TUNGO
TUNGO
Dhana ya tungo
Neno tungo ni nomino ambayo
hutokana na kitenzi tunga ambacho kina maana ya kushikanisha vitu pamoja kwa
kupitisha kitu kama uzi ndani mwake.
Hivyo basi tungo ni kuweka
pamoja au kupanga pamoja vipashio sahili ili kujenga kipashio kikubwa zaidi.
Tungo hujidhihirisha katika viwango vinne ambavyo ni:
a) Kiwango cha neno
b)Kiwango cha kirai
c) Kiwango cha kishazi
d) kiwango cha sentensi
hivyo basi kutokana na
viwango vya tungo tunapata aina nne za tungo ambazo ni
i. Tungo neno
ii. Tungo kirai
iii. Tungo kishazi
iv. Tungo sentensi
I.TUNGO NENO
Tungo neno ni tungo ambayo
huundwa na vipashio vidogo zaidi ya neno
ambavyo ni mofimu au fonimu.
Mfano;anacheza,kakimbia.
II.TUNGO KIRAI
Ni kipashio cha kimuundo
chenye neno moja au zaidi lakini ambacho hakina muundo wa kiima na kiarifu.
Kwa mfano;
a) Mtoto Yule
b) Mtoto Yule ni mzuri
c) Mzee huyu ni mjanja
d) Ajuza yuleni mwembamba
e) Kaka na dada
III. TUNGO KISHAZI
Kishazi ni tungo yenye
kitenzi ambacho chaweza kujitosheleza na
kukamilisha ujumbe uliokusudiwa na mzungumzaji au kuwa na kitenzi kisichoweza
kujitegemea chenyewe.
Tungo kishazi ni kubwa
kuliko tungo kirai lakini ni ndogo kuliko tungo sentensi.
Kwa mfano;
a) Mwanafunzi aliyesoma kitabu jana amefaulu mitihani
yake
b) Mwalimu alipoingia darasani alitugawia daftari zetu
c) Mama anapika chakula Baba analima shamba
d) Mwalimu anafundisha na wanafunzi wanasikiliza
e) Kaka anasoma kitabu na dada anaosha vyombo.
Aina za vishazi;
Kuna aina mbili za
vishazi nazo ni,
a) kishazi huru.
b) kishazi tegemezi .
A. KISHAZI HURU
Ni aina ya kishazi ambayo
hutoa taarifa kamili katika tungo,hubeba kitenzi kikuu au kishirikishi ndani
yake .kishazi hiki huwa hakihitaji maelezo ya ziada ili kukamilisha maana au
taarifa iliyokusudiwa na pia huweza kujitegemea kama sentensi kamili na huwa na
muundo wa kiima na kiarifu.
Mfano,Mtoto/anacheza
Mwanafunzi /anasoma kitabu.
Mwalimu/ ni mpole
B.KISHAZI TEGEMEZI.
Ni aina ya kishazi ambayo
huwa haitoi taarifa iliyo kamilibadala yake hutegemea kishazi huru ili
kukamilisha taarifa iliyokusudiwa na msemaji.kishazi hiki hutawaliwa na kitenzi
kisaidizi.kishazi tegemezi peke yake hakiwezi kutoa taarifa iliyokusudiwa.
Mfano wa vishazi ambavyo
havitoi tarifa kamili;
Mtoto unayemjua
Mwanafunzi anayesoma
Mahali alipoingia
Mama alipomchapa
Kaka aliporudi
Hivyo basi tunapoweka pamoja
vishazi huru na vishazi tegemezi taarifa iliyokusudiwa hukamilika kwa mfano;
Mwanafunzi anayesoma hapa ameondoka.
Kaka aliporudi alinifundisha.
Wakili msomi ameshinda kesi yake
Sifa za kishazi tegemezi
i. Hakikamilishi taarifa
pasipokuwepo na kishazi huru.
Mfano ;Mtoto anayecheza
mpira ameumia
Mama alipomkalibisha aliingia ndani
ii. kinaweza kikaondolewa
katika tungo bila kuathiri taarifa iliyokusudiwa.
Mfano;Mtoto aliyeugua
amepona
Mtoto amepona
Mama uliyemsalimia pale ameondoka jana.
iii.hutambulishwa na
vitambulishi vya urejeshi vinavyopachikwa katika vitenzi.
Mfano;Anayesoma,alichookota,uliokatika,iliyoibiwa
IV. TUNGO SENTENSI
Sentensi ni kifungu cha
maneno kuanzia neno moja na kuendelea chenye muundo wa kiima na kiarifu na
kinacholeta maana kamili.
Sifa za sentensi
i.Sentensi lazima iwe na
mpangilio wa maneno ambao unakubalika na
wazungumzaji wa lugha husika.
ii. Sentensi lazima
ikamilike kimaana,kimuundo na kisarufi.
iii. Sentensi lazima iwe na
muundo wa kiima na kiarifu.
iv. Sentensi inaweza kuundwa
na kitenzi kitenzi kikuu kimoja au zaidi.
v. Sentensi huonyesha hali
mbalimbali ,kama vile amri,ombi,mshangao
Comments
Post a Comment