semantiki ni msingi wa taaluma nyingine za isimu”Thibitisha kauli hi kwa mifano bayana ya kiswahili.

 

 

 CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA STELLA MARIS MTWARA

(Chuo Kishiriki cha Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino - Tanzania)

Maelelzo: Maelelzo: E:\Users\mwanafunzi\Pictures\index.jpg

KITIVO CHA ELIMU NA SAYANSI

 

IDARA:                                                 ELIMU

KITENGO:                                            KISWAHILI

MSIMBO WA KOZI:                            SW 323

JINA LA KOZI                                     SEMANTIKI YA KISWAHILI

MHADHIRI:                                         HAONGA, E

AINA YA KAZI:                                   KAZI YA KIKUNDI

TAREHE YA KUWASILISHA:          03/05/2021

WASHIRIKI:

NAMBA

 MAJINA

NAMBA ZA USAJILI

SAHIHI

 1

MONICA ZAKARIA

STE/BAED/164093

 

 2

LILIAN M COSTA

STE/BAED/164229

 

 3

JUDITH J KOMBA

STE/BAED/165199

 

 4

AILEN A MUGANDA

STE/BAED/164460

 

 5

GASPA D SINKALA

STE/BAED/165206

 

 

SWALI: “semantiki ni msingi wa taaluma nyingine za isimu”Thibitisha kauli hi kwa mifano bayana ya kiswahili.

 

Kazi hii imegawanyika katika sehemu kuu tatu, sehemu ya kwanza ni utangulizi kuuleza dhana ya semantiki kwa mujibu wa wataalamu mbali mbali, sehemu ya pili ni kiini cha kazi kuueleza umusingi wa semantiki kwa matawi mengine na sehemu ya tatu ni hitimisho la kazi kwa ujumla.

Massamba (2004:75) anafasili dhana ya semantiki kuwa ni taaluma ya isimu inayojishughulisha na uchunguzi na uchambuzi wa maana za maneno na tungo katika lugha. Semantiki imegawanyika katika makundi manne ambayo ni leksika, mantiki, muundo na nadharia.

hata hivyo hakuna ufafanuzi wa kutosha kuhusu maana ingawa katika hali ya kawaida tunaishia kutoa sifa za kitu na siyo maana.

Kwa mujibu wa Crystal, D (1987) semantiki ni utanzu wa isimu unaochunguza maana katika lugha. Kwa mukhtasari, semantiki hutalii maana katika vipashio vyote vya kiisimu katika viwango vyote vya lugha mathalan fonolojia, mofolojia na sintakisia.

Aidha, semantiki inaweza kufasiliwa kwa namna mbalimbali jinsi ifuatavyo:

Maana anuwai za dhana ya semantiki

1.      Semantiki ni stadi ya maana

2.      Semantiki ni utanzu wa isimu unaongalia maana ya maana.

Kwa mujibu wa  Leech (1981). Semantiki ni taaluma katika isimu ambayo hushughulikia maana ya maumbo au sentensi katika lugha. Taaluma hii ilianza enzi za Aristotle na Plato ambao walizingatia zaidi sifa za maana, katika kipindi hicho walitaka kujua sifa na tabia za maana.

Habwe na Karanja wakimnukuu Richard na Wenzake (1985) wanasema “Semantiki ni stadi ya maana. Semantiki ni utanzu unaochunguza maana katika lugha ya mwandamu”. Wanaendelea kusema semantiki hutafiti maana za fonimu, mofimu, maneno na tungo. Hivyo kutokana na fasili hii maana hushughulikiwa katika vitengo au viwango vyote vya lugha ambavyo ni fonolojia, mofolojia na sintaksia.

Hivyo maana zilizotolewa na wataalamu hapo juu Zina upungufu.

 Wanaeleza maana ya semantiki bila kuzingatia viwango vinavyokamilisha lugha Kama vile maana kiwango Cha neno , kiwango Cha tungo,na matini nzima.

Hivyo kutokana na maana zilizotolewa na wataalamu mbali mbali hapo juu wanakundi tumetoa maana ya semantiki kuwa,

Semantiki.ni utanzu wa isimu ambao unajishugulisha na uchunguzi,uchambuzi na kutafiti maana za lugha ya binadamu kutoka kiwango Cha neno mpaka kiwango Cha tungo na matini nzima.

Hivyo  kwa ujumla  Semantiki ni taaluma katika isimu ambayo hushughulikia maana ya maumbo au sentensi katika lugha. Taaluma hii ilianza enzi za Aristotle na Plato ambao walizingatia zaidi sifa za maana, katika kipindi hicho walitaka kujua sifa na tabia za maana. Hii inamaanisha kwamba semantiki hutalii maana katika vipashio vyote vya kiisimu katika  viwango vyote vya lugha yaani fonolojia, mofolojia na sintakisia.

Kwa sababu hii ni sawa kusema kuwa maana hujishugulikiwa katika tanzu za isimu Kama fonolojia ,mofolojia,na sintaksia .semantiki inakuwa ndio makutano ya taaluma nyingine

Semantiki kama taaluma nyingine ina mahusiano na taauma nyingine kama ifuatavyo katika mchoro na hatimaye katika maelezo yanayo eleza vipengele mbalimbali vya lugha:-

Mchoro kuonesha  mahusiano ya semantiki na vipengele vingine vya lugha kama sintaksia,mofolojia na fonolojia.Kuwepo kwa semantiki katikati inamaana kwamba tawi hili ni muhimili wa matawi mengine.

Isosceles Triangle: Semantiki
Oval: Sintaksia
 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 


 Fonolojia ni tawi la isimu ambalo hujishughulisha na uchunguzi na uchambuzi wa mfumo wa sauti katika lugha, huchunguza jinsi ambayo vitamkwa au sauti za lugha zinavyoungana ili kujenga maneno yanayokubalika katika lugha ya mawasiliano. Ili lugha ya mawasiliano iwe kamili ni dhahiri kwamba mpangilio wa sauti lazima uwe na maana ili kufikisha ujumbe, hivyo semantiki inauhusiano mkubwa na fonolojia.kwani katika fonolojia uweza kuangazia foni na kuziunganisha kupata kiseme kinacho zungumzwa na kuleta maana mfano wa foni zinavyotengeneza kiseme chenye maana,[b]+[a]+[b]+[a]= #baba#    [s]+[h]+[u]+[l]+[e]= #shule# sauti hizo zikiwa pwekepweke haziwezi kuleta maana ndipo ukaribu wa taaluma sauti na taaluma maana unapokutana.

  Mofolojia ni taaluma inayoshughulikia vipashio vya lugha katika kuunda maneno. Tawi hili la isimu huchunguzi na kuchambuzi wa maumbo ya maneno na jinsi maumbo hayo yanavyotumika katika lugha. Jukumu la mofimu husika katika sentensi hubainika vyema kulingana na uhusiano baina ya maneno mengine katika tungo. Maumbo ya kimofolojia huathiri vipengele vingine vya kisemantiki. Hivyo semantiki ina mahusiano na taaluma ya mofolojia kwa kuwa ili lugha iweze kueleweka lazima iwe na mpangilio na muundo mzuri wa vipashio vya sentensi ili kuleta maana katika mawasiliano.

Mfano:     Mwalimu anaimba

                     Walimu wanaimba

Katika mfano huu katika upande wa kiima kiambishi m kinaashiria  umoja na wa  inaashiri wingi,  katika upande wa kiarifu viambishi a katika upande wa kiima vinaashiria nafsi ya tatu umoja na wa vinaashiria nafsi ya tatu wingi, hivyo maumbo ya maneno lazima yawe na maana.

  Sintaksia, ni utanzu wa sarufi unaojihusisha na uchunguzi wa mpangilio wa maneno katika sentensi na uhusiano wa vipasho vyake. Utanzu huu huchunguza sheria  au kanuni zinazofuatwa katika kuyapanga maneno ili yalete maana inayokubalika na kueleweka katika lugha husika, . Kwa mantiki hii, kwa kuwa semantiki hushughulikia viwango vyote vya lugha, basi hushughulikia pia kiwango cha sintaksia ambapo huangalia maana za neno sentensi na tungo kwa ujumla kwani tungo lazima ikubalike kwa wazungumzaji pia tungo lazima ilete maana.   

         Kwa mfano,

Pana huimba vizuri akiwa mubashara

Mubashara huimba vizuri akiwa pana.

Vizuri huimba pana akiwa mubashara.

Katika mifano hii sentensi (1) inampangilio sahihi katika lugha ya Kiswahili hivyo inamaana na inawezesha mawasiliano, na sentesi zilizobaki hazijafuata mpangilio sahihi wa kimuundo wa  lugha ya Kiswahili hivyo hazina maana na hazifanikishi mawasiliano.

Kutokana na uwanja mkubwa wa semantiki imeweza kuibua  taaluma zingine ambazo zipo ndani ya semantiki nazo ni isimu ubongo na isimu jamii hivvyo tutaeleza isimu chache kwenye hii kazi kea sababu swali linataka tuangalie msingi wa semantiki katika taaluma zingine.

         Isimu ubongo ni tawi la isimu linalochunguza mahusiano kati ya lugha na michakato ya kiakili (ubongo) uzashaji wa matammshi katika ujifunzaji wa lugha msingi mkubwa katika tawi hili la isimu ni kuwa mchakato wa uzungumzaji huanza ktk akili ya mtu, hivvyo kinacho zungumzwa uleta mahusiano makubwa na semantiki ambalo uchunguza na kuchambua maana ya kile kinacho zungumzwa na msikilizaji unatambua maana ya kile kinacho zungumzwa na mtu kutoka kwenye ubongoni mwake.mfano juma amesafiri leo asubuhi.sentensi inapotoka akilini mwa mtu utengeza maana amboyo msikilizaji unatambua maana ya kile kinacho zungumzwa na mtoa kiseme.hivyo semantiki ni makutano ya matawi ya isimu katika lugha.

    Kwa mujibu wa Matinde R S akimurejelea Mathooko,P.(2000)  Isimu jamii.ni tawi la isimu linalochunguza namna lugha inavyotumika katika jamii kwa kuzingatia mazingira (muktadha) husika ambapo kile kinacho zungumzwa ni lazima kiendana na mazingira ambapo semantiki huusika kwa lengo la kuhakikisha kile kinacho zungumzwa kinaendana na mazingira (muktadha) kwa watumiaji na waweze kuelewana, mazungumzo baina ya watu uzungumzwa kwa kuzingatia maana ya kile kinacho zungumzwa.mfano juma anakamua mbuzi maziwa.muktadha wa zizini

                             Asha anakuna Nazi kwa kutumia mbuzi. Muktadha wa jikoni katika mapishi.hivyo neno mbuzi limetuka katika muktadha zaidi ya moja kwa kuzingatia muktadha inaleta maana ya kile kinacho zungumzwa.

 

Kwa ujumla semantiki ni tawi la isimu kama matawi mengine ya isimu ambalo haliwezi kujikamilisha lenyewe pasipo kuhusiana na matawi mengine ili kukamilisha mawasiliano. Lakini semantiki inaweza kutofautiana na matawi mengine kwa kuanza na tafsiri yake ambayo inajieleza na imetofautiana kabisa kidhima na matawi mengine ambayo ni fonolojia, sintaksia, na mofolojia. Pia dhima zake hazifanani na matawi mengine ya isimu.

 

           

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

MAREJEO

Habwe, J na P. Karanja (2004). Misingi ya Sarufi ya Kiswahili. Nairobi: Phoenix Publishers Ltd.

Massamba (2004) Anafasili dhana ya semantiki kuwa ni taaluma ya isimu inayojishughulisha na uchunguzi na uchambuzi wa maana za maneno na tungo katika lugha.

Massamba P. B. D (2004) Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha. Dar es Salaam: TUKI

Massamba, D.P.B na wenzake (1999). Sarufi Miundo ya Kiswahili Sanifu: Sekondari na Vyuo.                Dar essalaam: TUKI.

Leech, G (1981), Semantics, Harmondsworth: Penguin books limited hazel Watson &                                         veney Ltd.

Mofolojia

 

Comments

Popular posts from this blog

Information technology

MKATABA WA KUPANGA NYUMBA

Unominishaji,