Kwa mujibu wa wanaisimu wa kiswahili Masamba
UTANGULIZI
Masamba (2001) akimnukuu Lyons (1978) Anasema kuwa
kishazi ni kundi la maneno lenye kiima na kiarifu hasa likiwa ndani ya sentensi
.Au Vishazi ni
tungo yenye kitenzi ambacho chaweza kujitosheleza na kukamilisha ujumbe uliokusudiwa
na mzungumzaji au kuwa na kitenzi kisichoweza kujitegemea chenyewe . Kuna aina
mbili za vishazi yaani viishazi tegemezi na vishazi huru. masamba na wenzie (2001)
anasema kuwa sentensi ni kipashio kikubwa chenye maana kamili. Sentensi
imeanishwa kwa kuzingitia umuundo na kimaana. Kwenye muundo Kuna aina tatu za
sentensi yaani ni sentensi sahili, sentensi changamano, sentensi ambatano. Na upande wa kimaana Kuna sita za sentensi yaani
sentensi taarifa, sentensi ulizi, sentesi shurutia, sentensi mshangao, sentensi
yakinishi na sentensi kanushi.
Kwa mujibu wa wanaisimu
wa kiswahili Masamba (2001),
Nkwera (2013), Matinde (2012) , Kapinga (1983), Masebo (2012) ,waanathitisha kuwa ni kweri
kwamba kishazi ni sentensi lakini sentensi sio kishazi kwa kuonesha utofauti uliopo
baina ya sentensi na kiashazi kwa hoja zifuatazo;
Masamba ( 2001)
.Anasema kuwa kishazi na sentesi utofautiana katika maana zake, yaani kishazi ni tungo yenye kitenzi ambacho
chaweza kujitosheleza na kukamisha ujumbe uliokusudiwa na mzungumzaji au kuwa
na kitenzi kisichoweza kujitegemea chenyewe.
Kwa mfano I) Mzee analima.
II)Mzee
aliyekuja Jana.
tofauti za vishazi( I) na( II) hapo juu ni kwamba
kishazi( I) kina kitenzi kinachojitosheleza chenyewe kwani kina kamilisha
ujumbe. Kwakuwa sentensi (II) hakijajitosheza kimaana kwa sababu kina utegemezi
wa vipashio vingine ili kuleta maana. Wakati sentensi ni kifungu Cha maneno
kuanzia neno moja na kuendelea chenye muundo wa kiima na kiarifu na kinacholeta
maaana kamili.
Matinde
(2012). Anasema kuwa tofauti nyingine
ipo katika aina zake ,kwa maana kuwa kiashazi kina aina mbili yani kishazi huru
hii no aina ya vishazi ambavyo vimeunganishwa katika sentensi na viunganishi
hasa viunganishi huru kama vile na /
lakini na kishazi tegemezibni aina ya vishazi ambavyo vikidondoshwa katika
muktadha was sentensi kuu having kusimama peke ake Kama sentensi vinavyo
jitegemea. Wakati sentensi
Kuna aina tatu za sentensi kimuundo yaani sentesi sahili, sentensi changamano, na
sentensi ambatano.
Nkwera (2013). Sentensi sharti ilete maana kamili kwa maana
kuwa iwe inaonyesha lengo lililokusudiwa .
Kwa
mfano; juma anasoma kitabu Cha hadithi.
Mama na baba wanalima.
Hivyo inaonesha tendo linalofanywa ,lililofanywa au
litakalofanyika. Lakini kishazi sio
lazma kuleta maaana kamili kwa sababu kuna kishazi tegemezi na sifa kuu ya
kishazi tegemezi kuwa hakitoi maana iliyo kamili.
Kwa mfano; mbuzi
aliyepotea jana......
Japokuwa anasinzia ovyo.......
Hivyo kishazi tegemezi ili kiweze kutoa maana lazima
kiunganishwe na vipashio vingine ili kukamilisha maana.
Masamba
na wenzake (1999). Sentensi huonesha
hali na kauli mbalimbali. lakini si kila kishazi kuonesha hali na kauli. Kwa
mfano tunapozungumzia kauli ina maana
kuwa ni ule uhusiano uliopo baina ya, ama kitenzi na kiima au kitenzi kiima na
yambwa.katika sentensi kuna kauli mbalimbali Kama vile kauli ya kutenda, kutendwa, kutendeka,
kutendana ,kutendea na kujirejerea.
Masebo
( 2012). Anasema kuwa Sentensi ina kiima
na kiarifu. Yaani kiima nisehemu ya sentensi ambayo imetawaliwa na nomino na
kiarifu ni sehemu ya sentensi ambayo imetawaliwa na kitenzi.
Kwan mfano; Juma
/anapika ugali.
K A
Baba na mama/ wanasoma kitabu.
K A
lakini kishazi si lazma kiwe na muundo wa kiima na
kiarifu .
Kwa mfano;
Angekuja jana angeondoka leo.
Kama atakuja atakukuta
hapa .
Kapinga
, M. C . (1983). Amethibitisha kuwa
utofauti upo katika muundo , sentensi kuwa na muundo wa kitenzi peke ake ambao
umebeba viambishi vinavyo wakilisha vipashio vingine kama vile kiwakilishi Cha
kirai nomino au kiima. Mahususi miundo kama hi nikwamba haioneshi virai nomino
hasa katika nafasi ya kiima.
Kwa mfano
Kiswahili kingereza
Anakuja He/she is coming.
Tunakula we are eating.
kishazi
inamuundo unaojikita katika viambishi, vishazi hivi kujidhihirisha kuwepo kwa
viambishi ndani ya muundo wake.
Kwa mfano; Angelala mapema
angeliwahi kuamka.
Masamba
(2001). Sentensi kuweza kuwa na
upatanisho wa kisarufi, lakini kishazi
hakiwezi kuwa na upatanisho wa kisarufi
Kwa mfano; kijiko kidogo
kimepotea.(umoja)
Vijiko vidogo kimepotea.(uwingi)
mtoto amepotea. (umoja)
watoto wamepotea.(uwingi)
HITIMISHO
Hivyo basi ukweli kwamba kishazi ni sentensi lakini sentensi sio kishazi kwa
maana kuwa kishazi ni sehemu ya sentensi kuu, hii in maana kuwa bila ya kuwepo
kwa miktadha ya sentensi kuu iliyokibeba kishazi huwa no sentensi
inayojitegemea.
MAREJEREO
Kaipinga, M. C. (1983).Sarufi Maumbo ya Kiswahili Sanifu (SAMAKISA). Dar es Salam:TUKI.
Masamba,D.T. Kihora,M. Y. & Hokororo (1999). Sarufi Miundo ya Kiswahili (SAMIKIRA).
Dar
es Salam ; TUKI.
Massamba na wenzake ,( 2012). Sarufi ya Kiswahili Sanifu
Sekondari na Vyuo. Dar
es Salam.
Matinde, S. R.(2012) Dafina ya lugha Isimu na Nadharia. Mwanza: Serengeti Educational
publishers
(T) LTD.
Comments
Post a Comment