Dhana ya kategoria ya kileksika; imejadiliwa kwa namna tofauti tofauti:- Khamisi na Kiongo (2002); wamegawa kategoria katika mitazamo miwili ambayo ni:- mtazamo wanamapokeo na wanausasa, ambapo wanamapokeo walitumia dhana ya kategoria ya kileksika kumaanisha sifa bainifu ya vitu na wanausasa wanaona kategoria kuwa ni zile aina za maneno kama vile nomino, kivumishi, vielezi, viunganishi, vihusishi na vitenzi. Massamba (2009), anatoa maana ya kategoria ya kilekisika kwa kusema kuwa ni jumla ya maumbo, faridi au vipashio vingine ambavyo huchangia sifa fulani au ambavyo viko katika kiwango kimoja. Maana hii ni ya jumla kwani imeeleza dhana ya kategoria ya kileksika kwa ujumla bila kujikita katika kategoria za miundo ambayo ndiyo sintaksia. Kategoria za kileksika katka lugha ya kiswahili zipo kategoria nane za kileksika ambazo ni nomino, vitenzi, viwakilishi, vielezi, viunganishi, vivumishi, vihusishi na vihisishi. Kwamjibu wa Massamba, Kiho...
Comments
Post a Comment