10.1. Mwanachama atakaye ongea ndani ya mkutano bila ruhusa
ya mwenyekiti atatozwa faini ya TSH 2,000/= Na kiwango kitapangwa na kikundi na
kitakuwa kinabadilika mara kwa mara.
10.2. Mwanachama ambaye simu
yake itaita kwa sauti na kusababisha kuharibu kwa mazingira ya utulivu atalipa
faini ya tsh 2,000/= na kiwango kitakuwa
kinabadilika mara kwa mara.
10.3. Mwanachama atakaye
chelewa kufika kwenye mkutano wa kikundi kama ilivyo kubaliwa na wanachama wote
bila taarifa atatozwa faini ya Tsh
5,000/= ili kulinda nidhamu na kuhakikisha shughuli za kikundi zinafanyika kwa
muda uliopangwa,kutohudhuria bila tarifa 10,000/=,tsh 2,000/= kama ametoa
taarifa
Michango mbalimbali
10.4. Mwanakikundi atakaye
fariki dunia katika kikundi cha UMOJA WA WANACHUO STEMMUCO atachangiwa kwa kadiri wanachama
watakavyokubaliana. Fedha hizo atakabidhiwa mrithi wake wake pamoja na mafao
mengine ambayo ni Hisa na jamii.
10.5. Mwanachama yeyote atakeye
fiwa na Mume, mke na watoto/tegemezi
wake kama alivyoandikia majina yao katika daftari la tegemezi atachangiwa na kila
mwanachama wa kikundi hiki.
10.6. Michango mingine ni
katika sherehe ambazo ni ndoa, harusi, sendoff, kitchen party, graduation,
ubatizo, vipaimara na komuniyo.
NB :
TAFSIRI:
2.1
|
Umoja wa wanachama ambao wana lengo moja, wameamua na wako tayari
kuwa pamoja kwenye maswala mbalimbali ya maendeleo. Ni chombo huru na cha hiari chini ya sheria
na taratibu za nchi.
|
Association
|
|
|
|
2.2
|
Uongozi uliochaguliwa kukiongoza chama na mkutano wa wanachama
kwenye Mkutano Mkuu na wanachama wote wa Association.
|
Kamati
|
|
|
|
2.3
|
Mkusanyiko wa wanachama wote wa Association kwa uwiano utakaotokana
na makubaliano ya pamoja katika Association kutokana na idadi ya wanachama
katika maeneo ya uwakilishi.
|
Mkutano
Mkuu
|
|
|
|
2.4
|
Mwanachama mmoja mmoja ambaye amelipa kiingilio kwa mujibu wa
makubaliano ya wana Association wote.
|
Mwanachama
|
2.5
|
Maswala na mahitaji ya msingi yanayogusa wanachama kama msingi wa
uanzishaji wa Association kwa niaba na ridhaa ya wanachama wenyewe au yanayohitaji
msaada wa pamoja wa Association
|
Huduma
|
2.6
|
Akiba ni fedha anayoweka mwana Association kwenye mfuko wa pamoja na
ni fedha inayomsaidia mwana Association/ chama kujipatia mkopo pale ambapo
association itaamua kutoa huduma ya mikopo.
|
Akiba
|
2.7
|
Ada ni fedha inayotolewa na mwanachama kila mwezi ili aweze
kutambulika kama mwanachama hai.
|
Ada
|
2.8
|
Hisa ni umiliki wa sehemu ya investment ( ) inayofanywa na
Association au biashara yoyote inayofanywa ndani ya association.
|
Hisa
|
2.9
|
Mwanachama hai ni yule aliyelipa kiingilio na anatoa ada kila mwezi
na kulipa michango mingine na kushiriki kikamilifu kwenye shughuli
zilizowekwa kwa makubaliano ya zaidi ya ½ ya wanachama wote.
|
Mwanachamai
hai
|
Comments
Post a Comment